Kwa wapenzi wa Korean Dramas, hii ni thread yako!

Hamna,hii ni jamaa aliyeokotwa mtaan na familia ya kitajiri wakamdanganya wao ni wazazi wake,nia yao ni kuupata moyo wake ili kuupandikiza kwa kijana wao aliyekua na matatizo ya moyo. Badala yake huyu kijana akagundua janja yao na kuwazidi ujanja na kuwapindua kwenye kampuni yao na utajiri wao
Hii si ndiyo jamaa mwishoni anawachanganya mdogo mtu na dada ake? Maana nimeichek muda sana.
 
Ok nishakumbuka huwa nachanganya big man na bad guy,hii nadhani niliishia pale alipogongwa na pikipiki yule bibi aliyemuokota na kumlea.
 
Yeah ana smilling face mwenyew ananvutiga sana nlimpenda toka kim nana kwny city hunter
 
You are welcome oppa (ila nahisi unatakiwa uniite noona) . Binafsi kila nikilog in Jf huu ndo huwa uzi wangu wa kwanza kabisa kuchungulia. Hakika mchango wako ni mkubwa sana nisipokuona muda mrefu nakumisije na mahabari yako motomoto
 
You are welcome oppa (ila nahisi unatakiwa uniite noona) . Binafsi kila nikilog in Jf huu ndo huwa uzi wangu wa kwanza kabisa kuchungulia. Hakika mchango wako ni mkubwa sana nisipokuona muda mrefu nakumisije na mahabari yako motomoto
Hahahahaha ngoja mi nkuite "Unni" cjui nmepatia maana zinanichanganya
 
ahsante sana ila mara nyingi sana huwa nasahau kutofautisha kati ya noona(dada kwa mwanamme) na unni(dada kwa mwanamke) ndio maana naona tabu kutumia neno hilo
haha sema hata wao wanatuchanganya. Kwenye chuno nliona wanaume wanaitana unni sijui ilikuwa na maana gani
 
Hahahahaha,Thanks Mkuu, Sante Sana,Mi Pia Nimejikuta naitembelea hii thread Mara kwa Mara sababu yako nikajikuta Mpaka Nkumisi Mwayaa, Mambo yamekuwa Mengi Mkuu ila tupo......
 
Samahani Hivi nawezaje kudownload kwa kutumia pc... nimeshalizwa kakimeo kangu nilikokuwa natumia kupakua
 
kwa mara ya kwanza leo baba wa muigizaji song joong ki amefanya mahojiano kuhusiana na taarifa za mtoto wake kufunga ndoa na mwanadada aliyemzidi kiumri kwa miaka 2 song hye kyo na alisema maneno yafuatayo

"song yupo kwenye umri mzuri sana kwa ajili ya kufunga ndoa na kama wazazi ni jukumu letu kuheshimu maamuzi ya mtoto wetu na zipo taarifa za uvumi zinazodai kama sisi tunapingana na ndoa hii iliyotangazwa kufanyika october 31 jambo ambalo ni la uongo. ninapenda kuona nikiitwa babu na mtoto atakayezaliwa na mwanangu na pia kumuona mtoto wangu akitekeleza majukumu yake ya kifamilia na pia kuzidi kufanikiwa kwenye kazi yake ya uigizaji.

pia ameendelea kusema ya kwamba bado mtoto wake anamtembelea mara kwa mara pamoja na marafiki zake hususan lee kwang soo ambaye ndiye rafiki yake mkubwa sana.
pia wakatii wakifanya kazi kwenye drama ya descendent of the sun song couple,jin goo,kim jin woo walikua wanalala hapa baadhi ya siku kwa sababu film location ilikuwa ni karibu
 
Wow my song song couple. Mimi nlisikitishwa baada ya kuona taarifa hiyo eti baba yake yuko disappointed kisa Hye Kyo mkubwa kuliko mwanae..watu sijui wanavumishaga ili iweje yaani. Ila hawa nna wasiwasi wasijekuwa wanaoana kwa influence ya mashabiki maana mashabiki walikuwa wanawish sana hiki kitu kitokee yaani sijawahi kuona couple inayotamaniwa kwenda kwenye real life kama hii
 
mwanadada kim tae ri (27) amechaguliwa kuwa muigizaji mkuu wa kike kwenye drama mpya inayoitwa MR SUNSHINE ambayo inazungumzia stori ya kijana wa kikorea ambaye alitelekezwa nchini kwake kwenye miaka ya 1871 na baadae akawa mwanajeshi wa marekani aliyeongoza msafara wa jeshi la marekani kuja kuisaidia nchi ya korea dhidi ya uvamizi wa taifa la japan mnamo mwanzoni mwa karne ya 20.(1900-1905)
kwenye drama hii mwanadada kim tae ri atacheza nafasi ya msichana anayetokea kwenye familia za kifalme zilizokuwa zikijulikana kwa jina la Go family ambaye alijikuta akiwa kwenye mahusiano na mwanajeshi licha ya kwamba mwanajeshi huyo hakuwa akitokea kwenye familia zenye heshima nchini Joseon

wiki mbili zilizopita muandishi wa drama hii mwanamama kim eun sook(Script writer)ambaye pia ndiye muandishi wa drama ya descendent of the sun na Goblin alimtangaza muigizaji Lee byung hun (46) kuwa ni muigizaji mkuu wa kiume,hii itakuwa ni drama ya kwanza kwa lee byung hyun baada ya miaka 9 tokea ashiriki kwenye drama ya IRIS 1.
baadhi ya mashabiki wameponda uteuzi wa mwanadada kim tae ri na sababu kubwa ni utofauti wa umri uliopo kati yao ambapo Lee byung hun amemzidi Kim tae ri kwa miaka 20
 
noona huyu jamaa yako bado hataki tumuone sura yake, halafu nina wasi wasi ameshakusahau kwa sababu anapokea zawadi za wapinzani wako au umempa ruhusa?

 
noona huyu jamaa yako bado hataki tumuone sura yake, halafu nina wasi wasi ameshakusahau kwa sababu anapokea zawadi za wapinzani wako au umempa ruhusa?

Anajidai na sura yake. Mwache achukue tu kwaanza mimi nshakuwa Mrs Choi sasa hivi teh japo karoho kanauma
 
muigizaji kim soo hyun leo amekanusha taarifa zilizosambazwa na chombo cha habari ya kwamba atakwenda kutumikia shughuli za kijeshi ifikapo mwezi septemba. Kwa mujibu wa kim soo hyun agency (keyeast) wamesema ya kwamba taarifa zilizochapishwa ni za uongo kwa sababu mpaka sasa hatujapokea taarifa yoyote kuhusiana na shughuli hizo za kijeshi ila tutakapopata taarifa kutoka sehemu husika basi tutaiweka hadharani.kutokana na kusumbuliwa na tatizo la moyo pindi alipokuwa mdogo kim soo hyun ameruhusika asitumikie jeshini na atafanya kazi za kijamii
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…