Kwa wapenzi wa Korean Dramas, hii ni thread yako!

Injo anaweza kuwa miongoni mwa watawala wapuuzi kwa kufuata njia ile ile ya Seonjo, kiongozi anayeililia nafsi yake pekee huku akishindwa kuumizwa na maumivu ya kuuliwa, kubakwa na kutekwa kwa wananchi wake hafai kuigwa wala kufuata amri yake...
kiongozi anayeshangazwa na kutokusikia tena miwiko ya jogoo kwa sababu ya kuwala wote huonyesha jinsi gani amejazwa na uchu wa kuitakasisha nafsi yake na mlo bora haijalishi raia wake wanashindwa kupata hata mlo dhaifu hata wakati wa raha sembuse nyakati za vita dhidi ya barbarians.

at least gwanghae alionyesha uthubutu wa kusimama pamoja na raia wake, bahati mbaya wanasiasa hawakumpenda.

My dearest
 
Episode 5:
lee jang hyun alimshauri Nam Yeon Joon aondoe mawazo ya kwenda kumlinda mfalme hivyo ni bora aondoke kwenye uwanja wa vita ili amlinde mke wake mtarajiwa Kyung Eun-Ae (nafasi ilioigizwa na lee da in, mke halali wa lee seung gi).

Nam yeon joon akajibu:
akiwa darasani amejifunza, mtoto anapaswa amsikilize mzazi wake / mlezi wake, mke anapaswa kumsikilia mume wake / mpenzi wake, na blah blah.

nadhani hiyo ndio sababu inayomfanya amkatae Gil chae, kwa sababu yeye (gil chae) haonekani kuwa ni mwanamke aliye tayari kumfuata mume kwa lolote analolifanya hata kama litakwenda kinyume na haki au sheria.

tofauti na Eun Ae, yeye (gil chae) ni msichana aliye tayari kutoka kifua mbele kupambania jambo lolote lenye haki kwake na kwa wenzake japokuwa wengineo humuona ni troublemaker

Nileteeni Gil Chae
 
Sijui wanajua tulivyo na usongo,mana wanatoa hizo episode kwa mbinde kwelikweli,
Kila nikicheki nkiri hola
The struggle is real😁
 
Queen Seondeok ni nzuri sana huko mbeleni.

Dong Yi, na Dae Jang Geum (Jewell in the palace), nazo ziko vizuri.
 
Ndo naambiwa hapa
Bora sikuifuta

Yani nataman mtiririko wa visa vya wafalme cha baada ya hii six dragon

Nasikia bang won alikuja kuua ndugu zake baada ya kupata u king
Lee Bang Won Mnyama 🔥🔥🔥
 
King of the tears 🔥🔥🔥
 
Mie mgeni wa korean drama biambie series kalii za romance na action za kikorea ili nienjoy
 
Umenikumbusha Time between dog and wolf ni kati kdrama za mwanzomwanzo kabisa kuzitama naweza kusema ndio zilizoniingiza kwenye ulevi. Yule mwenzie na Lee joon ki pamoja na kutazama drama zake nyingi jina lake nimeshindwa kulishika...🤣🤣
 
Halafu nyie mmereport komenti zangu nini mbona huu uzi nikifungua kwenye app unagoma kufunguka wakati zingine zinafunguka
 
Ile imenifanya nilale night kali ila sikupenda Sambong na Lee Bang Won kuwa maaadui,kuna kale kadada nimekapenda uchangamfu wake kama katoto kanaitwa Gab boon ambaye alikuwa anaishi na Lee Bang Jee (Best swordman) kufanya maigizo kupiga pesa kitaa.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…