Kwa wanaoamini uumbaji wa Eden, wanyama wala nyama waliumbwa wakiwa wanakula nyama?

Kwa wanaoamini uumbaji wa Eden, wanyama wala nyama waliumbwa wakiwa wanakula nyama?

Katika bustani ya Eden, wanyama wote walikuwa wanakula chakula kingine kisichohusisha nyama. Hapa kuna maelezo ya kinagaubaga kuhusu chakula walichokuwa wanatumia:

Wanyama Waliokuwa Bustani ya Eden:
  • Simba, Chui, na Fisi: Walikuwa wanakula mimea, matunda, na majani.
  • Chatu: Alikuwa anameza matunda na mimea kama kitoweo chake.
  • Mamba: Alikuwa anakula samaki na mimea ya majini.
  • Ndege: Walikuwa wanakula mbegu,matunda, na miche ya mimea.
  • Samaki: Samaki walikuwa wakila mimea ya majini na samaki wadogo.
Katika Bustani ya Eden, hakuna wanyama waliokuwa wanakula nyama kwani mazingira yalikuwa ya amani na ushirikiano.
Umewapendelea Mamba na Samaki. Yaani sisi wengine tushindie nyasi kama Wanyaturu halafu wao wanakula vitoweo vya baharini. Kwani Samaki na Samaki wadogo wao waliandikiwa kifo tangu uumbaji??
 
Waliumbwa hivyo hivyo wakiwa wanakula nyama na kuraruana au kula nyama za wenzao kulianza baadaye?
Simba, Chui, Fisi na wanyama wengine wala nyama walikuwa wanakula nini katika bustani ya Eden?

Chatu alikuwa anameza kitoweo chake katika bustani ya Eden?

Mamba alikuwa anakula nini??

Ndege wala nyama na samaki walikuwa wanakula nini?
 
Mbona inaeleweka.

Hapo mwanzo vyote vilikuwa vinakula miche ya kondeni yote yenye tunda na Mbegu kama chakula chao. Mwanzo 1:29-30.

Maisha ya Eden yalikuwaje?
Isaya 11:6-9 inaeleza ilivyokuwa na itakavyokuwa wakati wa Mbingu na nchi Mpya kwamba Simba atakula majani kama mwana kondoo na ndio ilivyokuwa. Wanyama wote walikula Majani kama chakula chao including wanyama wa Majini.

Baada ya dhambi na anguko la Mwanadamu tunaona kuna uumbaji mwingine unatokea.
1. Mwanamke kuzaa kwa utungu(Zaidi ya Uchungu)
2. Ardhi kuotesha miiba ambayo haikuwepo mwanzo.
3. Kuumbwa kwa wadudu ardhini wana decompose. (Sijapata lugha nzuri ya kiswahili)
4. Nyoka kuondolewa miguu yake. Alikuwa na miguu 4 kwa kulingana na baadhi ya vitabu(Abrahamic Text)
5. Kila alacho nyoka hata umpe nyama atahisi anaingiza vumbi mdomoni (Sijajua nielezeje nieleweke)
6. Wanyama kufungwa kuongea lugha inayoeleweka na wanadamu kwani mwanzo walikuwa wanaongea na kuelewana kama ambavyo nyoka aliongea na Hawa.
7. Wanadamu kuingiwa na hofu juu ya wanyama waliotiishwa kwake(Uadui)

Baada ya kutoka kwenye gharika, Mungu anawapa Nugu na wanawe pamoja na wanyama wengine chakula kingine. Yaani "Nyama" ila anaambiwa asile "nyama pamoja na damu yake" ila akapewa na angalizo kuwa kila damu au uhai wa mnyama au binadamu inayomwagwa na mnyama au binadamu itadaiwa.

So tuna conclude kuwa hapo "mwanzo wanyama wote walikula Miche yenye mbegu na matunda yenye mbegu ndani yake"
Inabidi ujizime data na kupachikwa ubongo wa roboti la Nape ili uweze kuamini stori hii
 
Simba, Chui, Fisi na wanyama wengine wala nyama walikuwa wanakula nini katika bustani ya Eden?

Chatu alikuwa anameza kitoweo chake katika bustani ya Eden?

Mamba alikuwa anakula nini??

Ndege wala nyama na samaki walikuwa wanakula nini?
Mkuu Yoda Je Adam akiwa kwenye bustani alikuwa anakula nyama za wanyama wanyama mbalimbali na vegetable?
Jibu ni hapana, binadamu kula nyama waliruhusiwa baada ya gharika ndipo walipo ruhusiwa,
 
Hapo Mwanzo kulikuwa na Darkness/kiza/Giza, Maji na the Great god, Bumba.

Siku Moja alijipata tumbo likimsokota, Kisha akatapita Jua,

Jua likakausha Maji, Ardhi/land ikatokea,

Kisha akatapika Tena, Crocodile/mamba, mjisui, Simba, chui na wanyama wengi wakatokea.

Kisha akatapika Tena , Akatokea Mtu/binadamu/Homo Sapiens.

Hii ni creation Myth ya bushongo people kutoka Central Africa.


Creation Myth , zipo nyingi sana.

Hiyo bustani ya Eden, mojawapo.


Ni katika harakati tu za homo sapiens kujitafuta, Nini yote haya, tumetoka wapi, origin-beginnning Universe,
Floods, Earthquake, Solar Eclipse, Solar system, Galaxy,Lunar Eclipse, Meteor's, disease, genetic disorder, death,life.n. k

Na kwa kiasi kikubwa Hatua zimepigwa kubwa, kulinganisha na Miaka ya nyuma /Karne za nyuma za akina Bishop Ussher ambao walidai ulimwengu uliuumbwa Saa sita mchana October 22 ,4004 B.C

Sasa mambo mengi yanamajawabu yake na uelekeo Bora kwa mengine.

Mwisho,The Universe(Matter , Energy,Space)is the Ultimate free Lunch.
 
Back
Top Bottom