Kwa waliomaliza form 4, kama una roho ndogo usiende kusoma special schools (shule za vipaji maalumu)

IPO nami nilibance nikaona hiyo imetiki sasa yeye anadai PCB nikamwambia haiwezekani kwa Sie wahenga A level 90s huko nikashangaa kuwa tcha wake amemwambia possible
Kama ni wa kike hizo points 10 anaweza kuchaguliwa PCB, wa kiume labda atasubiri second selection Au mpeleke private. Muache mtoto asome anachokipenda, kwanza CBG Haina dili Siku hizi

Pia anaweza kuchaguliwa CBG na akahamia PCB Kama Shule aliyopangiwa wanayo hiyo combination
 

Saivi unatusumbua kwenyejukwaa la Sports jamii,Kenge wewe
 
Kuna kichwa kimoja huwa nakikubali Sana huyu jamaa alikuwa vizuri kichwani alitutesa Sana pale mzumbe ...
Akaenda kibaha PCB huo mwaka 2007 akapiga div. One ya tatu ....dav mwasota alikuwa mwamba kweli kweli!
Nampata huyo Dr .Mwasota (MD)

Sent from my TECNO BE6 using JamiiForums mobile app
 
Bora wewe mi wakati naripoti form 5 nilikuta madogo ndo wanafundisha walimu yani mwalimu ndo anakula kipindi ananolewa nilibaki nashangaa na tranka yangu kichwani
🤣🤣🤣Acha fix mzee
 
Haha dah umenikumbusha mbali sana , kuna watu walikuwa na mikwara balaa ila baada ya muda mnakuwa sawa
 
Ndegeulaya alikua na kipaji cha kufundisha ila kuanzia O level mpaka advance alikimbizwa na wadau ambao walikua hawan kelele.
 
Alikua headboy wangu MKUU nimesoma nae O level na Na advance nimepiga nae yeye alipiga PCM Mimi nilikua napiga EGM tulikua tunakutana kwenye Pure mathematics.
Hivi ndege aliwahi kua headboy azania? mbona sikumbuki.
 
Broo umenikumbusha mbali pigo inaanza nafauli comb za science basi nikaanza kupiga mapindi nilikuwa bitozi san enzi hizo mapind sifiki pesa ya tuition naishia kulamba mademu...... basi nikapangiwa advance nikatimba maskuli fresh kufika nakutana na mwana mmja alikuwa pcb enzi hizo.....
Jamaa akanikuta nimelal kweny kitanda bwenini akanitukana dogo unazingua umekuja sayansi na unalal sa3 sijui alikuja bwenini kufanyaje lakin stor ndo ilianzia hapo.
Mimi sikujali sana nikaendelea kulala freshi siku ya pili akanikuta tena akasimama bwenini dogo boya huyu analala sa3 humu amekuja kusoma au laa niliogop sana sem nilikuwa mtukutu ...... badae nikaenda darasani nakutana na wanafunzi wana solve organic ma chandi nikapagawa nikasem nimeyatimba lakin nashukur mungu nili adpt mazingira nikaanza kukata mapindi
Pigo ikaenda jamaa alikuwa form six nikawa nasem daah huyu jmaaa anajua sana maan kulala kwake ni sa9 usik mimi nikijiona sa3 nimejitahid
Jamaa akapiga ascee matokeo kutoka amelamba 17 three nikakaa kitandani nilicheka mpka machozi sijui yupo wapi sasa ingawa mimi pia sikufany vyema nilipat dv 2
 
Bila shaka we umesoma Ilboru pale Nyumbani kabisa unaangalia Mount meru na hizo sifa za madogo kuulizana maswali mkiwa mmepumzika walikua nazo madogo wa Bweni la KIBO.😂
Mi nilitaka nihame Day one😂😂
 
Kwa tulipofika shule yoyote mtu anatoboa kikubwa jitihada tu, naheshimu special lakini elimu popote tu.
 
Matokeo ya ACSSEE yametoka, shule za vipaji hazijangusha kabisaa, ni full kuweka 1 kaliii afu nyingiii.
🔥🔥🔥
 
Hahahah hii nilipitia pia japo nilitoka na div I but nikilala huwa naota nipo advance huwa nalia maana physics ilininyanyasa sana nikiamka nacheki cheti changu nacheka sana na kulia kwa furaha.
Ile stress imenifanya hata kazini siwezi ku panic kwa lolote,i can handle anything in this life yaani siwezi kushindwa jambo nilikotoka ni mbali sana😁
 
Wahanga wakubwa wa nacte ni 2012 4m 4 na 2013 4m 6, lilipita gharika ikabidi warudie rudie kupachika pachika tu, wapo waliobahatika na wengine walilalia kuti kavu. Ndio ikaletwa BRN baada ya hapo ufaulu ni kupaa tu toka hapo mpka leo.
Prof Ndalichako hatosahaulika kamwe kwenye vichwa vya hawa watu
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…