Eiyer
JF-Expert Member
- Apr 17, 2011
- 28,259
- 20,891
Kinachonifanya niwatambue na kuwapongeza WANAWAKE wa ukweli ni jambo ambalo nimekua ninalishuhudia karibu kila siku kwa rafiki yangu mmoja.Huyu jamaa,baba yake ni mlevi sana,hajui wanae wanakula nini na wanalalaje. . . . . . . . . . . . . . . . . . . .Nilimuuliza yule jamaa yangu kuwa wapo kw kwenye maisha hayo kwa muda gani akaniamba kuwa ni muda mrefu umepita tangu baba yake aanze tabia hiyo,aliniambia ni miaka 15 sasa.Yeye baba huondoka asubuhi na hurudi usiku akiwa amelewa. . . . . . . . . . . . . . .. . . . . . . . . , . . . . . . . . . . . .Kijana ameniambia kuwa amekua akimsikia mama yake akimlalamikia baba yake kila asubuhi juu ya tabia yake ya ulevi.Mdogo wake wa mwisho jamaa yangu ana miaka 10,yani ina maana huyu amekua kwa nguvu ya mama peke yake,huyu mama ni mama lishe.Huyu mama ni mama hasa,ameweza kuilea familia pamoja na dume lisilokua na maana kwa miaka 15,sijui ataendelea na majukumu hayo kwa muda gani. . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . Nampongeza sana huyu mama,pia nawapongeza wanawake wengine wote wanaojituma kwaajili ya familia zao.Japokua ni wachache,nawapongezeni,lakini nawapa pole wanawake ambao wana wanaume wa hovyo kama huyu!