TIGO WANATOA MB ZA BURE?
Wakuu, kwa mwenye line ya Tigo anaweza jaribu bahati yake.
Leo baada ya game ya Spurs nikawa naperuzi you tube kwa line ya voda.
Sasa sms ika pop up kuonesha MB zlinakaribia kuisha. Na muda mfupi baadae kweli MB zikaisha.
Sasa nikasema ngoja nijaribu ku-switch nitumie line ya Tigo labda kuna MB.
Kujaribu line ya Tigo nikaona mzigo unatiririka. Hapo nikakumbuka mbona MB za tigo nilizimaliza? Inawezekanaje ikubali kuperuzi sasa?
Ikabidi niangalie salio. Kuangalia salio SMS ikaja nina MB 0.
Nikarudi you tube mzigo unatembea bado, chrome imo, twitter na IG zinatiririka.
Hapo mawazo yakanijia hii itakua nimeokota dodo chini ya mnazi . Fasta nikakimbilia Uc browser kupakua movie.
Nimepakua movie mpaka saa 8 MB naona haziishi. Nikalala mpaka saa 11 kujaribu naona MB bado zinashusha muvi kwa kasi ya 4G.
Mpaka muda huu bado zipo zitakua unlimited hizi.
Sasa nawashukuru zana Tigo kwa upendo wenu wa dhati kwa wateja. Nikirudi jioni kitaa kama MB zitaendelea kuwepo basi nawafungulia free WiFi mtaa mzima ili tufaidi wote mema ya nchi.