Warembo wengi huwa tunajitahidi kuvaa nguo zitakazotukaa vizuri
kulingana na maumbo yetu lakini viatu tunavaa tu vyovyote tunavyoona vizuri. Hii si sahihi!
Kama mjuavyo, muonekano mzuri wa mavazi hukamilishwa na kiatu. Leo napenda kuzungumzia viatu virefu maarufu kama "high heels". Hii itatuhusu tunaovaa high heels kwenda ofisini na hata kwenye sherehe mbalimbali.
1. Kwa wenye miguu minene
Epuka viatu vyenye mkanda kwenye kifundo cha mguu(ankle) kwani itagawa miguu yako na kufanya sehemu ya goti hadi kifundo kuonekana fupi na nene zaidi
View attachment 574684
Vaa viatu vilivyo na ncha kwa mbele(pointy toes) au vilivyo na uwazi kwenye vidole(peep toes) ili kusaidia miguu yako kuonekana mirefu na miembamba.
View attachment 574682
Epuka rangi zinazovuta attention kwenye miguu na badala yake vaa rangi zilizopoa kama brown, na zinazoendana na ngozi yako(nude). Pia vaa material ya ngozi au suede na si viatu vya kung'aa.
View attachment 574681
2. Kwa wenye miguu mirefu
Vaa viatu vyenye mkanda kwenye kifundo cha mguu(ankle strap).
Vaa viatu vyenye kamba mpaka juu au urembo mbalimbali kama hapa chini.
View attachment 574691
3. Kwa wenye miguu miembamba
Vaa wedges ili kuongeza ujazo maeneo ya miguuni.
View attachment 574702
Vaa viatu vyenye mikanda miembamba badala ya minene.
View attachment 574701
Vaa viatu vya material za kung'aa ili viakisi mwanga na kung'arisha miguu yako.
4. Kwa wenye miguu mifupi
Vaa viatu vyenye mkanda kwa nyuma(slingback style) na vilivyochongoka kwa mbele ili kurefusha miguu yako.
View attachment 574709
View attachment 574710