Kwa wanasiasa tulionao, Tanzania hatuwezi kusonga mbele

Kwa wanasiasa tulionao, Tanzania hatuwezi kusonga mbele

Chagu wa Malunde

JF-Expert Member
Joined
Jul 11, 2015
Posts
8,734
Reaction score
5,750
Taifa letu limetokea kuwa la ajabu sana tumekuwa na wanasisa wa ajabu ambao hawana mikakati ya kuwasaida wananchi.

Wananchi nao wamekuwa watu wa ajabu wanadanganywa kama watoto wadogo ambao wakipewa zawadi ya peremende basi wao husahau shida zote.

Sijaona mwanasiasa ambae yupo serious na hali duni ya maisha wanayoishi Watanzania. Watanzania wana maisha duni, kula kwa tabu, ajira za tabu, elimu duni na zisizo na tija.

Lakini wanasiasa wanawadanya wananchi kwa kuweka Concert za music na kuwalaghai wananchi kuwa watawasaidia huku tukiwa hatusikii mkikakati ya kukomboa maskini wa taifa hili.
 
CCM yako na mfumo kandamizi kuwafanya wanasiasa wengi wanafiki.

Tukisema Katiba mpya itaondoa hawa wanasiasa uchwara hamtak mnatuona kama wahaini au foreigner. It's going to be very tough.
 
Mkuu umesema kweli, watanzania ni watu wa ajabu kweli. Kila mtu ni mliaji tu; wanasiasa wanalia tu, wananchi na vilio tupu, wasomi wetu nao midomo juu kulia tupu, great thinkers wa JF nao ni vilio tu. Wewe mleta mada nawe umeona tatizo, ukaja JF kulia bila kuwa hata na chembe ndogo ya kusidia kutatua tatizo!

Kama ni hivyo basi tuendeleeni kulia matatizo yetu labda utafika wakati nature itasaidia kuyatatua.
 
..Sgr, tieglers, ndege, ndio muarubaini wa matatizo yetu. Uchumi utapaa miradi hiyo ikamilika. Hapa Kazi Tu.
Nafikiri unatania ndugu yangu. Kama tutaendelea kuikumbatia chama hiki chakavu cha CCM, tutasubiri sana. Ni mataifa machache yaliyobahatika kuwa na mali asili kama Tanzania lakini kama wahenga walivyowahi kusema...a fool and his money are soon parted!
 
Nafikiri unatania ndugu yangu. Kama tutaendelea kuikumbatia chama hiki chakavu cha CCM, tutasubiri sana. Ni mataifa machache yaliyobahatika kuwa na mali asili kama Tanzania lakini kama wahenga walivyowahi kusema...a fool and his money are soon parted!

🤣🤣
..niliamua kuwa MFARIJI.
 
Bila kuiweka pembeni ccm tutendelea kulia tu ktk nchi hii

CCM ndiyo kirusi kibaya kuzidi hata korona.
 
hatusikii mkikakati ya kukomboa maskini wa taifa hili.
Ungezungumzia hili mada yako ingependeza sana, na kwa mara ya kwanza nigetambua kwamba sasa akili zimerudi kichwani baada ya kuzikodisha mahala.

Toa mifano ya mikakati hiyo tuanze kujadili mada yako.

Mada yako nzima unalalamika tu, bila hata kusema ni kipi unakilalamikia mbali ya hao viongozi unaolalamika juu yao.
 
Mkuu umesema kweli, watanzania ni watu wa ajabu kweli. Kila mtu ni mliaji tu; wanasiasa wanalia tu, wananchi na vilio tupu, wasomi wetu nao midomo juu kulia tupu, great thinkers wa jf nao ni vilio tu. Wewe mleta mada nawe umeona tatizo, ukaja jf kulia bila kuwa hata na chembe ndogo ya kusidia kutatua tatizo!
Kama ni hivyo basi tuendeleeni kulia matatizo yetu labda utafika wakati nature itasaidia kuyatatua.
Umeandika kama unatania, lakini ukweli wenyewe ndio huo uliouweka wazi.
 
CCM yako na mfumo kandamizi kuwafanya wanasiasa wengi wanafiki...
Tukisema Katiba mpya itaondoa hawa wanasiasa uchwara hamtak mnatuona kama wahaini au foreigner... it's going to be very tough.
Sawa tunakubali CCM chama kandamizi. Hebu sasa tuambie ni chama gani mbadala tunaweza kukiamini.
 
Sawa tunakubali CCM chama kandamizi. Hebu sasa tuambie ni chama gani mbadala tunaweza kukiamini.
Tatizo ni kwamba CCM imeng'ang'ania madaraka na haiko tayari kutoa nafasi kwa chama chochote kuonesha uwezo na sifa ambazo zimekuwa nudra kwa CCM. Utajuaje uwezo wa mchezaji kama hauko tayari kumpa hata nafasi ya kuingia uwanjani?

Wapo waliozaliwa CCM ipo, wanakua CCM ipo, wanaanza shule CCM ipo, wanamaliza shule CCM ipo, wanatafuta ajira CCM ipo, wanaoa/kuolewa CCM ipo, wanapata watoto CCM ipo, wanazeeka CCM ipo...

...
Wanastaafu CCM ipo, wanapata wajukuu CCM ipo, wanakufa CCM ipo, wanazikwa CCM ipo, surely this borders on insanity! Halafu wapo wapuuzi wanadai eti wanaotaka kuwatoa madarakani wana uroho wa madaraka.

Halafu baada ya miaka yote hiyo CCM hiyo hiyo ndio iwe tumaini na tegemeo letu Watanzania kupiga hatua na kusonga mbele...! Yaani CCM hii hii, kweli Watanzania tuna hasara.
 
Ungezungumzia hili mada yako ingependeza sana, na kwa mara ya kwanza nigetambua kwamba sasa akili zimerudi kichwani baada ya kuzikodisha mahala.

Toa mifano ya mikakati hiyo tuanze kujadili mada yako.

Mada yako nzima unalalamika tu, bila hata kusema ni kipi unakilalamikia mbali ya hao viongozi unaolalamika juu yao.
Tatizo sio wewe kama wewe. Tatizo ni uwezo wako mdogo wa kupambanua mambo. Akili ndogo uliyonayo ndio ndio inakufanya uwe zuzu wa kutupwa.

Kuna mtu kalalamika? Ulitaka uambiwe kuwa kuna upungufu wa madarasa na ukosefu wa maji safi ndio upate mwanga wa kuchangia?
 
Wanasiasa wanao lobby tusipate chanjo ya Covid wakati madhara yake tumesha yaonja.
 
Tatizo ni kwamba CCM imeng'ang'ania madaraka na haiko tayari kutoa nafasi kwa chama chochote kuonesha uwezo na sifa ambazo wewe huna tena? Utajuaje uwezo wa mchezaji kama hauko tayari kumpa hata nafasi ya kuingia uwanjani?

Hata pale wananchi wanapoamua kuwapa wewe kwa kutumia vyombo vya dola unakataa kata kata maamuzi yao kwenye sanduku la kura? Uko tayari kuua au kuiba uchaguzi mradi hao wengine hawapati nafasi ya kuonesha uwezo wao?
Mkuu upo serious kabisa chama kama Chadema kipewe nafasi kuongoza nchi yetu? Hata kama ni ni kuwapa nafasi waonyeshe uwezo?
 
Back
Top Bottom