Kwa wapenzi wa Korean Dramas, hii ni thread yako!

Kwa wapenzi wa Korean Dramas, hii ni thread yako!

Injo anaweza kuwa miongoni mwa watawala wapuuzi kwa kufuata njia ile ile ya Seonjo, kiongozi anayeililia nafsi yake pekee huku akishindwa kuumizwa na maumivu ya kuuliwa, kubakwa na kutekwa kwa wananchi wake hafai kuigwa wala kufuata amri yake...
kiongozi anayeshangazwa na kutokusikia tena miwiko ya jogoo kwa sababu ya kuwala wote huonyesha jinsi gani amejazwa na uchu wa kuitakasisha nafsi yake na mlo bora haijalishi raia wake wanashindwa kupata hata mlo dhaifu hata wakati wa raha sembuse nyakati za vita dhidi ya barbarians.

at least gwanghae alionyesha uthubutu wa kusimama pamoja na raia wake, bahati mbaya wanasiasa hawakumpenda.

My dearest
 
Episode 5:
lee jang hyun alimshauri Nam Yeon Joon aondoe mawazo ya kwenda kumlinda mfalme hivyo ni bora aondoke kwenye uwanja wa vita ili amlinde mke wake mtarajiwa Kyung Eun-Ae (nafasi ilioigizwa na lee da in, mke halali wa lee seung gi).

Nam yeon joon akajibu:
akiwa darasani amejifunza, mtoto anapaswa amsikilize mzazi wake / mlezi wake, mke anapaswa kumsikilia mume wake / mpenzi wake, na blah blah.

nadhani hiyo ndio sababu inayomfanya amkatae Gil chae, kwa sababu yeye (gil chae) haonekani kuwa ni mwanamke aliye tayari kumfuata mume kwa lolote analolifanya hata kama litakwenda kinyume na haki au sheria.

tofauti na Eun Ae, yeye (gil chae) ni msichana aliye tayari kutoka kifua mbele kupambania jambo lolote lenye haki kwake na kwa wenzake japokuwa wengineo humuona ni troublemaker

Nileteeni Gil Chae
 
1692934772588.png


View: https://youtu.be/Cd9Pc-XlW7Q?si=GNEF-I9MtU9HgnQe
 
Jang hyun:
smart kichwani and a very skilled warrior mwenye upendo dhidi ya watu wake wa karibu (marafiki) pamoja na wananchi wa tabaka la chini. Wapi anatokea bado haijulikani but nina wasiwasi kwa kuangalia haiba na muonekano wake wa kimavazi, tafakuri na hata nguvu yake ya utoaji msaada kwa wahitaji na connection alionayo huenda anatokea katika familia za tabaka la juu.

je? anatokea familia ya kifalme au kizazi chake kiliwahi kuwa na uhusiano wa karibu na royal families?
kama ni hivyo bila ya shaka huenda atakuwa ni miongoni mwa wahanga wa mapinduzi yaliofanywa ya kumuondoa mfalme Gwanghae yalioongozwa na different political factions waliokasirishwa na utawala wa Gwanghae.
nguvu ya theory hii inatiwa nguvu na kitendo cha Lee jang Hyun kumchukia sana mfalme Injo, huyu bwana Injo ndiye aliyewekwa madarakani baada ya kuondolewa kwa Gwanghae. Lee jang hyun hakuwa tayari kumwaga hata tone la nguvu na jasho lake kwa ajili ya kumpigania mfalme Injo dhidi ya uvamizi wa Taifa la QING.

Hopefully tutajifunza historia yake kwenye sehemu hii ya kwanza iliobakisha episode 4 kumalizika.

My Dearest drama
Sijui wanajua tulivyo na usongo,mana wanatoa hizo episode kwa mbinde kwelikweli,
Kila nikicheki nkiri hola
The struggle is real😁
 
Wazee wa Mapazia nimekubali taste zenu[emoji1787]

Aah hii six flying dragon haipoi haiboi

Kwakweli tangu nimeqnza episode 1 sijarukisha
Vitu ka hii ni vipi? alafu uzur bado ipo na quality nzuri

Queen seondok niliacha episode za mwanzo sijui itachanganya huko mbele
Queen Seondeok ni nzuri sana huko mbeleni.

Dong Yi, na Dae Jang Geum (Jewell in the palace), nazo ziko vizuri.
 
Ndo naambiwa hapa
Bora sikuifuta

Yani nataman mtiririko wa visa vya wafalme cha baada ya hii six dragon

Nasikia bang won alikuja kuua ndugu zake baada ya kupata u king
Lee Bang Won Mnyama 🔥🔥🔥
 
talnam
Picha: General Yi Songgye Vs General Choi Young
View attachment 2725445
Kuna hii kazi inaitwa Jeong do Jeon,. Ni drama ambayo infanana na hiyo six flying dragon zote zinaelezea jinsi Joseon ilianzishwa. Six flying dragon imeandaliwa na SBS na ilitoka mwaka 2015. Wakati Jeong Do Jeon ilitoka mwaka 2014 na imeandaliwa na KBS.
JEONG DO JEON
Hiii drama inamuelezea zaidi Jeong do Jeon a.k.a Sambong ambaye ni moja ya wasomi wakubwa katika historia ya Korea, pia alikuwa Neo Confuciunist Philosopher, waziri mkuu wa kwanza wa Joseon. Pia Lee Songgye( King Taejo) mfalme wa kwanza wa Joseon. Naweza kusema kwenye hii drama General Choi Young uhusika wake umeoneshwa zaidi kuliko hata Yi Bang Won.
Kwa sababu hao watubwa 3 ndio walikuwa na funguo za Goryeo ibaki na iangushwe. Ingawa hatuwezi kumbeza Yi Bang Won( King Taejong) mfalme wa 3 wa Joseon, kwa maana yeye ndiye aliyetuma wapambe wakamuue Joeng Mong Ju a.k.a Peoun ambaye alionekana kama kikwazo kwq mapinduzi ambayo Sambong pamoja na Lee Songgye( King Taejo) alikuwa ameyapanga.
Joeng Mong Ju ( Peoun) Huyu ni moja ya wasomi wakubwa kwenye hisoria ya Korea na alikuwa ndiye Waziri mkuu wa mwisho wa Koryeo. licha ya kuwa alikuwa mpinzani mkubwa wa Joeng Do Jeon ( Sambong) hawa walikuwa ni marafiki wakubwa toka utotoni mwao na ndoto yao ilikuwa ni kuleta mapinduzi kwenye Taifa lao lilikuwa linanuka rushwa na ufisadi. Kwahiyo Peoun na Sambong hawa wamesoma shule moja na wote walikuwa ni Confuciunist Philosophers. Baada ya mtihani wa Taifa Peoun aliongoza kisha Sambong akishika nafasi ya 3. Uadui wao wakisiasa ulikuja pale ambapo wawili hao walitofautiana kiitikadi kwa maana
View attachment 2725733

SAMBONG aliamini kuwa Goryeo ilipofika haiwezi kurudishwa nyuma Kwahiyo inapswa kuzamishwa kisha ianzishwe Dynasty nyingine ambayo itakuwa na mifumo bora ya utoaji huduma kwa watu na kiutawala mpaka sera za kijeshi mpya.

PEOUN aliamini kuwa kubadilisha Taifa jina sio suluu kwa matatizo yaliyopo kwenye Nchi yao bali wale viongozi wabadhilifu ambao wanafanya maisha ya watu kua magumu wachukuliwe hatua kaili za kuajibishwaji.

Kwahiyo pamoja na tofauti zao bado Sambong pamoja na Lee Songgye walikuwa bado wanamuheshimu sana Peoun kwa maana ndiye aliyekuwa kiongozi( Waziri)mwadilifu kupita hata Nyumba ya kifalme( Ukoo wa Wang) pia kiongozi mkuu wa Majeshi Choi Young alikuwa na heshima kubwa sana kwa wadilifu wake.
Tofauti ya Jeong Do Jeon (Sambong) na Lee Bang Won ilianzia hapo baada ya Yi Bang Won kumuua Joeng Mong Ju ( Peoun) baada ya hili tukio Sambong alimkataa kabisa Lee Bang Won ingawa mwanzoni Sambong alionekana kumpenda Bang Won sababu ndiye alikuwa brightest kati ya watoto wote wa Yi Songgye. Hata Yi Songgye alimkataa Bang Won baada ya Jambo hili la kumuua Peoun ambaye alionekana mwiba mkali kwa kina Lee Songgye na Sambong Ingawa tukio hili liliwapoa kina Sambong kufanya mapinduzi so Sambong akamwbia Chukua jEshi ukakamilishe kazi mie huku kwenye siasa tayari.
kifupi moja kati ya sababu ya Sambong kuuliwa na Lee Bang Won ilianziapo baada ya Sambong kumkataa na ikumbukwe Lee Songgye alikuwa anamsikiliza sana Sambong hata katika utawala wake mambo mengi alikuwa anapanga Sambong. Sambong hakutaka yaliyotokea Goryeo yajirudie tena Joseon hivyo alitaka kuanzisha mfumo wa Constitutional Monarch ambapo Waziri mkuu ndiye kiongozi wa mambo ya serikali na atachaguliwa na watu, hivyo familia ya kifalme kwakua wao wanarithi madaraka hivyo watakuwa tu kama Wakuu wa Nchi. Yi Songgye ( King Taejo) hakuwa na shida alikubali, baada ya Lee bang won kusikia hayo akafanya njama akamuua Sambong kisha Akachukua Nchi maana aliona kama mzee wake kila kitu anachoambiwa na Sambong anafuata na aliona kama Sambong anaidhalilisha nyumba ya kifalme. Kifupi Lee Bang Won alikuwa ni moja ya Viongozi bora wa Joseon licha ya kuwa aliichukua Nchi kwa njia mbaya na aliongoza kwa sheria kali mno. Pia Lee Bang Won alikuwa akiwapenda watu wa Joseon ingawa alikuwa akijuta sana kwa namna ambavyo alimwaga damu za watu ndio maana drama nyingi zina muhusisha na neno 'TEARS'

Hii drama utajifunza siasa, Falsafa pia vita zimo. pia imejikita zaidi katika historia kama unataka kuelewa kwa undani jinsi Joseon ilivyoanzishwa hii ndio first recommendation then ufanye revision na Six flying dragon.
View attachment 2725732

SIX FLYING DRAGON
Hii drama imejikita zaidi kuelezea maisha ya Yi Bang Won jinsi alivyopambana na Sambong mpaka Joseon ikaanzishwa, cha kushangaza humu ndani Lee Songgye hakupewa attention kubwa kiiivyo.
Kwenye hii drama ya six flying dragon kuna baadhi ya washiriki katika historia hawapo au visa katika historia havipo ila directors walijiongeza hivyo ilikuleta utofauti na ile drama ya Jeong do Jeon.
Ndani ya Six flying dragon utajifunza Siasa, Falsafa pia utaenjoy Action humu ndani, kuna mdada anaitwa sijui Chuksangwa anagawa dozi huyo!!!..

Kifupi drama zote ni nzuri, na kila moja inaupekee wake. Na zote ni fupi tu zina episode 50 kwa 50
NOTE: SAMBONG anahesabika kama msomi wa Joseon na msaliti wa Koryeo while PEOUN anahesabika kama msomi wa Goryeo na mwaminifu wa Goryeo

General Choi Young anahesabika kama Shujaa wa Goryeo wakati Lee Songgye anahesabika kama shujaa wa Joseon.

Recommendation
Drama yenye Story mwendelezo wa hizo mbili ni
THE GREAT KING SEJONG inamuelezea mtoto wa Lee Bang Won aitwaye Lee Do au Yi Do( Sejong the Great), ingawa Tree with Deep root nayo inaelezea japo nayo wamejiongeza director, Jang young sil pia
zote hizo zinamgusa Sejong na utawala wake.

Hawa ndio Wafalme 5 bora wa Joseon
1. Sejong the Great( mtoto wa Yi Bang Won)
2. Jeong Jo( mtoto wa Prince Sado na Mjukuu wa Yeong Jo)
3. Yeong Jo( mtoto wa Dong yi na Sukjong)
4. Taejong ( Lee Bang Won)
5.... utajaza hapa.

TAHADHALI: Chunga ulevi wa Historical drama usije ukakuathiri bure.

Alamsiki.
King of the tears 🔥🔥🔥
 
Mie mgeni wa korean drama biambie series kalii za romance na action za kikorea ili nienjoy
 
Kijana wako huyu, Lee Joon gi a.k.a Bishoo wa Soul sina mashaka nae, kwangu huyu bishoo ndiye mfalme wa hawa vijana.
Nimemuonq kwenye Time Between Dog qnd Wolf, Il Jimae, Two Weeks, Joseon Gunman, Arthdal Chronicle, Moon Lovers ( Scarlet Heart) & A tale of Arang. Sina mashaka na huyu mwamba
Umenikumbusha Time between dog and wolf ni kati kdrama za mwanzomwanzo kabisa kuzitama naweza kusema ndio zilizoniingiza kwenye ulevi. Yule mwenzie na Lee joon ki pamoja na kutazama drama zake nyingi jina lake nimeshindwa kulishika...🤣🤣
 
Halafu nyie mmereport komenti zangu nini mbona huu uzi nikifungua kwenye app unagoma kufunguka wakati zingine zinafunguka
 
Wazee wa Mapazia nimekubali taste zenu[emoji1787]

Aah hii six flying dragon haipoi haiboi

Kwakweli tangu nimeqnza episode 1 sijarukisha
Vitu ka hii ni vipi? alafu uzur bado ipo na quality nzuri

Queen seondok niliacha episode za mwanzo sijui itachanganya huko mbele
Ile imenifanya nilale night kali ila sikupenda Sambong na Lee Bang Won kuwa maaadui,kuna kale kadada nimekapenda uchangamfu wake kama katoto kanaitwa Gab boon ambaye alikuwa anaishi na Lee Bang Jee (Best swordman) kufanya maigizo kupiga pesa kitaa.
 
Back
Top Bottom