Kwa Wanawake: Vaa viatu vinavyoendana na umbo la miguu yako

Kwa Wanawake: Vaa viatu vinavyoendana na umbo la miguu yako

ha hahahaha
ila siku hizi kuna viatu vizuri tu kwa wanene high heels ni kujitesa
_10507654.jpg
_5642177.jpg
_101498746.jpg
_101527804.jpg
ukiwa na collection yako ya hivi inatosha .
 
Warembo wengi huwa tunajitahidi kuvaa nguo zitakazotukaa vizuri kulingana na maumbo yetu lakini viatu tunavaa tu vyovyote tunavyoona vizuri. Hii si sahihi!

Kama mjuavyo, muonekano mzuri wa mavazi hukamilishwa na kiatu. Leo napenda kuzungumzia viatu virefu maarufu kama "high heels". Hii itatuhusu tunaovaa high heels kwenda ofisini na hata kwenye sherehe mbalimbali.

1. Kwa wenye miguu minene

Epuka viatu vyenye mkanda kwenye kifundo cha mguu(ankle) kwani itagawa miguu yako na kufanya sehemu ya goti hadi kifundo kuonekana fupi na nene zaidi

View attachment 574684

Vaa viatu vilivyo na ncha kwa mbele(pointy toes) au vilivyo na uwazi kwenye vidole(peep toes) ili kusaidia miguu yako kuonekana mirefu na miembamba.

View attachment 574682

Epuka rangi zinazovuta attention kwenye miguu na badala yake vaa rangi zilizopoa kama brown, na zinazoendana na ngozi yako(nude). Pia vaa material ya ngozi au suede na si viatu vya kung'aa.

View attachment 574681

2. Kwa wenye miguu mirefu

Vaa viatu vyenye mkanda kwenye kifundo cha mguu(ankle strap).

Vaa viatu vyenye kamba mpaka juu au urembo mbalimbali kama hapa chini.

View attachment 574691

3. Kwa wenye miguu miembamba

Vaa wedges ili kuongeza ujazo maeneo ya miguuni.

View attachment 574702

Vaa viatu vyenye mikanda miembamba badala ya minene.

View attachment 574701

Vaa viatu vya material za kung'aa ili viakisi mwanga na kung'arisha miguu yako.

4. Kwa wenye miguu mifupi

Vaa viatu vyenye mkanda kwa nyuma(slingback style) na vilivyochongoka kwa mbele ili kurefusha miguu yako.


View attachment 574709

View attachment 574710





Safiii,tuwekee na picha za the opposite,yaani mguu mirefu amevaa viatu vya miguu mifupi n.k,ili utupunguzie stress...

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Back
Top Bottom