Injo wa Joseon aliishi miaka 54 na alikuwa mfalme wa 16, Injo alikuwa ni mjukuu wa mfalme Seonjo (mtawala wa 14 wa Joseon). Injo alibeba madaraka ya ufalme kufuatia mapinduzi yaliomuondoa mfalme Gwanghae mnamo mwaka 1623.
Baada ya Joseon kujisalimisha dhidi ya Qing iliamuliwa crown prince soe hyun achukuliwe mateka na hatimaye akaweka makaazi yake eneo la Simyang ambapo huko aliishi kwa takribani miaka 8.
mwaka 1644, crown prince alihamia Beijing na huko ndipo alikutana na Jesuit missionary Johann Adam Schall von Bell. crown prince alifariki mwaka mmoja baadae baada ya kufanikiwa kurudi nyumbani kwao.
In 1627, mwana wa mfalme alimuoa binti wa bwana Gang Seok-gi (binti huyo ni uzao wa 17 wa kizazi cha General Gang Gam chan wa Goryeo). Sohyeon alikimbia pamoja na baba yake (Injo) kuelekea ngome za Namhan ila kwa pamoja waliamua kujisalimisha mbele ya mfalme Hong Taiji wa Later Jin baada ya kudhibitiwa kwa kisiwa cha Ganghwa na wanajeshi wa Later jin Dynasty.
ndipo hapo safari yake ya kuwa mateka ilipoanzia, Crown prince alitambulishwa rasmi katika ulimwengu wa kimagharibi pamoja na ukatoliki mara baada ya kukutana na Johann Adam Schall von Bell.
crown prince alirudi nyumbani kwao akiwa na mtazamo mpya juu ya dunia jambo lilomweka kwenye upinzani mkali dhidi ya baba yake aliyeamini mwanawe tayari ameshakunywa maji ya bendera ya Qing, ukatoliki na umagharibi.
siku chache baadae mwana wa mfalme aliyeonekana chumbani kwake akiwa amefariki huku akivuja damu, zipo nadharia zinadai ya kwamba mwana wa mfalme aliuliwa kwa njia ya sumu, huku wengine wakienda mbali zaidi kwa kudai mfalme Injo alimuuwa mwanawe kwa kumrushia usoni ink slab (kibao fulani hivi wanatumia kwa ajili ya kuchanganyia wino)
mfalme Injo alipunguza siku za maombolezo ya mwanawe, aliweka kizuizi kwa kila aliyejaribu kuchunguza kifo cha mwanawe, si hivyo tu inasemekana mfalme Injo hakuwahi kutembelea kaburi la mwanawe.
baadae Injo aliamuru wajukuu zake watatu (watoto wa mwana mfalme so hyun) waondoshwe (exile)ndani ya mji kuelekea kisiwa cha JEJU, ni mtoto mmoja tu kati ya hao aliyefanikiwa kurudi mainland kwani wengineo waliuliwa. Hata aliyekuwa mke wa crown prince naye aliuliwa kwa hoja ya uhaini.
=========
Kama umeangalia slave hunter utakuwa umeshavuta picha ya mkasa mzima wa kumgombania yule mtoto mdogo, yes alikuwa ni mtoto wa crown price sohyeon. Na yule bwana Song taeha alikuwa ni mlinzi wa crown prince Sohyeon hukoo Simyang, naye aliporudi Joseon pamoja na crown prince alijikuta anatengenezewa kesi ya kuiba chakula cha wanajeshi.
View attachment 2794730
==========
turudi kwenye my Dearest drama, unadhani ni kipi kitamkuta lee jang hyun pindi atakaporudi Joseon kutoka Simyang?
Unakumbuka episode 1 ilianzaje, kwenye ukanda wa bahari wanajeshi wa Joseon walikuwa wamemzunguka Lee Jang Hyun huku akiwa anavuja damu.
unadhani sababu ilikuwa ni nini?
View attachment 2794717
===========
kuna historical movie inaitwa
the night owl ya mwaka 2022 ndio naiangalia, inazungumzia hadithi ya mfalme Injo na mwanawe crown prince sohyeon pamoja na daktari mwenye uhafifu wa kuona (blindness) aliyeshuhudia mauaji ya mwana wa mfalme
jioni njema
View attachment 2794729