Nissan Note mwenye uzoefu nazo??
Nimeimiliki kwa miaka mitano...naweza kusema yafuatayo.
UZURI WAKE.
1.Nafasi ya kutosha ndani.
2.Consumption ya kawaida highway unapata mpaka 14 to 15 km/L
3.Key less entry/ignition
4.Siti za nyuma zinajikunja hivyo unaweza kupata room kubwa zaidi ya mizigo..
5.Ina balance ya kutosha hata ukiwa above 120kph....nadhani hii inasaidiwa na kuwa na wheel base kubw ukilinganisha na IST au vitz.
6.Inavaliana spea na Nissan tiida, Nissan wingroad, baadhi Nissan march,Nissan AD van, Nissan Suuny na baadhi kwenye nissan bluebird zote zikiwa za miaka ya 2009 kurudi nyuma.
7.Inachanganya haraka coz ina body ndogo na injini ni cc 1500.
8. Ukilitunza unasahau kama kuna maeneo yanaitwa garage.
9.Ni gari ndogo ila ipo comfortable
10.Inamudu safari ndefu bila shida.
11.Driving experience yake inanoga sana the way walivyo design steering system yake.
UDHAIFU WAKE..
1. Spea ni ghali kulinganisha na toyota ila ukifunga ni mkataba.
2.Ina HR 15 engine ambayo inatumia umeme mwingi hivyo umakini na ustaarabu unahitajika.
3.Mafundi wanaziogopa....baadhi..
4.Kama ujuavyo nchi yetu imejenga dhana Toyota ndiyo gari , simshauri mtu anunue Nissan yoyote endapo upo nje ya Dar, Arusha,Mwanza,Tanga,Moshi na angalau Mbeya....utapata taabu ya spea....binafsi nipo Chuga so spea zote napata hapa original na fake pia zimeanza kuingia.
5. Ina CVT gearbox ambayo inatumia Cvt fluid ya Nissan NS 2 lita 4 hapa Arusha inauzwa 140k.....ukiweka tofauti na hiyo imekula kwako..
6.Madhaifu mengine ni yale yale ya kawaida yanayotokea kwa magari mengine mfano bush kuisha kutokana na hali ya barabara zetu za kizalendo
7.kwenye injine usije ukaweka zile plugs za 6400/=
Plug zake Og iridium ndefu nyembamba moja 30000 to 35000/ mkataba wa km 25000+
Generally, ni gari nzuri ukitii mashart yake itakupa fadhila.