Kwa wamiliki wote wa magari ya Nissan tukutane hapa

Kwa wamiliki wote wa magari ya Nissan tukutane hapa

Boeing 747

JF-Expert Member
Joined
Mar 30, 2018
Posts
3,515
Reaction score
9,415
Heshima kwenu wakuu,

Binafsi ningependa kwa wale wote ambao wamewahi kumiliki au wanamiliki na wale wenye ndoto za kumiliki magari ya kampuni ya NISSAN tukutane hapa tubadilishane uzoefu kulingana na aina ya NISSAN unayomiliki au uliyowahi kumiliki.

Ingependeza utueleze gari hilo la nissan umelimiliki kwa muda gani na ni changamoto zipi za kiufundi umekutana nazo na ulizitatua namna gani.

Hii inaweza kutusaidia kuondokana na dhana kwamba magari ya TOYOTA ndiyo yanayofaa kwa Tanzania na si vinginevyo.

Tukubali kwamba kuna kampuni nyingi za magari tofauti na TOYOTA za Japan na nje ya Japan ambazo zinatengeneza magari mazuri sana kuliko hata yale ya Toyota ila shida inakuja kwa mafundi wetu wanatukaririsha kuwa toyota ndiyo gari bora.

Kwa kuanzia labda niorodheshe baadhi ya models za NISSAN ambazo zimekuwa common hapa Tanzania.
1. Nissan Patrol
2. Nissan Safari
3. Nissan Murano
4. Nissan Elgrand
5. Nissan Serena.
6. Nissan Fuga
7. Nissan Dualis
8. Nissan X-Trail
9. Nissan Skyline
10.Nissan March
11.Nissan Tiida
12. Nissan Note
13. Nissan Blue bird
14. Nissan Sunny
15. Nissan Caravan
16.Nissan Juke
17.Nissan Terano
18. Nissan Wingroad

Unaweza kuongezea Nissan nyingine ambayo sijaitaja hapo.

Karibu tubadilishane uzoefu.
images%20(4).jpeg


Sent using Jamii Forums mobile app
 
Nina swali kuhusiana na hii gari.

Kwa nini sokoni, kwa iliyotumika hapa nchini, Bei yake huwa chini sana??

Je huwa zinatatizo gani common hizi gari??
Mkuu sijawahi kumiliki Xtrail....waliowahi kuimili watatusaidia...
Ila ninachofahamu toleo la gari likishapitwa na wakati bei yake sokoni hushuka ili kufanya yaishe na kuruhusu toleo jipya kutawala soko

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Ni ghali ila siyo ghali coz ukifunga ni mkataba...kuna spea nilifunga kwenye nissan sasa hivi ina miaka mitatu imefunguliwa kukaguliwa ipo kama vile imefungwa juzi.

Sent using Jamii Forums mobile app
Tatizo spare moja ikiharibika mfuatano wa kuharibika vitu vingine nao unafuatano, unaweza kupata kichaa!

Yeah spare zake ukifunga huwazi tena!

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Kwa sasa gari yangu ni Nissan tu. Nikitoka Nissan ni gari za ulaya. Nimekuwa na Nissan Terrano 2, Nissan Note 2 na Xtrail. Pia naagiza Elgrand, dualis na Fuga Hybrid.

Ooohoo how I love Nissan! Riding is my passion...

Zipo stable barabarani, imara na spea ukifunga unasahau.

Tangu nihamie Nissan, no stress at all.
 
Tatizo spare moja ikiharibika mfuatano wa kuharibika vitu vingine nao unafuatano, unaweza kupata kichaa!

Yeah spare zake ukifunga huwazi tena!

Sent using Jamii Forums mobile app
Gari linaundwa kwa mifumo inayotegemeana kama binadamu. Kifaa fulani cha gari kikiharibika usipokibadilisha kwa wati, lazima kifaa kingine ambacho kipo kwenye mfumo huo kiharibike.

Ndiyo maana inashauriwa ukihisi sehemu fulani inagonga wahi kutatua kabla haijaambukiza sehemu nyingine..
Hii ipo kwa magari yote

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Namiliki Nissan Dualis, changamoto niliyopata na baadhi ya wamiliki ni Navigation System (Nissan Carwings) kuwa kwa Kijapan. Mpaka sasa hatujapata mtu ambaye anaweza kubadilisha language from Japenese to English. Otherwise gari iko vizuri sana
 
VQ35 engine...V6..very powerful....high performance...ni kama ndege ya chini
Usipokuwa makini na pedal ya mafuta...jiandae kurest in peace

Sent using Jamii Forums mobile app
Hapo kweny pedal ya mafuta sasa,[emoji3][emoji3][emoji3] mkuu huu mzgo kwanza barabaran adim sana....wacha tujichange mkuu

Sent from my SM-G920P using Tapatalk
 
Back
Top Bottom