Kwa wapenzi wa Korean Dramas, hii ni thread yako!

Kwa wapenzi wa Korean Dramas, hii ni thread yako!

Korea Broadcasting Actors Union Rep Provides Deeper Insight Into Drama Payment Controversy
taarifa zinazohusu kutokulipwa fedha zao kwa baadhi ya waigizaji zimezidi kuongezeka jambo ambalo limepelekea chama cha waigizaji nchini korea kulitolea ufafanuzi suala hilo.
wiki iliopita baadhi ya waigizaji kama rain, lee na young,jung yoo mi na kim min jung kwa nyakati tofauti walizungumzia mkasa huo wa kutokulipwa fedha zao baada ya kuigiza drama.
Rain-Lee-Na-Young.jpg

siku ya jana (17/01/2018) bwana Song chang gon ambaye ni mkuu wa korean brodcasting actors external relations alipata nafasi ya kulizungumzia suala hilo kwenye mahojiano aliyoyafanya kupitia vyombo vya habari.
kwanza aliyelezea jinsi mfumo wa malipo unavyofanyika kwa waigizaji ambapo song chang gon alisema ili kuelewa sababu ya waigizaji kutokulipwa fedha zao baada ya kushiriki kwenye drama ni lazima tufahamu ya kwamba;
kwenye film waigizaji wanalipwa baada ya film kukamilika na kwenye drama waigizaji wanalipwa baada ya drama kuanza kuonekana kwenye televisheni, kwa mfano kama zoezi la kuigiza drama litaanza december na baadae drama ikaanza kuonyeshwa mwezi january kwenye televisheni basi muigizaji hulipwa fedha zake mwishoni mwa mwezi february kwa sababu mashirika ya habari nchini korea hulipa mishahara mwishoni mwa mwezi.
mfumo huu ndio husababisha makampuni kushindwa kuwalipa waigizaji fedha zao kwa kusubiri mpaka drama itakapomaliza kuonyeshwa na hapo ndipo tatizo linapotokezea, alisema song chang gon.
Gong-Seung-Yeon-Jung-Yoo-Mi-XPN.jpg

alipoulizwa ni kiasi gani cha fedha ambacho waigizaji hawajalipwa song alisema siwezi kuzungumzia deni la kila muigizaji analodai kwa sababu hiyo ni ishu binafsi ila kwa waigizaji waliojiunga kwenye chama wanadai jumla ya won billion 3.2 (usd 2.98 million) kupitia mashirika ya KBS,MBC na SBS, lakini hayo ni madeni ya zamani kwa sababu kwa sasa hakuna muigizaji ambaye amewahi kulalamika kutokulipwa fedha zake.
pia amezungumzia sababu inayopelekea kuwa na ugumu wa kutatua tatizo hilo ambapo aliendelea kusema wakati wa utawala wa lee myung bak haki yetu ya kukaa na kuzungumzia suala hili liliathiriwa zaidi na kanuni za serikali.
lakini suala hili lipo mahakamani na tunategemea mwezi machi au april hukumu ya kesi hii itatolewa.baada ya hapo tutakaa na mashirika ya habari, production company na serikali kwa niaba ya waigizaji ili kuweza kulitatua suala hili.
Wawakilishi pia wamebainisha ya kwamba wizara ya utamaduni,michezo utalii na fair trade commission waliiingia makubaliano waigizaji ila kwa jinsi inavyoonekana makubaliano haya hayafuatwi ipasavyo, makubaliano hayo yanasema kama kutatokezea tatizo la malipo basi shirika ndilo litakalohusika na suala hilo.

Sunbae,
Kuna dramas zipi zenye kuzungumzia maisha ya mfalme Sejong the Great?

Nimewahi kuyaona kwa ufupi katika dramas kama 'Six Flying Dragons' & 'Jang Yeong-sil'.
King_Sejong.jpg

  • itapendeza zaidi kama utaiangalia great king sejong drama kwa sababu ndio inazungumzia maisha yake kuanzia alipokuwa mdogo mpaka kuja kurithi madaraka ya baba yake.
  • kiukweli kwa mujibu wa stori ya drama hii yi do (sejong) alikutana na changamoto nyingi sana kwa sababu tokea udogoni kwake hakuvutiwa na utawala wa baba yake ambaye ni lee/Yi bang won(taejong) jambo ambalo lilipelekea hata kuondoshwa kwenye jumba la kifalme na baba yake.
  • taejong alitaka mwanawe wa kwanza ndiye awe mrithi wake wa madaraka lakini alikuwa ni mpenda mambo ya anasa sana.
  • Taejong alikuwa ni mtawala mkorofi na wakati wa utawala wake alibadilisha sheria na kuamua jambo lolote lile linalohusu nchi ni lazima aliamue yeye kwanza ndipo litekelezwe.
  • hata alipokabidhi madaraka kwa mwanawe alibaki na mamlaka ya kusimamia suala la ulinzi wa nchi na kuendelea kumuendesha mwanawe (puppet king) hata kufikia kumuua baba wa malkia kwa kumtengezea kesi ya uasi.
  • lakini EMPTY dongsaeng licha ya kuwa great Sejong alikuwa ni kiongozi mwenye fikra mbadala na maono makubwa sana ila huwezi kuzungumzia mafanikio yake bila ya kuwataja watu kama Jang young sil japo kuwa yeye ndiye aliyempa nafasi na kuthamini kipaji cha mtumwa.
  • herufi za hangul zilianza kutumika wakati wa utawala wake na hata science na technology.
  • cha kufurahisha zaidi ni kwamba kim young chul ameigiza nafasi ya lee bang won humu ndani na pia kwenye jang young sil, vile vile kim sang kyung ameigiza nafasi ya sejong na pia kwenye jang young sil aliigiza nafasi ya king sejong.
    2edd0b5ebe091e5d62c14d76b658dffe.jpg
    Jang-Yeong-Sil3.jpg
 
leo nataka nianze kuiangalia drama ya Admiral Yi SOON SHIN (joseon naval commander)
https://ondramanice.io/drama/the-immortal-yi-soon-shin-detail
img_0143.jpg

leo nataka nianze kuiangalia drama ya Admiral Yi SOON SHIN (joseon naval commander)
https://ondramanice.io/drama/the-immortal-yi-soon-shin-detail
img_0143.jpg

EMPTY Naomba tumrudishe Kwao Uyu Coz Sidhani Kama kazaliwa Zanzibar Uyu..
 
leo nataka nianze kuiangalia drama ya Admiral Yi SOON SHIN (joseon naval commander)
https://ondramanice.io/drama/the-immortal-yi-soon-shin-detail
img_0143.jpg

Na Mie ngoja Nianze Angalia Hiii.
 
EMPTY Naomba tumrudishe Kwao Uyu Coz Sidhani Kama kazaliwa Zanzibar Uyu..
aigooooo unaanza utani, jana black knight imeendeleaje?
naona mzee park episode ya wiki iliopita alimtumia message za uchochezi jung hae ra kuhusiana na baba yake kuhusika na kifo cha baba yake moon so hoo.
ila Sharon naye ni king'ang'anizi
Black-Knight-The-Man-Who-Guards-Me-SSK-2.jpg
 
Mpka muda huu sijaitazama ndo naishusha APA.
 
chombo kimoja cha habari kinachoandika taarifa mahususi zinazohusu tasnia ya uigizaji nchini korea leo hii kimeripoti ya kwamba mwanadada jang na ra amepata ofa ya kuigiza kupitia drama inayokwenda kwa jina la Dog, witch and me.
kwa ufupi jang na ra ataigiza uhusika wa mwanamke ambaye ni mlemavu wa macho ambaye alikuwa na upendo mkubwa kwa mnyama wake.
wakati huo huo Rawon Culture ambayo ni kampuni inayomsimamia jang nara wamethibitisha taarifa hizo lakini hakuna makubaliano yoyote yaliofikiwa mpaka sasa kwani mteja wao ana offer nyingi sana.
kama jang nara atakubali kushiriki kwenye drama hii itakuwa ni project yake ya kwanza kwa mwaka 2018,mwaka uliopita alishiriki drama inayojulikana kwa jina la go back couple
dca9c647e6e865a99523903cfbc500c2--jang-nara-fated-to-love-you.jpg
 
Mpka muda huu sijaitazama ndo naishusha APA.
  • ngoja nami niihifadhi kabisa ila sitaiangalia kwa leo.
  • hwayugi episode ya sita sijaiangalia mpaka muda huu, halafu inashangaza sana drama ya hwayugi inafika jumanne subtitle haijakamilika kuwekwa.
  • nimebahatika kuangalia gu family book, my girlfiend is gumiho, king to hearts na shining inheritance ila project hii ya hwayugi nahisi ndio bora zaidi tokea lee seung gi aanze kazi ya uigizaji.
    w644
  • cha seung won naye ameitendea haki sana nafasi ya ma wang, nilipokuwa naangalia episode ya 5 aliporudi kwenye dunia ya mwaka 1930 wakati sam jang alipopigwa risasi kwa ajili ya kumtafuta mtoto wa kijapan kiukweli nilikuwa natamani ma wang na yule mwanadada anayempenda sana anaitwa na chal nyeo warudi pamoja kwenye dunia ya sasa hivi, ila ndio hivyo fate
    Cha-Seung-Won11.jpg
  • P.K (lee hong ki) na yule mdada bong soon (zombie) wananiburudisha sana uhusika wao
 
EMPTY Naomba tumrudishe Kwao Uyu Coz Sidhani Kama kazaliwa Zanzibar Uyu..
Hihihiiihi!
Yaani huwezi amini nikipokea alert/notification ambayo inatoka kwake huwaga naibofya upesi upesi kisha naaza kuisoma post aliyoweka nukta hadi nukta.

Sunbae Damushin,
Tuweke wazi 'sababu mabandiko/posts zako sio za nchi hii.
 
chombo kimoja cha habari kinachoandika taarifa mahususi zinazohusu tasnia ya uigizaji nchini korea leo hii kimeripoti ya kwamba mwanadada jang na ra amepata ofa ya kuigiza kupitia drama inayokwenda kwa jina la Dog, witch and me.
kwa ufupi jang na ra ataigiza uhusika wa mwanamke ambaye ni mlemavu wa macho ambaye alikuwa na upendo mkubwa kwa mnyama wake.
wakati huo huo Rawon Culture ambayo ni kampuni inayomsimamia jang nara wamethibitisha taarifa hizo lakini hakuna makubaliano yoyote yaliofikiwa mpaka sasa kwani mteja wao ana offer nyingi sana.
kama jang nara atakubali kushiriki kwenye drama hii itakuwa ni project yake ya kwanza kwa mwaka 2018,mwaka uliopita alishiriki drama inayojulikana kwa jina la go back couple
dca9c647e6e865a99523903cfbc500c2--jang-nara-fated-to-love-you.jpg
Hiii Signature Yako Duuh.
 
  • ngoja nami niihifadhi kabisa ila sitaiangalia kwa leo.
  • hwayugi episode ya sita sijaiangalia mpaka muda huu, halafu inashangaza sana drama ya hwayugi inafika jumanne subtitle haijakamilika kuwekwa.
  • nimebahatika kuangalia gu family book, my girlfiend is gumiho, king to hearts na shining inheritance ila project hii ya hwayugi nahisi ndio bora zaidi tokea lee seung gi aanze kazi ya uigizaji.
    w644
  • cha seung won naye ameitendea haki sana nafasi ya ma wang, nilipokuwa naangalia episode ya 5 aliporudi kwenye dunia ya mwaka 1930 wakati sam jang alipopigwa risasi kwa ajili ya kumtafuta mtoto wa kijapan kiukweli nilikuwa natamani ma wang na yule mwanadada anayempenda sana anaitwa na chal nyeo warudi pamoja kwenye dunia ya sasa hivi, ila ndio hivyo fate
    Cha-Seung-Won11.jpg
  • P.K (lee hong ki) na yule mdada bong soon (zombie) wananiburudisha sana uhusika wao
True Ni best drama Kwake, Ukilinganisha Na Family Book.

Umu Ndani Naona Kazidi Vituko Na Ile Kumpenda Jin Sun Min Bila Mwenyewe Kutaka Ndo Inayoreta Utamu Wa Drama.
PK Na BU-JA Ni Vituko Kiukweli Na PK anavyojua Kuwasumbua Kina Oh Song Na Ma Wang.Hahahahah!
 
Hihihiiihi!
Yaani huwezi amini nikipokea alert/notification ambayo inatoka kwake huwaga naibofya upesi upesi kisha naaza kuisoma post aliyoweka nukta hadi nukta.

Sunbae Damushin,
Tuweke wazi 'sababu mabandiko/posts zako sio za nchi hii.
Tumrudishe Kwao Tuuh Uyu Wala Si Mwenzetu.
 
leo nataka nianze kuiangalia drama ya Admiral Yi SOON SHIN (joseon naval commander)
https://ondramanice.io/drama/the-immortal-yi-soon-shin-detail
img_0143.jpg

Hahahahaahhaaaaaa Damushin Shukrani sana ndugu umenikumbusha mbali sana kwa bandiko lako hili. Hii Drama nakumbuka niliangalia mwaka 2015 tena sikuimaliza sikumbuki ata nilihishia episode ya ngapi. Hahaha hii Drama ilinitesa sana nakumbuka nilikuwa naenda kuitizama kwa rafiki yangu kila siku ilipo kuwa ikifika saa 3 usiku tunashusha kama episodes 2 ama 3 kisha ndio naenda kulala. Nakumbuka nilihama yale maeneo ndio ikawa mwisho wa kuifuatilia hii kitu, aisee leo nimekutana na bandiko lake humu hahaaa safi sana kiongozi.

The Immortal Yi Soon Shin Bonge moja la Drama kama unasikia vita basi hii kitu ni fire. Vita ambayo inapigwa humo ni hatari, yaani kwa ubabe wa kamanda yule ni balaa tupu. Hahisi waJapan wakimkumbuka wanatikisa kichwa na kusema kweli alikuwa mwanaume wa shoka. Aisee yule kamanda alikuwa ni mbabe balaa yy kuhusu vita haogopi ndio kwanza anapeleka jeshi mbele, ule ubabe sijawahi uona. Mpaka kuitwa Joseon Naval Commander si kitu kidogo uje.
449432e67eed1f1fe128079b4f8d954f.jpg

Hahahaa umenikumbusha ngoja nikamalizie kipolo changu pendwa cha mda mrefu. Sasa nina kazi mbili Emperor Wang Gun na The Immortal Yi Soon Shin nikamaliza hizi nitashusha Age Of Warriors. Kuhusu Ongoing Drama saizi siangaliii kabisa ngoja kwanza ziwe complete ndio nitazirudia, sikumbuki ata drama ya mwisho kuangalia ilikuwa ipi kati ya hizo Ongoing.

Hahahahaahhaaaaaa Damushin agiza kinywaji nakuja kulipia.
 
Nitajie dramas zako bora za miaka yote ambazo umewahi kuziona.
Nataka nione taste yako. Hihihihihi.
Zile Drama Ndo Hizi kwa Ninazozikumbuka.
Jumong
The Land of Wind
Emperor of The Sea
Gu Family Book
Empress Ki
Kings 2 Hearts
Night Watch Man
Scholar who Walks The Night
DOTS
Blood
Doctors
Faith
Personal Taste
The Heirs
Healer
K2
City Hunter
The Legends of the Blue Sea
Criminals Mind
Six Fly Dragon
Suspicious Partner
Remember
The King In Love
Moorim School
Cheese In The Trap
Goblin
Uncontrollably fond
My Love from Another Star
It's OK,This is Love
Warrior Baek Dong So
Rebel.Thief who stole the People
Ruler Master of the Mask
Moon Lovers Scarlet Heart Ryeo
Queen 4 7 Days
While You Were Sleeping
W
My Sassy Girl
Entertainment
Reunited World
You're All Surrounded
SCHOOL 2017
Cinderella & 4 Knights
Money flower - Ongoing
Black
Hwayugi - Ongoing
My Girlfriend Is Gumio
I'm Not A robot - Ongoing
Black Knight - Ongoing
 
Asante sana! Ila umenisababishia kukesha maana huu mzigo bila nihgt bando hausogei hautoboi
 
mjr95 ,EMPTY dongsaeng,aminas noona hii tabia yenu ya kuniambia niagize kinywaji halafu mutakuja kulipa huku kwetu haikubaliki kwa sababu kila mwenye duka kwenye mlango wake ameweka tangazo linalosomeka;
  • mkopo kesho
  • mkopo adui
  • mkopo hauna shehe wala askofu
 
Back
Top Bottom