Kwa Wapendanao tu..

Kwa Wapendanao tu..

Culture Me

JF-Expert Member
Joined
May 24, 2017
Posts
10,490
Reaction score
21,398
Huu ndio mwezi wetu wale wote tulio penzini, yaan lile penzi shatashata sio penzi la upande mmoja, raha ya penzi liwe 'nachuro' sio penzi la mizizi na kuaguliwa,
Anyway, kikubwa penzi liwepo na lionekane, mnunuliane mazawadi, toaneni outs, nunulianeni maua, mpeane mipesa na muambizane maneno mazuuuuuuri ya mahaba, (ladies na nyie mjitoe hakuna asiyependa vitu vizuri [emoji38])

Watakuja wale wa "valentine ni sikukuu ya kidini... sikukuu ya kikafiri... kwani siku zingine hampendani?..." wapendanao msiwasikilize hao masingle sugu wanakuaga na makasiriko sana nyie vimbeni na mtambe na wapenzi wenu,

Nawaonya na wale wa "mimi nampenda mama angu, nampenda mtoto angu...." blah blah blah jamani hii siku ni maalum kwa ajili ya wapenzi, msituchanganyie habari nyie masingle sugu, mama ana siku yake, baba ana siku yake, mtoto ana siku yake hii ni siku yetu sie wapenzi kuadhimisha mahaba yetu, huna mpenzi basi lala mapema au weka bundle la kutosha uwe una comment kwenye posts zetu sie wapendanao "wow!", "you guys mko mwaah" lol

Na nyie wapendanao msheherekee vizuri siku yenu ikifika msije mkavujisha connection mkatupofua macho [emoji851]

Happy Valentine in advance and happy new month y'all....[emoji323][emoji322][emoji324][emoji257]
 
Back
Top Bottom