Kwa waliopo Dar, wanahitajika shareholders

Kwa waliopo Dar, wanahitajika shareholders

flowerss

JF-Expert Member
Joined
Nov 25, 2017
Posts
640
Reaction score
591
Habari zenu wadau,

Poleni na kazi na mihangaiko ya maisha. Ninayo furaha ya kuwashirikisha kwenye Jambo la manufaa na lenye heri.

Kama Kichwa Cha habari kinavyosema, nahitaji watu jinsia zote wenye ari na uchungu wa maisha na mafanikio kwa ujumla ambao nitashirikiana nao kwenye miradi mbalimbali ikiwemo kilimo cha Greenhouse pia na ufugaji wa kuku wa nyama na kuku wa mayai.

Eneo tayari lipo Mbezi na lenye maji ya kutosha. Pia banda kubwa la kufugia kuku wa nyama na wa mayai lipo tayari.

KINACHOHITAJIKA:
Rasilimali watu kwa jili ya uanzilishi na uzalishaji na usambazaji wa bidhaa zitakazoanza kuzalishwa. Ili kufanikisha Jambo hili kwa yeyote mkazi wa Dar, njoo PM kwa maelekezo zaidi na kujua tarehe ya kikao cha kwanza.

Na baada ya idadi ya watu wanaohitajika kufika itapangwa siku ya kikao na kujadili jinsi miradi na Mambo mengine yatakavyokuwa.

Pia, kikao kitafanyika eneo husika la mradi kwa maana wadau wapate kufika na kuona eneo na baada ya hapo kikao kitafanyika hapo hapo ili utekelezaji uanze Mara moja baada ya kujadili na kuweka misingi imara.

Karibuni sana kwenye kufanikisha jambo hili. Pia lengo la kupenda kushirikisha wadau wengine zaidi ni kupanuana mawazo na kujenga network imara kwa kuanzisha miradi mbalimbali mbali na wazo tajwa.

Tukumbuke: UMOJA NI NGUVU.

KARIBUNI SANA.
 
ndugu hii ni lini
Hapa ndo mchakato wa kuwakusanya wadau kwa jili ya kikao cha kwanza ndo hatua iliyopo kwa Sasa.

Nà tayari wadau wameshaanza kuja inbox kwa jili ya maelekezo zaidi.
Karibu Pm.
 
Kila la heri!
Shukrani
Mchakato unaendelea Pm Aksanteni Sana wote mnaoendelea kujiunga na mchakato wetu . Tunatoa wiki moja zaidi ili watu wengine Zaidi wajiunge kwa jili ya kusudio tajwa hapo juu...

Group la whatsaap litaundwa ili kuwezesha kupata taarifa muhimu kwa wakati.
Aksanteni
 
Shukrani
Mchakato unaendelea Pm
Aksanteni Sana wote mnaoendelea kujiunga na mchakato wetu .
Tunatoa wiki moja zaidi ili watu wengine
Zaidi wajiunge kwa jili ya kusudio tajwa hapo juu..
Gro wup la whatsaap litaundwa ili kuwezesha kupata taarifa muhimu kwa wakati see
Aksanteni
Safi Sana! Umoja ni nguvu!
 
Safi Sana! Umoja ni nguvu!
Ni kweli kabisa.
Hakuna linaloshindikana kwenye umoja na hasa mawazo tofauti tofauti.
Ni Imani yangu kuwa tutaenda leta mapinduzi makubwa kwa Njia ya mshikamano.

Na viongozi watateuliwa miongoni mwa Wadau kwa maana Kila kitu kutakuwa Ni Cha kushirikishana.

Na hatimae tutasajiri.
Together as one!
 
Aksanteni.sana wadau mbalimbali mliojitokeza Pm na wengine mkaomba kutumiwa picha za eneo la mradi na nikaweza kutuma kwa waliohitaji kabla ya kikao.na wengine tutawasiliana kwa Njia ya whatsaap na kawaida.

Mawazo na mapendekezo yenu yanathaminiwa na kufanyiwa kazi.
Pia siku ya Jmos hii ndo siku rasmi ya kuunda group la pamoja ili Sasa kwa pamoja tupange siku nzuri ya kikao.

Eneo la kikao Kama ilivyoelezwa awali Ni pale pale eneo la mradi Na Ni Mbezi.
Baada ya kikao na kuafikiana Mambo ya msingi ndipo tutaanza rasmi miradi tukianza mmoja baada ya mwingine Kama Uzi unavyoeleza.

Karibuni.
 
Back
Top Bottom