Kwa wamiliki wote wa magari ya Nissan tukutane hapa

Kwa wamiliki wote wa magari ya Nissan tukutane hapa

Kuna Nissan Patrol moja Old Model nilipata kwa mzungu mmoja aliyekuwa anafanya research ya wanyama pori ..Yeye alilinunua DT Dobbie
Basi ikafika wakati anaondoka akaliuza kwa bei ya kishkaji sana ...sijawahi badilisha hata bolt zaidi ya kufanya service ya kawaida na kubadilisha Timing Belt

Juzi nasafiri nikamuachia jamaa yangu mmoja sasa sijui alipasulia wapi rejeta bila kujua akaendesha hivyo kilichotokea gari ilizima yenyewe kuja kufungua Bonnet ya gari engine imeoza yote kilicho baki salama ni cylinder head na block ..80% ya engine imekufa ..kuulizia sasa spare na kuifanyia overhaul niliishia kushika kichwa ,nilichofanya ni kutoa matairi nikalifunika mpaka majaliwa tena

Jamaa yangu mwenyewe maisha ya kuunga unga kama yangu ,mke wake mwenyewe sio mzuri maana ningemmegea kupunguza hasira basi ndio hivyo tena

Nissan ni gari nzuri sana ila isije ikaua kitu kikubwa lazima ulie.

Sent using Jamii Forums mobile app
[emoji16][emoji16][emoji16][emoji16][emoji1787]haaaahaaaa jus haaahaaa

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Mkuu sijawahi kumiliki Xtrail....waliowahi kuimili watatusaidia...
Ila ninachofahamu toleo la gari likishapitwa na wakati bei yake sokoni hushuka ili kufanya yaishe na kuruhusu toleo jipya kutawala soko

Sent using Jamii Forums mobile app

Mkuu kuna kitu cha toyota rav 4 old model au toyota ist old model,fasheni zake zimepita lakini bei zake show rooms hazijawahi kupungua,hapo imekaaje??
 
Unataka kunambia kuwa bega moja likiteguka basi na la pili hivohivo or?

Sent using Jamii Forums mobile app
Hapana ...kumbuka beaga la kushoto linashirikiana na viungo vingine vya kushoto....so sitaki kuamini kuwa ukivunjika bega la kushoto...mkono wa kushoto utakuwa na uwezo wa kubeba kitu vhochote kizito.....hii ni kwa sababu mfumo mzima wa mkono unaanzia begani mpaka kiganjani..

Hivyo hivyo kwenye gari...mfano bush fulani ikifa usipoibadilisha ugonjwa utaambukiza kifaa kingine cha karibu yake ambacho kwa kapamoja vinafanya kazi moja...


Sent using Jamii Forums mobile app
 
Mkuu kuna kitu cha toyota rav 4 old model au toyota ist old model,fasheni zake zimepita lakini bei zake show rooms hazijawahi kupungua,hapo imekaaje??
Hizo bei haipungui sana kwa sababu ya demand yake sokoni....
Kwenye biashara kuna kitu kinafanya kazi namna hiyo....high demand leads to high price

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Kwa sasa gari yangu ni Nissan tu. Nikitoka Nissan ni gari za ulaya. Nimekuwa na Nissan Terrano 2, Nissan Note 2 na Xtrail. Pia naagiza Elgrand, dualis na Fuga Hybrid.

Ooohoo how I love Nissan! Riding is my passion...

Zipo stable barabarani, imara na spea ukifunga unasahau.

Tangu nihamie Nissan, no stress at all.
Kwani Toyota usahau mkuu? Funga bush original! Spark plugs recommended na vyote uone kama hutasahau!
 
Hapo kweny pedal ya mafuta sasa,[emoji3][emoji3][emoji3] mkuu huu mzgo kwanza barabaran adim sana....wacha tujichange mkuu

Sent from my SM-G920P using Tapatalk
Hela ya mafuta ipo lakini au ndio vijana mnataka ku bling na mafuta ya efu 10/10
 
Back
Top Bottom