Kwa wamiliki wote wa magari ya Nissan tukutane hapa

Hizi ndio kero ambazo hutakaa uzipitie ukiwa na Toyota, unless ununue 2021 model iliotoka kiwandani mwezi huu halafu ikuletee shida
Nissan inataka ufuate preventive maintenance program yake kama wanavyoshauri nissan wenyewe, sasa wabongo wengi hawawezi kutokana na hali ngumu ya kiuchumi/ubahili na hapo ndipo toyota inapoonekana ni gari zuri kwa mazingira ya afrika maana yenyewe hata usipofuata maintenance kama walivyoshauri wenyewe toyota kwa kiasi kikubwa sana bado utadunda nayo tu. Yaani nissan ni sawa na mwanamke ambaye anataka mwanaume mwenye hela ambaye anaweza kumtunza kwa kiasi kikubwa. But toyota ni mwanamke ambaye siku una hela poa siku zimepungua poa tu unapata mapenzi kama yote. Kingine Nissan ni sensitive kwenye mifumo yake mingi lakini toyota siyo sensitive sana. Yaaan kikubwa kama mtu hayuko tayari kutoa hela kuihudumia nissan vile vitu inataka hii si gari ya kuwa nayo utaishia kuipa sifa mbaya tu wakati kumbe uwezo wako kiuchumi hauendani nayo. Mtu huna hela ya coolant origional ushazoea maji tena ya chumvi kisimani unategemea nini kwa Nissan lazima ikukatae tu, mtu ashazoea toyota plug za elfu 10 kwa moja twende, oil za kupima, na mafuta machafu ya oilcom twendeee
 
Hata toyota anaelekea hukohuko.

Toyota za sasa ni sawa na nissan.
 
Mkuu umeandika vizuri lakini toyota za siku hizi hazina tofauti na Nissan kimifumo...Tofauti kubwa inakuja kwenye upatikanaji wa spea na resale value.

Kwa mfano injini ya toyota Brevis haiwezi kuvumilia shida kama injininza BMS2000 zilizopo kweny GX100,110

Halikadhalika injini za Crown, Mark x 4GR,3GR,2GR haziwezi kuhimili shida na majanga kama BMS 2000...

Yaani hizo Injini mifumo yake haina tofauti na Injini za Nissan, tofauti kibwa ni mfumo wa VVTi ambao kwenye Nissan haupo.
 
basi huko tuendako toyota zitaanza kuchukiwa na wabongo maana wabongo kwa kupenda vya kunyonga hatujambo.
 
Lifestyle ya watu inafanya hata magari yanayotengenezwa yaendane na uhalisia wa maisha ya watu.

Gari za sasa 80% ni hybrid.

Mifumo stand alone inaanza kuondoka mf. Petrol au diesel tu. Unakuta sahivi ni petrol hybrid au diesel hybrid.

Miaka 10 ijayo itakuwa ngumu kuagiza gari la petrol au diesel tu. Lazima hybrid iingie hapo.
 
basi huko tuendako toyota zitaanza kuchukiwa na wabongo maana wabongo kwa kupenda vya kunyonga hatujambo.
Ni kweli na ndiyo maana utakuta watu wengi wanalalamika Injini za brevis kimeo...D4 ile wabongo hawajua namna ya kuitunza..
 
Sure..
Ulaya na America kwa sasa ni mambo ya hybrid cars...

Hapa kwetu bado mtu anaagiza Rav Masawe yenye 3s..[emoji41][emoji41][emoji41]
 
Nissan
Nissan Pathfinder
 
Kwa kifupi tu Toyota anakusalimieni kwa salamu ya jamuhuri ya muungano! “Anasema acha ruti ziendelee”🤩🤩🤩
Nissan ni slay queen tupa kulee
 
basi huko tuendako toyota zitaanza kuchukiwa na wabongo maana wabongo kwa kupenda vya kunyonga hatujambo.
Hamna uzuri Toyota hakurupuki! Zitatoka Hybrid za makampuni mengi ila utashangaa ya Toyota inadumu mda mrefu zaidi!

Sahizi gari za kuchaji zinashika kasi sana dunia ya kwanza ni kama new evolution of cars. Wengi wanatumia lithium ion batteries ila shida kubwa ni low mileage na wear and tear timeframe. Zinachoka haraka na zinaenda umbali mfupi at full charge huku zikitaka masaa mengi kwenye charge!

Toyota alikuwa anafanyia utafiti Solid state battery technology na ndio ambayo atakuja nayo 2025 ambako wengi watakuwa washaangukia pua na ma lithium ion battery yao! Anakuja na gari ambayo itakupa convenience kama tu kukaa kwenye pampu ya petroli. Dakika 10 from 0-80% of charge kisha utembee kilometre 500 hivi kwa kila charge moja! No heating issues very safe and excellent endurance and performance battery!

Toyota amechelewa kwenda full electric ila nina hakika gari yake akitoa walioteseka kwengine kote watahamia huku!
 
Sure..
Ulaya na America kwa sasa ni mambo ya hybrid cars...

Hapa kwetu bado mtu anaagiza Rav Masawe yenye 3s..[emoji41][emoji41][emoji41]
Na hawa mafundi wakiendelea kukaza shingo wajanja wachache watatumia huo mwanya.
 
Na hawa mafundi wakiendelea kukaza shingo wajanja wachache watatumia huo mwanya.
mkuu tatizo mafundi wetu hawapendi kujiendeleza huko youtube kuna mavideo kama yote kuhusu ufundi wa magari lakini mwambie fundi link hiyo upate shule atakwambi shule ya nini
 
mkuu tatizo mafundi wetu hawapendi kujiendeleza huko youtube kuna mavideo kama yote kuhusu ufundi wa magari lakini mwambie fundi link hiyo upate shule atakwambi shule ya nini
Dogo akishanunua set ya box spanner, ameshamaliza maisha...hataki kusogea zaidi ya hapo..[emoji3][emoji3]
 
Bora watie moyo wanaotamani kununua wanunue wasiogope maneno
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…