Kwa wamiliki wote wa magari ya Nissan tukutane hapa

Kwa wamiliki wote wa magari ya Nissan tukutane hapa

Nina Nissan Hardbody ya mwaka 1988....ilipaki toka 1996 mwaka huu 2020 nkanunua battery mpya nkafanya overhaul gari ikawaka nkashangaa sana....bado iko vzurii sana....

Sent using Jamii Forums mobile app
Hizi roho za paka mno.
Nna Nissan Datsun pickup ya engine ya TD27 Diesel model ya 1991.Nilinunuaga bei ya mbuzi kwa mwarabu mmoja wa mombasa mil 4 tu mwaka 2008 na alikua nazo mbili anauza zote zilikua double cabin.
Nikaikata yangu ikawa single cabin.

Kuna bro wangu nkamwambia achukue akasuasua sasa alivyo boya eti akaenda kununua kirikuu!mpaka leo anajuta kuiacha ile gari.
Napita nayo popote,4wd ya low ratio na high range,napanda nacho milima kukiwa na tope na mzigo wa maana nyuma.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Naomba msaada wenu wakuu, nilipeleka Nissan-X-Terra kule kwa dealer ambaeni D.T.Dobie ya zamani kuhusu gari kuonesha taa ya CHECK ENGINE kuwaka hata baada ya kuifanyia service!

Wakaniambia sababu kubwa ya hiyo taa kuwaka ni sababu ya grade ya Mafuta tunayotumia Kuwa ya chini ukilinganisha na yale ya ulaya ndio maana taa inawaka!! Je hiyo ndio sababu ya hiyo taa ya check engine kuwaka?
 
Naomba msaada wenu wakuu, nilipeleka Nissan-X-Terra kule kwa dealer ambaeni D.T.Dobie ya zamani kuhusu gari kuonesha taa ya CHECK ENGINE kuwaka hata baada ya kuifanyia service!! Wakaniambia sababu kubwa ya hiyo taa kuwaka ni sababu ya grade ya Mafuta tunayotumia Kuwa ya chini ukilinganisha na yale ya ulaya ndio maana taa inawaka!! Je hiyo ndio sababu ya hiyo taa ya check engine kuwaka?
Inaweza ikawa ni sawa kwa asilimia fulani....kwa sababu magari mengi ya Nissan yanachagua chagua mafuta....sasa kama mafuta ni ya low quality, yanaweza yakawa hayaungui vizuri, yakafanya oxygen sensor ichafuke sana...ndiyo upate hiyo ckeck engine ligh.

kwani wao walivyofanya diagnosis, walikuambia code iliyooatikana inahusu nini?

My be oxygen sensor au Maf sensor.
 
Back
Top Bottom