Kwa wapenzi wa Korean Dramas, hii ni thread yako!

Hizo zote ulizotaja nilishindwa kuzimaliza licha ya kusifiwa sana, tupo pamoja.
 
kuna matukio huyaona nikiwa usingizini (ndotoni), baadae hujitokeza siku za mbeleni.
Imenibidi leo niandike mbele ya hadhira (it is too much to bear)

kwa jinsi baadhi ya ndoto zinavyojidhihirisha kwa matukio halisi napatwa na woga hususani kwa hizi ndoto mbaya nilizowahi kuziota hata kama hazinihusu moja kwa moja
Nimeanza kuwa na khofu na kujiogopa.
 
Nyakati za uvamizi wa pili wa Manchu nchini korea (second manchu invasion) wanajeshi wa Qing walikuwa na shauku ya kuwakamata na kuwafanya mateka wanawake wa Joseon, wengine waliamua kuwauza kwa dhumuni la kujipatia fedha na wengineo waliamua kuwafanya kuwa mahawara (masuria).

zilikuwa ni nyakati ngumu kwa wanawake wa Joseon, si tu walipata adhabu ya kuwa wahanga wakuu kwenye uwanja wa vita bali pia walikuwa wahanga wakuu hata baada ya vita kwani wanawake wengi walisafirishwa kuelekea Simyang. kufuatia hali hiyo baadhi ya familia zikiongozwa na wanaume wanaotokea jamii ya kati na ya juu zaidi (nobleman) ziliwataka wanawake (ndugu, wake zao) wachukue hatua ya kusitisha uhai wao kwa kujiua ili kuepusha miili yao kusafirishwa na kutumika kinyume na utashi wao na kuzishushia heshima koo zao.

walioepukana na hasira za wanajeshi wa Qing ndio hivyo walipelekwa Simyang, huko nako wakakutana na majaaliwa wasioyatarajia. Wapo waliounguzwa kwa maji ya moto na wanawake wenzao kwa sababu ya wivu, sijui wanawake wa korea waliwapa nini wanaume wa Qing dynasty mpaka ikafikia hatua ya kufanyiwa ukatili na wake wakuu (first lady)

wapo ambao baadae walirudishwa nyumbani kwao (joseon) lakini baada ya kupita mchakato wa kulipiwa fidia na wanafamilia, lakini furaha zao hazikuwa ni za muda mrefu kwani maisha ya nyumbani nayo yalibadilika dhidi yao.
  • kwa mfano wanawake walioolewa hawakuruhusiwa kurudiana na waume zao, mwaka 1638 chini ya utawala wa Injo viongozi wakuu wawili (Jang Yu na Han I-gyeom)waliwasilisha rufaa (appeal)mbele ya mfalme Injo wakimtaka aruhusu mtoto wao wa kiume ampe talaka mke wake ambaye aliwahi kuwa wa Qing Dynasty kwa lengo la kulinda heshima ya familia yao, Jang hakumruhusu hata mkwe wake kuandaa vyakula kwa ajili ya kuwafanyia maombi wafiwa (ancestral memorial services).
  • bunge la Joseon likajikuta mgawanyiko wa pande mbili, wapo ambao walikubaliana na hoja ya kupewa talaka kwa wanawake wote waliorudi kutoka China, hawa waliamini mwanamke aliyekuwa mbali na mwenza wake hana sifa tena ya kuwa mke kwani atakuwa bila ya shaka ameshavunja kanuni ya kwenda kinyume na ndoa yake kwa tendo lilee (lost her chastity) hata kama alichukuliwa bila ya ridhaa yake.
  • na wapo ambao walipingana na uamuzi huo, hawa waliamini endapo sheria hiyo itaruhusika basi itapelekea wanawake wengi kujitoa uhai kwa sababu ya kujiona hawana thamani tena.
mfalme Injo akakataa mpango wa kuwapa talaka wasichana waliotoka matekani huko China lakini waunga mkono mpango wa talaka hawakuridhika na uamuzi huo, mwishoni iliamulia kila mtu atafanya uamuzi wa mujibu wa matakwa yake....

Atakayeamua kumuacha mke wake ni sawa na atakayeamua kuendelea na ndoa yake pia ni sawa.

Je Inspector Goo Won Moo atampokea Gil Chae kama mke wake pindi atakaporudi Joseon?
 
I wish angekuwa main character namkubali sana anajua kuigiza alafu ni mrembo haswa
Angalia Celebrity humo ni mpole sana hata anavyoongea utampenda ni mkarimu.

Humu kwa My Dearest ana wenge sana katili halafu ana wivu kinoma eti akimpenda mwanaume akamkataa basi atamfanya ajute[emoji23]

Sema licha ya kufanya mambo ya kukera sijachukia character yake kama unavyojua ufanboy huu,kwa age yake bado anaita ila ukikaa ukifuatilia now kuna waigizaji vijana wana visuals aisee[emoji1316]
 

Nam goo min atakua anamkubali sana
Safar hii mpaka wamegusanisha vidomo
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…