Kwa wapenzi wa Korean Dramas, hii ni thread yako!

Huwa naona nikianza season 1 nitalazimika na kuangalia inayoendelea wakati nina msururu wa drama zinaningoja (kama nalipwa kwa kuangalia drama nyingi [emoji16])

Sent from my TECNO BA2 using JamiiForums mobile app

Ifike wakat watulipee[emoji1787][emoji1787]
Kuna wale wa nigeria hadi wanaongea kikorea
Sema vile wana variety nying inaweza kua fursa kama jonathan na patricia
 
Ifike wakat watulipee[emoji1787][emoji1787]
Kuna wale wa nigeria hadi wanaongea kikorea
Sema vile wana variety nying inaweza kua fursa kama jonathan na patricia
Jonathan na Patricia ndio nani tena [emoji16]. Kuna mdada nilimuona insta aisee anaongea kabisa mweusi kama mimi hapa. Sema mimi hata kwenye kdrama nikiona mtu mweusi huwa naona kama anafanya lip syncing siamini kama wanaongea kweli
 
Hii kitu ni ya moto kizazi kipya kimejitahidi. Kama kuna nyingine ya mahudhui haya mwenye kuijua atupie hapa. Maana za zamani zote nimeishaangalia.
Hahaha unajeuri sana wewe,
Kuna kazi nilitazama mwaka 2020 inatwa TEARS OF THE DRAGON iliandaliwa na KBS1. Ilitoka mwaka 1996 ina episodes 159. Mie nilitazama mpaka episode ya 53 maana hapo ndio kissasian walipoishia kuweka Subtitles. Habari njema ni kuwa sasa hivi episodes zote zina Subtitles na tayari kazi inapatikana pia Netflix soon nitaendelea nayo. Na nina kazi kibao kwenye playlist na bundle hili Malkia wa Jeju Island tutafika, enzi zile unakuta nadownload mpaka episode 100 kwa siku moja kisha kazi inabaki wewe na muda wako tu, hizi nishasahau kabisa kudownload naangalia online. GB 1 T.sh 3000/= nacheki episode 3-5 . Lakini pamoja na hayo haininyimi kumalizia hii kazi ya TEARS OF THE DRAGON

Hii kazi ya mwana dada Ha ji won inaitwa HWANG JINI Ilitoka mwaka 2006 ipo kwenye playlist yangu pia. Sina mashaka nae nilimwona kwa mara ya kwanza kwenye EMPRESS KI, DAMO, The King 2 Hearts na Tears of the dragon
Ukweli ni kuwa nilitegemea kuwa vijana wa sasa watakua the best maana wamekuzwa na watu ambao ni wajuzi kweli kweli, lakini imekuwa tofauti sana na matarajio yangu.juzi tena nilipokuwa natazama Documentary yangu pendwa toka Al Jazeera English iitwayo EAST 101 walikuwa wanaeleza kuwa wazee wengi wa South Korea hawa- enjoy tena Nchi yao wanadai Korea hii sio ile waliokuwa wanaijua maana imekuwa na umarekani mwingi tamaduni zao kwa sehemu kubwa zimefifishwa na Tamaduni za magharibi. Wanadai kuwa North Korea ndio Korea halisi ilobaki. Na hata Lugha yao sasa kwa sehemu kubwa inatohoa maneno kutoka kwenye Lugha ya kingereza.
Na hili limeonekana wazi kabisa kwenye drama nyingi za siku hizi hazikugusi kama zile za zamani. Anyway acha niendelee kuimba mapambio labda nami nitapata uteuzi.

Soon nitakupa list ya drama .
 
Sio jeuri mkuu kati ya watu walio addicted na wakolea hasa wakongwe nami nimo, tokea 2007 nimehamia kwenye movies na drama za wakorea na kusahau kabisa mambo ya magharibi.

Nashukuru kwa hii assignment uliyonipa, ila naomba unijuze je ipo Kimoi au Nkiri maana hizo ndio website zangu pendwa.

Natanguliza shukurani
 
Jonathan na Patricia ndio nani tena [emoji16]. Kuna mdada nilimuona insta aisee anaongea kabisa mweusi kama mimi hapa. Sema mimi hata kwenye kdrama nikiona mtu mweusi huwa naona kama anafanya lip syncing siamini kama wanaongea kweli

[emoji1787][emoji1787] lip syncing
Jaman unaona hafananii na lugha ndo maana huamin

Watu wapo serious

Patricia na jonathan mtu na kakaake ni wacongoman ila wamekulia korea

Jonathan ana variety yake wasanii wengi huwa wanaenda, ana zile humour za kikorea kabisa, yani utapenda interview zake
 
Jonathan na Patricia ndio nani tena [emoji16]. Kuna mdada nilimuona insta aisee anaongea kabisa mweusi kama mimi hapa. Sema mimi hata kwenye kdrama nikiona mtu mweusi huwa naona kama anafanya lip syncing siamini kama wanaongea kweli

Mi nadhani hata huku wapo wanaoongea
Kama wenzetu wa historical na family drama hawa watakua wanakimanya
 
Jonathan na Patricia ndio nani tena [emoji16]. Kuna mdada nilimuona insta aisee anaongea kabisa mweusi kama mimi hapa. Sema mimi hata kwenye kdrama nikiona mtu mweusi huwa naona kama anafanya lip syncing siamini kama wanaongea kweli
Hao wameishi Korea miaka mingi Jonathan alikuwa bado mdogo so kwa muda wote huo zaidi ya miaka 15 lazima Kikorea kijae wakiongea ni pure Korean
 
Waooh nitawatafuta
 
Mkuu nipe chimbo la kupakua hiyo drama
 
Umemtaja Ha Ji Won, bila shaka utapokea pongezi nyingi sana kutoka kwa INNO.

😄
 
hivi, korean drama ndio kitu gani, siku zote naona mnaandika hapa ila sijui ni nini? ujinga gani huo ati.
 
Haya hayaaa wale wa King the land umefika wakati wetu pendwa,uliokuwa ukisubiriwa kwa hamu...wa kushuhudia drama ndani ya drama, wakati wa kukasirisha na na kuvunjana mioyo.
Ndio maana kwenye drama hizi za rich guy - poor girl, What's wrong with secretary Kim ndio the best kwangu...mle hakuna drama za ajabu ajabu, zinanikeraga si kidogo [emoji1787][emoji1787]na vile ukiwa unaangalia drama unasahau kabisa kwamba ni maigizo
 
Wajamvi, nilipotea kidogo hapa kati,

Kati ya Yisan na The throne nianze wapi wakuu
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…