Kwa wapenzi: Niwakati gani sahihi wakupima afya yako ?

Kwa wapenzi: Niwakati gani sahihi wakupima afya yako ?

Ndengaso

JF-Expert Member
Joined
Jul 18, 2014
Posts
7,831
Reaction score
14,259
Napenda kufahamu ni upi muda sahihi/mzuri wa kupima afya zenu kwa wapenzi, je ni kabla ya mwanamke au mwanaume kumkubalia kwenye mahusiano, au ni baada ya kuwa kwenye mahusiano na sasa wanataka kupeana unyumba ?

Nimeuliza hivi kwasababu nimekumbuka kisa cha Mike Martin ambaye aligundua ni Mwathirika wa virusi vya ukimwi muda mrefu baada ya kuwa kwenye mahusiano na binti na alipomweleza binti waachane (walikua hawajawahi kukutana kimwili) binti alikataa katukatu na hata alijaribu kujiua kwasababu hisia za mapenzi zilikua juu sana baina yao!.

We unaonaje kupima ni kabla ya mtongozaji kusema ndio au ni pale mmeshakua kwenye mahusiano na mnataka kwenda kwenye step inayofuata ?

Kupima afya nazungumzia kupima Uwepo wa VVU mwilini.
.
.
.
.
vvm
 
Itategemea na mtu na mtu, ila me nilipokubali kua kwenye mahusiano tukapima

Na naona ni vyema baada ya kukubaliana muanze rasmi mahusiano mpime

Mwengine anaweza akwambie tukapime kwanza ikiwa hata hujakubaliwa
 
Baada ya kutiana kavu ili mkipima muwe na status moja
 
Mimi ninavyoona ni vizuri kupima baada ya kukubaliana ingawa huwaga siamini sana kama hiyo inaeza zuia maambukizi kwa wapendao.

Maambukizi yanazuiwa na wahusika wenyewe, mf labda mmepima leo wote wazima na baada ya wiki mmoja wenu kaenda kukutana kimwili na muathirika hapo ww unaamini huyu ni mzima cuz tumepima so mnaenda kavu, inakua tatizo cuz lazima akuambukize.

Hii ni sababu utakua unaendelea kuamini huyu mtu ni negative cuz tumepima kumbe mwenzio kashaenda kuutafuta.

Ni Mungu pekee ajuae destiny ya kila mtu that's why hatutakiwi hata kumnyooshea kidole muathirika na hii ni kwa sababu hatuijui kesho yetu.

Tuwe waaminifu ktk mahusiano yetu na KAMA KWELI UNAMPENDA UTAMLINDA
 
Prevention is better than cure japokuwa UKIMWI hauna tiba!
 
Itategemea na mtu na mtu, ila me nilipokubali kua kwenye mahusiano tukapima

Na naona ni vyema baada ya kukubaliana muanze rasmi mahusiano mpime

Mwengine anaweza akwambie tukapime kwanza ikiwa hata hujakubaliwa
Hajakubaliwa ombi lake unaanzaje kwenda kupima nae??

Does it make any sense??
 
Ila hili swali lako linachekesha sana.... sasa kama hamjakubaliana kuingia kwenye mahusiano mtaendaje kupima??

au mimi ndio sielewi maana ya mahusiano?

Anyway, ni vema kupima kabla hamjashiriki tendo la ndoa.
 
  • Thanks
Reactions: bbc
Hajakubaliwa ombi lake unaanzaje kwenda kupima nae??

Does it make any sense??
Swali langu ni hivi kabla msichana hajasema ndio aseme mkapime kwanza au aseme ndio halafu kupima baadae?
 
Mnapokuwa na kauli moja kua "tuanze mahusiano" na ktk hali ambayo mnajua itahusisha mahusiano ya kushirikiana miili yenu.
 
Back
Top Bottom