Kwa wapenzi wa Korean Dramas, hii ni thread yako!

Kati ya hizo zote basi nimeipenda 'Hwayugi' na 'Money Flower'.

Black Knight kiroho safi naamua kuishia ep ya 10.

I am Not A Robot kila nikilazimisha macho kuamini lakini moyo unakataa.

Nothing 2 Lose huyo villan hana jipya nishamzoea.
Hmmmm!!!! Unataka Angalia Drama Za Aina Gani!?????
 
Sunbae,
Unaonaje ukiwa unazidownload hizo episodes kisha unazisahau kabisa?

Kisha utaziangalia tu pindi ukiwa free na una mzuka wa kufanya hivyo?
Halafu kama ikitokea drama fulani hujaipenda basi ni kuiacha tu kwenye disk au hata kuifutilia mbali?

takribani wiki nzima iliopita nilikuwa naangalia drama ya emperor wang guhn (taejo wang guhn) ya mwaka 2000 yenye episode 200 ambayo ni kiporo changu cha muda mrefu sana,kihistoria wang guhn ndiye mfalme wa kwanza wa taifa la goryeo (koryeo) na aliingia madarakani baada ya kumpindua mfalme gongyae ambaye alikuwa ana tabia za kidikteta.
ndani ya wiki moja nilibahatika kuangalia kuanzia episode 90 hadi episode ya 122, kwa sasa nimeamua kuiweka tena kiporo kwa sababu upande wa kwanza wa maisha ya wang guhn nimesha ufahamu kwa sababu hadi episode ya 121 ndio anabeba madaraka. licha ya kuwa ni drama ya zamani lakini haikunichosha kuitazama kwa sababu hadithi yake ni ya kusisimua na cha kufurahisha zaidi nusu na robo ya stori yake ni ukweli mtupu yaani namaanisha matukio mengi yamerikodiwa kwenye vitabu vya kihistoria.

kuhusu kizidownload episode na kuziangalia baadae ilo suala nalifanya ila tatizo linakuja kwenye kuziangalia, kiukweli mzuka wa kuangalia ndio umepungua, napata tabu sana siku hizi.
  • money flower ndio drama pekee ambayo episode zake nikizodownload naziangalia muda huo huo,nakumbuka mwezi uliopita niliwahi kuandika natamani siku za wiki zipungue ili jumamosi ifike haraka nipate kuiangalia money flower.
  • hwayugi episode ya 3, 4 tayari nimezidownload tokea jumatatu lakini hakuna hata moja niliyoiangalia.
  • father is strange drama episode 4 za mwanzo tayari nimezidownload tokea siku ya jumatatu ya mwaka mpya lakini hadi leo sijaiangalia hata moja.
  • 2 cops drama hii imechangia kuwa mvivu wa kuangalia drama, baada ya kujilazimisha jana ndio nimefanikiwa kuendelea kuangalia episode ya 11,12,13,14. sitaiangalia tena.
  • the producer drama, ni drama ya 2015 ambayo ameigiza kim soo hyun kidogo hii ndio naweza kuiangalia japo kwa nusu saa, nimeishia episode ya 8.
  • defendant drama nimeidownload siku aliyotangazwa ji sung kuwa ni mshindi wa grand prize kupitia sbs drama awards, nakumbuka ilikuwa ni mwaka mpya lakini hadi leo sijaiangalia hata nusu episode.
  • kill me heal me nayo hivyo hivyo nimeidownload lakini mzuka wa kuiangalia sina
  • hadi leo goblin nimeishia episode ya 4 na kwenye pc ninayo mpaka mwisho.
  • black knight episode ya 9,10 kwenye pc ninazo lakini sijaziangalia.
  • temperature of love nilikuwa naipenda sana hii drama lakini nimeishia episode ya 16 na nahisi tabu kuiendeleza.
  • nadhani ni muda muafaka wa kuipumzisha akili labda mzuka unaweza kunirudia tena.
 
Sunbae drama zote ulizozitaja hapo ukiachia hiyo ya mwanzo ni kutoka Seoul.
Unaonaje tukarudi asilia yetu, Joseon?
joseon, goryeo, balhae, shilla, gaya, baekje, goguryeo.
si wazo baya kwa sababu zipo drama nyingi sana sijaziangalia ila ngoja nilifikirie zaidi wazo lako.
 
Ata mm nafanya mazoezi ya kuachana na hiv vitu. Huu mwaka niko busy sana nikisema nizipe nafasi kwakwel sito ambulia chochote. Mda wowote nitawakimbia
 
Ivi uko Seriously Kabisaaa !???
ni kweli nahitaji mapumziko na nafahamu ni vigumu sana kwa sababu kuangalia drama imekuwa ni kama sehemu ya maisha yangu.
kiupande wa pili kuacha kufuatilia drama na maisha ya hallyu stars itanibidi nitafute starehe nyengine ndipo tatizo jipya linapozaliwa, sijui nifatilie kitu gani.
lakini kwenye JF nitafuatilia jukwaa la teknolojia na intelligence naamini nitajifunza masuala mengi sana ya kiulimwengu.
nimedhamiria kweli kupumzika au kuacha kabisa kuangalia korean drama
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…