unajua hizi pombe mpya nazo zimechangia kunifanya niwe na mawazo ya kuacha ulevi huu pendwa wa korean drama. Zamani kabla sijawa na uwezo wa kumiliki PC nilikuwa siangalii recent drama hivyo basi nilikuwa nashindwa kufahamu drama ninayoangalia ni toleo la mwezi gani hivyo basi nilipokuwa nakwenda library nilikuwa nachagua drama yoyote tu.
lakini sahivi napata tabu sana kuangalia drama zilizopita kwa sababu naziona ni za kizamani sana na hizi recent drama nazo zinanifanya niwe mvivu kuzifatilia kila wiki utafikiri ni dozi ya mgonjwa wa kisukari.