Kwa Wanawake: Ukipokea pesa kutoka kwa wakala au namba ngeni unafanyaje?

Kwa Wanawake: Ukipokea pesa kutoka kwa wakala au namba ngeni unafanyaje?

Kwa mwanamke mwenye mpenzi mmoja lazima uende direct kwa muhusika wako na kumuuliza nimeona muamala asante..kama sio yeye then utafatilia kwa kina ni nan hasa amefanya huo muamala sasa kama huna wanaume wengi utaanzaje kuogopa kwenda direct kwa mpenzi wako na kumuuliza kuhusu muamala...
 
Huo muda wa kuhangaika na wakala mtu unautoa wapi?

Kwanza atamjuaje?????

Ukizingatia kama hela imekosewa kutumwa si kuna option ya kureverse hiyo transaction????

Maisha mafupi haya mkuu...acha kufanya majaribio ya uaminifu!!!!
 
Kuhusu wakala ndio msingi wa swali langu, kwamba hawezi kumuuliza aliyetuma.

Haiwezi kuwa na maana kwamba kuna wanaume wengine wanaweza kumtumia, kwa hiyo hana uhakika aulize yupi?
Yaani binti wa watu unamtafutia kesi ya bure dah! Kama unampenda basi achana kabisa na tabia hii ya kuweka hii mitego yako ya kiutopolo topolo hii. Utakuja kumpoteza kwa uboya wako na inferiority complex yako...
 
Kuhusu wakala ndio msingi wa swali langu, kwamba hawezi kumuuliza aliyetuma.

Haiwezi kuwa na maana kwamba kuna wanaume wengine wanaweza kumtumia, kwa hiyo hana uhakika aulize yupi?
Nilijua tu hili ndio kusudio lako, sasa pesa imetumwa na wakala namuulizaje babe? What if ni mama ndio katuma au mtu kakosea kutuma!! Hivi pesa ikitoka kwa wakala huwa inakuja na namba ya simu ya wakala?
 
Majaribu mengine bhn......
Hicho ni cha kuokota siyo ya kuiba, sawa na kukuta hela kwenye nguo zako wakati wa kufuaa.....
 
Inawezekana huna mazoea ya kumtumia pesa hvyo anajiuliza Ni Nani hasa ametuma hyo pesa hapati majibu kichwani.

Kuhusu mwanaume mwingine kumtumia pesa inawezekana ikawa kweli au hata ikawa sio kweli Ila tu apo anasubiri apigiwe sim ya kukosea muamala arudishe Ela ya watu.

NB: Wanawake wengi tuko hvo hasa pesa ukitoka kwa wakala
 
Kuhusu wakala ndio msingi wa swali langu, kwamba hawezi kumuuliza aliyetuma.

Haiwezi kuwa na maana kwamba kuna wanaume wengine wanaweza kumtumia, kwa hiyo hana uhakika aulize yupi?
Why umefikiria mwanaume mwingine kumtumia?

Anaweza kuwa katumiwa na baba,mama,kaka, rafiki au mdaiwa wake.Next time usitumie wakala, Just tuma kwa namba yako and ukae tu kimya.It is better that way.

Then avoid negativity.
 
Hajakuuliza sababu si kawaida ako kumtumia pasipo kumwambia. Halafu pesa imetumwa na wakala anafanyeje??

Anampigiaje simu wakala sasa?
Hapa ndio msemo wa kuishi na binadamu ni kazi. Mtu anataka kumchokoza mwenza mtulivu, apate kumtoa kasoro.
 
Natulia tuliii na siitoi isije ikawa mtu kakosea kutuma. Hivyo natulia airudishe mwenyewe au anipigie nimrudishie. Au la alieituma aseme.

Una umri gani hadi ufikirie kufanya vitu vya ajabu ajabu hivyo!! Tusijaribiane namna hiyo jamani.
Kuna siku nmekaa sina hata mia.....mara paaap TIGO PESA umepokea tsh 98000 nikaona Mungu kaamua kuniwezesha, nikaipigia bajeti haraka na hesabu ya nyama choma nikaweka, nduki kwa wakala kuitoa.....nmekaa dakika 20 tu nikatafutwa sitasahau niliumia utadhani ilikua hela yangu 😁
 
Zingine huwa ni mbinu za kiintelejinsia za mabahari,true story kuna mwamba ashatafuna manzi 'pisi kali' hapa job,manzi alitumiwa 600k alipopigiwa simu jioni alikiri kupokea hyo pesa,mwamba alimuuliza upo maeneo gani tuonane huku akijua manzi ni wa maeneo hayo hayo,manzi alipofika alisifiwa sana kwa ukarimu,mwamba baada ya vinywaji na story mbili tatu aliomba apewe 400k tu na manzi azuie 200k inayobaki km kufidia usumbufu na ukarimu aliouonyesha.
Baada ya siku kadhaa alitafunwa vzuri tu...
 
Kuna siku nmekaa sina hata mia.....mara paaap TIGO PESA umepokea tsh 98000 nikaona Mungu kaamua kuniwezesha, nikaipigia bajeti haraka na hesabu ya nyama choma nikaweka, nduki kwa wakala kuitoa.....nmekaa dakika 20 tu nikatafutwa sitasahau niliumia utadhani ilikua hela yangu [emoji16]
[emoji1787][emoji1787][emoji1787][emoji1787][emoji1787]
Kwahiyo hukuirudisha!!!
 
Back
Top Bottom