Kwa wapenzi wa Korean Dramas, hii ni thread yako!

Ni movie au series?
Itakuwa ni series sijui ila naona itakuwa ni series ya kikorea niliona Trailer tena ilikuwa imetafsiliwa ...mapolisi walikuwa na mabosi wao wanakwenda kwenye treni kufanya mafunza jinsi ya kuzuia wezi kuibia abiria mara hao mapolisi mabosi wenye kutoa mafunzo wakashangaa wamesha ibiwa hapo kwa hapo bila ya kujua hata wameibiwa namna gani wala kumuona mwizi wakati wanaibiwa ndani ya treni .
 
Kuna anaeielewa hii strong girl namsoon?nasikia ni mwendelezo wa ile ya kwanza ila naona huyu namsoon hanivutii anavyoact au ni mimi tu?
 
My Dearest sehemu ya 17 haijaenda hewani leo.? Nimeiangalia site zote mpaka sasa haijawekwa.
 
My Dearest sehemu ya 17 haijaenda hewani leo.? Nimeiangalia site zote mpaka sasa haijawekwa.
Hii drama mnaipendea nini? mimi nimeishia episode 1 nimeona story ni zile zile za kitoto eti mwanamke anamtafuta mwanaume ambaye anamuona kwenye ndoto, la pili ni main characters wamecheza kama comedy fulani hivi Hawapo serious hii pia imechangia kutoendelea kuifuatilia labda kama uko mbele kuna mabadiliko
 
Hii drama inakupa furaha na majonzi kwa wakati mmoja mana kuna love story,uvamizi wa ming huko joseon yaan maswala ya political na mengineyo,hakuna utoto kivilee..anyway nasubiri part 2 imalizike yote kisha niiangalie..mana wana mpango wa kuirefusha kidogo...
 

Hii drama sio ya kutazama eposode moja maana ina stori tofauti ndan kibao

Nam goo min kacheza characters zake bora zote humu yani mkusanye kwenye genre zake unamkuta humu full na nyongeza ya kisses scene
 

Kwakweli labda wairefushe maana mpaka sasa sijaelewa tunarudije ep 1 ya season 1 na zimebak ep nne
 
Tatizo ni haraka haraka, episode moja tayari umekuja kufanya analysis na kisema drama sio nzuri? Komaa nayo walau mpaka ep ya 4 au 5.
 
Vipi slave hunter ni kali ? nimewekewea hapa Library ya mtaani iliyotafsiriwa na MaDJ na nimeanza kuicheki episode za mwanzo ila bado sijaona amsha amsha wala msisimko mzuri wa stori na matukio.
Kali sana,

Hao madj watu bado mnacheki kazi zao🤣
 
TIGO WANATOA MB ZA BURE?
Wakuu, kwa mwenye line ya Tigo anaweza jaribu bahati yake.

Leo baada ya game ya Spurs nikawa naperuzi you tube kwa line ya voda.

Sasa sms ika pop up kuonesha MB zlinakaribia kuisha. Na muda mfupi baadae kweli MB zikaisha.

Sasa nikasema ngoja nijaribu ku-switch nitumie line ya Tigo labda kuna MB.

Kujaribu line ya Tigo nikaona mzigo unatiririka. Hapo nikakumbuka mbona MB za tigo nilizimaliza? Inawezekanaje ikubali kuperuzi sasa?

Ikabidi niangalie salio. Kuangalia salio SMS ikaja nina MB 0.

Nikarudi you tube mzigo unatembea bado, chrome imo, twitter na IG zinatiririka.

Hapo mawazo yakanijia hii itakua nimeokota dodo chini ya mnazi . Fasta nikakimbilia Uc browser kupakua movie.

Nimepakua movie mpaka saa 8 MB naona haziishi. Nikalala mpaka saa 11 kujaribu naona MB bado zinashusha muvi kwa kasi ya 4G.


Mpaka muda huu bado zipo zitakua unlimited hizi.

Sasa nawashukuru zana Tigo kwa upendo wenu wa dhati kwa wateja. Nikirudi jioni kitaa kama MB zitaendelea kuwepo basi nawafungulia free WiFi mtaa mzima ili tufaidi wote mema ya nchi.​
 
Liadong ingekua ngumu kuiziwia isichukuliwe ukiangalia kwenye ramani hapo unaona ipo mdomoni mwa China.

Nakumbuka vita ya Koguryeo kuilinda Liadong dhidi ya Han kwenye "Jumong" ilibidi mpaka mzee baba Daeso aungane na Jumong ili waweze kumpiga Han.
Halafu mpka General Mugol alikufa katika vita hiyo ya kuitwaa Liaondong ..
 
Hamna nikiwa sina MB naenda kwa dogo kibandi huwa ananiwekea bure mimi nachagua yeyote naisongesha mpka . Japo wanaongopa ila wananogesha picha sana.
BAndo limekua mtihani hata mm nimekaa pembeni kwanza nazisave recommendations tu
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…