Kwa wanaume mnaotafuta wanawake humu

Kwa wanaume mnaotafuta wanawake humu

kaka km

JF-Expert Member
Joined
Nov 16, 2013
Posts
1,336
Reaction score
686
Kwa wanaume mnaotafuta wanawake humu,naomba kujua mnakabiliana na changamoto gani huko nje hadi mje kutafta mabinti humu?

Maana sielewi inakuaje hadi unakosa mwanamke huko unakoishi hadi unakuja kulia humu kwamba upweke unataka kukuua.

Mbona mabinti ni wengi sana na wanapatikana kwa urahisi au mimi tu ndio naona hivyo? Tatizo ni nini?

je;
1. Mmekosa sifa za mabinti mnaoishi/kusoma /kufanya nao kazi?
2. Mko bize sana na kazi/shule hadi mnakosa muda wa kusocialize na watu[wanawake] hadi kuwapata?
3. Mabinti hawapatikani huko mnakoishi[wachache na wameshachukuliwa na wengine]?
4. Hao mnaoishi,soma au kufanya nao kazi hawana vigezo vyenu?
5. Udomo zege?[kama ndio hivyo hizi mitandao zisingekuepo mngefanyaje?mngebaka?

Kwa kweli sielewi hasa mwanaume unakosaje binti huko hadi uje kulia upweke hapa. Kumbuka: simaanishi kwamba wa humu hawafai au hawatakiwi,ndio hao hao tunaoishi nao.
 
Mkuu nashukuru sana kwa kuuliza hili swali maana huwa najiuliza kila siku.....ndio maana huwa nashawishika kuamini kwamba wengi wao ni matapeli hawana shida ya wachumba wala wasebule

Kwa kweli sielewi mtu anakosaje mke/mpenzi huko kwenye maeneo yake,mi naona wanawake wapo wa kutosha,wenye sifa zote,wa kila aina,mtu anakosaje?

Juzi hapa niliamua kutembea tembea maeneo ya watu,nikashangaa kukuta hata watoto wakali na wa maana wanapatikana hata uswazi,nikajiuliza watu wanakosa nini?mbona uswahilini kuna watoto wa maana hata kuliko wa maofsini,na wanapatkana kwa garama ndogo?
 
It is always interesting to meet some one new you never met before! Inachosha sanaa kutoka na watu unaowajua sababu unawajua tayari si loloye si chochote hawana jipya!

Huyo wa kwenye mtandao pia ukishamzoea unamuona the same as unavyomuona wa mtaani au sehemu ya kazi unles otherwise u a luking for one night stand.
 
Hapa ni pazuri sana kupata rafiki, mpenzi, mke au mume kwasababu hakuna aibu ya waziwazi atakayoipata mtu anapokataliwa kwasababu yoyote ile. Hii ni sehemu nzuri ya mawasiliano na tunaojadili humu ndio watu tuliokaribu pamoja na kwamba hatuonani wala kujuana kiundani ila kwa michango tunafahamiana. Humu kuna watu wanamichango inayoonyesha wanabusara na wanaweza kuishi na mtu yeyote na kuwa na maisha mazuri. Ila wengine wanajionyesha jinsi walivyo viazi au na tabia mbaya kwa michango yao pia. Mi naona ni sahihi kutafuta mwenza popote unapopata nafasi iwe kazini, mtandaoni, safarini, shuleni, barabarani, kanisani, harusini, mkutanoni, bungeni na hata msibani.
 
Mkuu nashukuru sana kwa kuuliza hili swali maana huwa najiuliza kila siku.....ndio maana huwa nashawishika kuamini kwamba wengi wao ni matapeli hawana shida ya wachumba wala wasebule

Nashukuru mkuu kwakuongea pointi
 
Swali la kitoto hili....online attraction is very unique...ina involve zaidi personality na brain...mtu anakuvutia kwa anayoyaongea akiwa very free since yuko anonymous....hujui huyo mtu ni professa au ni Secretary ..mtaani utam judge mtu na kabila lake au kazi yake..Attraction is not a choice
 
Huyo wa kwenye mtandao pia ukishamzoea unamuona the same as unavyomuona wa mtaani au sehemu ya kazi unles otherwise u a luking for one night stand.
Not necessarly HE COMES FROM DIFF BACK GROUND REMEMBER! Hawezi kuwa sawa kimtazamo na sie! TO FREE YOURSELF FROM VICIOUS CYCLE OF POVERTY YOU NEED A PASS TO THE OTHER SIDE WHERE THE GRASS IS ALWAYS GREENER REGARDLESS OF THE SEASON!
 
Swali la kitoto hili....online attraction is very unique...ina involve zaidi personality na brain...mtu anakuvutia kwa anayoyaongea akiwa very free since yuko anonymous....hujui huyo mtu ni professa au ni Secretary ..mtaani utam judge mtu na kabila lake au kazi yake..Attraction is not a choice

Mbona u sound like the relationship wil strictly be online chief ,vp the way anabehave online ikiwa tofauti na in real life,bado utakua interested naye?
 
wanaume wengine wanaotafuta wanawake mitandaoni ni waongo, na ukimkuta alie mkweli basi ujue ana tabia fulani ambazo huko mitaani hawezi kupata mwanamke
 
Back
Top Bottom