Kwa wanaoifahamu Zambia; Msaada tafadhali nahitaji kwenda kufanya biashara huko

Mwamba028

JF-Expert Member
Joined
Nov 15, 2013
Posts
4,595
Reaction score
3,670
Heshima kwenu Mabibi na Mabwana.
Mimi nilishakaa pale boda ya Tanzania na Zambia kwa miezi kadhaa kwa ajili ya shughuli za ujasiriamali, na katika kuwa kwangu pale kuna mtu nilikutana nae na akanambia kule Zambia kuna fursa nyingi tu za biashara kwa kuwa bidhaa nyingi za Zambia zinatokea Tanzania japo hakunielezea kwa undani ila alinambia bidhaa km mafuta,unga,sabuni zinaenda sana kule
Sasa kama kuna mwenye taarifa za kutosha na jinsi ya kupeleka biashara na kupata fursa uko Zambia atuekee hapa ili tupate pa kuanzia,
Mchango wako ni muhimu sana mana ajira imekua zoezi
Natanguliza shukrani Wakuu.
 
Na pia pesa ya Zambia iko chini kuliko ya Tanzania, jamaa alinambia ukiend Zambia na milion 3 za ki Tz unakua na pesa nying sana kule, so mwenye mchanganuo mzuri tafadhali.
Nawasilisha
 
Mkuu, umenifanya nimekimbilia uzi wako kumbe sifuri tu.
 
sasa kwanini usingemuuliza huyo jamaa wa zambia akueleze kiundani
 
sasa kwanini usingemuuliza huyo jamaa wa zambia akueleze kiundani

Jamaa alikua safarin hivyo hakua na muda mrefu,na baada ya muda nikawa simpati kwenye simu
 
Mwamba028 jamaa wasikukatishe tamaa. Fursa ni kweli zipo. Mathalani ulipeleka hizo bidhaa unauza sana tu. Sasa ukipata pesa ya Zambia (Kwacha) unarudi nayo boda. Unabadirisha kuwa Tsh yaani unapata faida ya pili. Au unanunua USA Dola maana Zambia Dola iko chini kidogo. Kisha ukija Bongo unauza hizo Dola unapata mkwanja wenye faida. Unachukua tena bidhaa unapeleka Zambia. Maisha yanaenda! Halafu kuna viazi pori fulani vinaitwa chikanda kwa kizambia. Huko wanavipenda sana. Bongo hatuvitumii. Vinachimbwa maporini. Bongo vipo sana. Kazi kwako kamanda!
 

Pamoja sana Kamanda, ss ndo nlitaka nijue ni bidhaa gani haswa na uuzaji kwa kule ukoje,ikiwezeakana nipate mtu ambae anafanya au ashawahi kufanya anipe mwanga zaidi.
Ila shukran sna kwa mchango kaka
 
ngoja tusubili wadau waje kutupa habari napia kuhusu fursa zinazopatikana Congo kama kuna mdau anaweza kutujuza fursa zilizopo itakua ni vyema sana
 
tukaangalie fursa huko kwa watu

umenikumbusha wakati tunavuka boda hilo tunduma kwenda nakonde.....kwa sasa sjui huko kuna fursa zipi ila kipindi cha nyuma tulikuwa tuna fata skrepa kuleta huku tanzania.....ila badaye mchongo ukaja haribika
 
Habari za mchana wakuu,naamini sote ni wazima wa afya na tunaendelea na majukumu ya kulijenga taifa,leo nimekuja kwenu kupata information zozote kuhusu fursa za watanzania kwenye nchi ya zambia kwangu nime plan kuanzia mwezi wa kwanza mwakani niwe napeleka bidhaa za culture hususan viatu vya kimasai ugumu ninaoupata sasa sijajua mazingira yake yakoje na wala nitafikia wap maana sina ndugu wala jamaa ninae mfahamu yupo kule msaada wenu tafadhali wowote wenye information
 
Kwani unataka kuanza biashara bila ya hata utafiti mdogo? Sasa hizo product zako umejuaje kama zitauzika?
 
Kwanini unataka kwenda kuuza bidhaa za culture na hasa viatu vya kimasai na si bidhaa nyingine?
 
Kwanini unataka kwenda kuuza bidhaa za culture na hasa viatu vya kimasai na si bidhaa nyingine?
Bidhaa zingine zitafata baada ya kuona mazingira ya kule...kuhusu kazi za culture ndo ninazojishughulisha nazo mda huu na nahitaji ku expand market
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…