Kwa Wanawake: Vaa viatu vinavyoendana na umbo la miguu yako

Zurie

JF-Expert Member
Joined
Jul 6, 2014
Posts
2,012
Reaction score
5,571
Warembo wengi huwa tunajitahidi kuvaa nguo zitakazotukaa vizuri kulingana na maumbo yetu lakini viatu tunavaa tu vyovyote tunavyoona vizuri. Hii si sahihi!

Kama mjuavyo, muonekano mzuri wa mavazi hukamilishwa na kiatu. Leo napenda kuzungumzia viatu virefu maarufu kama "high heels". Hii itatuhusu tunaovaa high heels kwenda ofisini na hata kwenye sherehe mbalimbali.

1. Kwa wenye miguu minene

Epuka viatu vyenye mkanda kwenye kifundo cha mguu(ankle) kwani itagawa miguu yako na kufanya sehemu ya goti hadi kifundo kuonekana fupi na nene zaidi



Vaa viatu vilivyo na ncha kwa mbele(pointy toes) au vilivyo na uwazi kwenye vidole(peep toes) ili kusaidia miguu yako kuonekana mirefu na miembamba.



Epuka rangi zinazovuta attention kwenye miguu na badala yake vaa rangi zilizopoa kama brown, na zinazoendana na ngozi yako(nude). Pia vaa material ya ngozi au suede na si viatu vya kung'aa.



2. Kwa wenye miguu mirefu

Vaa viatu vyenye mkanda kwenye kifundo cha mguu(ankle strap).

Vaa viatu vyenye kamba mpaka juu au urembo mbalimbali kama hapa chini.



3. Kwa wenye miguu miembamba

Vaa wedges ili kuongeza ujazo maeneo ya miguuni.



Vaa viatu vyenye mikanda miembamba badala ya minene.



Vaa viatu vya material za kung'aa ili viakisi mwanga na kung'arisha miguu yako.

4. Kwa wenye miguu mifupi

Vaa viatu vyenye mkanda kwa nyuma(slingback style) na vilivyochongoka kwa mbele ili kurefusha miguu yako.










 
Mpe hela akapake tena rangi maana naona imefutika kabisaaa
Kwangu rangi za kucha...mawigi....kujichubuwa USO....means nothing to her beauty....napenda natural mkuu...mweke na ww wako tuone MATEGE YAKE.....usipende kukosoa vya wenzio.....wakati mwenyewe unaishi na UCHAFU na sio mwanamke

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Kwani huo mguu...ni CHUPI?au ukiona huo mguu unamjuwa huyo msichana?kwn kuna picha ngp za akina zari zipo humu....kwani huo ni UCHI?mimi nilijuwa naongea na dume.....nimeshaona avater yako....wala sibishani na wwe.....sibishani na MWANAMKE......

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…