Kesi kama hii imemkuta rafiki yangu...yeye ana Nissan xtrail....mambo ya ushkaji yakamponza.
Kuna mshkaji wake akaja akamuazima gari jamaa akaenda Sehemu inaitwa mbuguni karibia na ukuta wa Magufuli...kumbe njiani kuna tatizo lilitokea rejeta ikawa inavijisha jamaa yeye akakanyaga mafuta tu...si unajua tena gari la kupewa, unalifanyia sifa.
Injini ikapata moto sana jamaa haelewi yeye na gia tu, kwa bahati akafika safari yake..anafika anataka kupaki gari likazima lenyewe...malaika alimuongoza hakuliwasha...akafanya yaliyompeleka kwa muda mrefu huku gari linapoa ila boya haelewi chochote.
Alipomaliza mishe zake akaja kwenye gari, kupiga jino moja gari likawaka..kama kawaida mzee na gia anafika tu home kwa mwenye gari, gari likazima...sasa hapa wote wawili walikutana vichwa maji...hawakujishughulisha kutafuta tatizo ni kwa nini gari limezimika..Ikawa usiku, ikawa asubuhi...mwenye gari akawasha ,likawaka akenda mtaa wa jirani kama Km 2 hivi akaeguza kurudi home wakati anaiacha barabara ya vumbi aingie kwenye lami gari ikazima na kulikwa na kamteremko pale so usukani ukafeli na brake zikawa ngumu gari likamshinda jamaa coz naye ni lena lena...likaserereka kwenye lami likagonga gari lingine ubavuni....wakaongea sijui walielewanaje...ila wakayamaliza..
Akaita break down kufikishwa garage mafundi kufungua bonnet engine imekaangika to the maximum...rejeta haina maji hata tone....wakamsimulia fundi tangu mwanzo kule mbuguni gari ilivyozima...akawaambia wangeongeza maji wangenusuru Injini..
Kulikuwa hakuna namna hata ya kureface cylinder head....
Jamaa akanunua injini nyingine maisha yakaendelea..from that day, anakagua maji kuliko kitu kingine kwenye lile gari.
Haya ni madhara ya kupeana gari na washkaji wazembe na mwenye mali kuwa mzembe kutokukagua gari mara kwa mara
Mimi huwa nina desturi...rafiki yangu ni rafiki yangu mimi...ila si rafiki wa mali yangu hata kama nimeinunua 750/=
Bongo tunarudishana sana nyuma kisa ushkaji usio na mashiko
Sent using
Jamii Forums mobile app