Kwa Wanasheria Tuu, Mtu Akihitajika Mahakamani Kutoa Ushahidi, Anaweza Kukataa?

Kwa Wanasheria Tuu, Mtu Akihitajika Mahakamani Kutoa Ushahidi, Anaweza Kukataa?

GenuineMan

JF-Expert Member
Joined
Jun 13, 2017
Posts
7,885
Reaction score
18,636
Wanasheria na Mawakili Wasomi
Mtusaidie sisi mbumbumbu wa Sheria.
1.Mtu Akihitajika mahakamani kutoa ushahidi je, analazimika kwenda?
Na akigoma kwenda kuna kosa.?

Au akitoa sababu labda ni mgonjwa au sababu nyingine yoyote, kesi itasimama kumsubiri au itaendelea?

2. Na je huyo mtu akiwa ni kiongozi mkubwa kama waziri mkuu au Rais , nae inakuwaje?
Rejea Kesi inayoendelea Jamhuri vs Lissu.
 
Kwenye case ya jinai shahidi hawezi kugoma. Kama ni mgonjwa case itaahirishwa au ushahidi kuchukuliwa kwa kiapo (witness statement).

Kwenye viongozi mfano Rais halazimiki kutoa ushahidi ni akiamua kukubali mwenyewe. Kwa hivyo move ya kujaribu Rais awe shahidi wako ni siasa tu hata Lissu anajua kwa sheria zetu hilo haiwezekani.

P.s. Logically shahidi anatakiwa kuwa upande wako! Sasa ikiwa shahidi hataki kutoa ushirikiano hata akija atakuharibia tu case.
 
Wakati mwingine unaweza kukataa au hata kukimbia kabisa! ili tu kuficha aibu (iwapo huo ushahidi unaokwenda kuutoa ni wa uongo)
 
Ni Kosa Kisheria tena Sheria inasema hakimu au Jaji anaweza kukuweka ndani shahidi hadi siku kesi itakapokuja tena ili utoe ushahidi wako Sheria ya Mwenendo wa Makosa ya Jinai Criminal Procedure Act (CPA) R.E 2023 inasema ukikataa na mahakama ikajiridhisha kuwa umekaa utakamatwa ili utoe ushahidi huo
Soma Section ya 147 CPA
IMG_3097.jpeg
 
Wakati mwingine unaweza kukataa au hata kukimbia kabisa! ili tu kuficha aibu (iwapo huo ushahidi unaokwenda kuutoa ni wa uongo)
Usipopatikana yale maelezo uliyoyaandika Polisi automatically yatapandishwa na kama mabaya basi yatamuumiza mshtakiwa pale hakuna wa kumuuliza maswali ya cross examination ili ajichanganye.
 
Back
Top Bottom