Msaada siyo haki yako; na hakuna mtu aliyezaliwa hapa duniani ili aje akusaidie wewe (labda wazazi wako tu kama wanataka!). Maisha yako ni jukumu lako kwa asilimia 100. Mpaka utakapolitambua hili, utaendelea kulaumu watu bure kumbe tatizo ni wewe na saikolojia yako potofu.
Hivyo mheshimu sana mtu anayekusaidia kwa namna yo yote ile maana kusema kweli siyo jukumu lake. Asipokusaidia napo mshukuru na kumheshimu maana pengine kwa kutokukusaidia huko ndipo anakusaidia zaidi hasa kifikra, kifalsafa na kimtazamo (kuhusu maisha, ubinadamu, mahusiano na watu, familia n.k)
Kua! πΆπΏββοΈπΆπΏββοΈπΆπΏββοΈ