Kwa wapenzi wa Korean Dramas, hii ni thread yako!

Kwa wale ambao waliwahi kushindwa kuangalia Yi San drama kutokana na kukoseana kwa Eng subtittles katika site nyingi, option rahisi ni kuiangalia kupitia VLC app ambayo inakupa nafasi ya kudownload subtitles katika lugha yoyote ile unayotaka.
 
Huyo mzee nilimuona kwa mara ya kwanza kwenye The Great King Sejong, alifanya vizuri mno kwenye ile kazi. Alionesha uwezo mkubwa mno wa kisiasa kwenye drama ile.


Baadae nikamkuta kwenye
Money Game ndiye aliyekuwa adui mule ndani. Alitisha sana alionesha ukomavu kwenye siasa kiuchumi
Hii money game ndio drama ambayo niliinjoy mambo ya misosi na soju, mara baada ya wafanyakazi wa wizara ya fedha pindi wanapomaliza majukumu yao lazima wakajipongeze jioni. Au asubuhi lazima msosi wa maana kabla ya kuanza majukumu yao.
 
Hiyo money game nitaitafuta Asante kwa recommend
 
Habari wakuu. Nimekuwa busy sana na mimi pia mdau wa huu uzi bali ni mdau mkubwa wa Korean drama (Historical) nimeangalia nyingi sana ila hizi morden huwa hazinikoshi napenda zile za kizamani harakati nyingi mapanga shaaaaa.

So far Jumong, Six Flying Dragons, Tree With Deep Root, Baek Dong So, Thr Moon that Embraces the Sun n.k ni master pieces.

Sasa shida yangu naomba kwanza mnipe njia ya kudownload hivi series kupitia simy maana naona dramacool nikitafuta sielewi. La pili naomba mnipe historical dramas nyingi nzuri maana nipo likizo na nina bundle lakutosha. Nina kama GB 83 hivi nadhani naweza kuangalia drama nyingi.

Mac Alpho Khantwe DAEMUSHIN
 
Japo tunatofautiana tastes jaribu hizi


The Princess' Man
River Where The Moon Rises
The Kingmaker:Change Of Destiny
Night Watchman
Shine Or Go Crazy
Joseon Gunman
Scholar Who Walks At Night
Gye Baek
King's Daughter Soo Baek Hyang
Jung Yi:Goddess Of Fire
The King's Face
The Great King's Dream
The Merchant




I think hapo itakuwa ushaziona kadhaa
 
Karibu mdogo wangu..umemisika. Naona suggestions za drama umeshapata. Kuhusu wapi kwa kupakua ingia nkiri.com au Kimoi tv mimi ndio hutumia hizo website mbili. Nkiri naipenda kwa sababu mb chache na quality nzuri , kasoro yake ni kuwa kuna drama nyingi hazipo. Kimoi nayo mb zao si nyingi ingawa quality sina uhakika sana...huwa naenda huko kama drama ninayoitaka haipo nkiri.
Baada ya kusema hayo hebu tuongee hizo gb 83 umezipataje mwenzetu [emoji3]
 
Dong Yi
Mr.Queen
Dae Jang Geum (jewel in the palace)
Queen Seondeok
Splendid politics
Kingdom
Crowned Clown
 
Nimevutiwa zaidi na hiyo sentesi ya mwisho.[emoji1]
 
Dada nina mchongo haramu kama uko yente nitafute nikupe ramani
 
1. Koguryo Kingdom
kingdom of the wind : maisha ya mfalme yuri na mwanawe muhyul (later king daemusin), main themes ni kuanguka kwa utawala Buyeo.

king gwanggaeto the great : maisha ya prince damdeok ambaye baadae alitawazwa kuwa mfalme wa 19 wa taifa la koguryeo. Alipewa heshima ya gwanggaeto kutokana na mafanikio yake ya kuipanua tawala ya koguryeo na kuwa emperor.
king dae joyeong : kuanguka kwa koguryeo kingdom kufuatia kipigo dhidi ya TANG, baadae kuanzishwa kwa taifa la Balhae.

2. Baekje kingdom

king geunchogo:
maisha ya mfalme chogo wa baekje ambaye alikuwa ni mtawazwa wa 13, Alisaidia kwa kiasi kikubwa sana kuifanya kingdom ya baekje kuwa na nguvu nyakati za uhai wake na hata baadae
Gye baek: maisha ya general gye baek na uzalendo wake kwa taifa lake la baekje, kifo chake kilipelekea kuanguka kwa taifa la baekje

3. Shilla kingdom

queen seondeok : maisha ya malikia seondeok

king's dream (the dream of emperor): maisha ya bwana chun chu na ndoto zake za kuifanya shilla kuwa taifa lenye nguvu. humu ndani utafanya repeatition ya hicho utachokiona kwenye queen seondeok, gye baek n.k.
emperor of the sea: maisha ya jang bogo na harakati zake za kutengeneza ufalme wa biashara kwa njia ya bahari
4. Koryeo kingdom

emperor wang guhn: muanzilishi wa taifa la goryeo, kama una GB zako 80 nadhani robo yake utazitumia hapa...hiki chuma kina episodes 200 lakini hutojutia kuitazama. usivunjwe moyo na video qualities ya hii drama.
Age of warriors: chuma chengine cha kibabe, ukimkuta bishoo humu ndani nitalipia nusu ya gharama yako ya bando. Pale wanajeshi wanapochoshwa kutawaliwa na wanasiasa na hatimaye kuamua kujifisha koti la uwanasiasa. Unajua kilitokezea kitu gani?......tafuta hiki chuma (nimeshaandika sana kuhusiana na hizi drama, nimechoka).
empress chunchu: kwenye utawala wa shilla., chun chun alikuwa ni mwanaume ila huku goryeo alikuwa ni mwanamke, ndio yale ya baraka wa kike na kiume. huyu cheon chu alikuwa mjukuu wa mfalme wang guhn na ni empress wa tatu katika utawala wa Goryeo. Kuna balaa lake alilifanya huyu mama.....Ni lipi wewe itafute (mimi ninayo lakini inanipa uvivu kuiangalia).
empress ki: kwa maelezo zaidi mtafute Hziyech22 na hata link atakupa yeye kwa sababu ndiye chawa wa empess ki.

BONUS:
kama unapenda vita ya bunduki na mabomu, tafuta hii drama inaitwa comrades....
inazungumzia vita ya korea
======================
nasubiria mrejesho wako, ikiwa umeangalia zote basi tuma na ya kutolea ili nipate nguvu ya kuandika list ya drama zinazozungumzia tawala ya JOSEON.
mchana mwema.
natumai msimu ujao utakuwa mshabiki wa manchester united
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…