EMPTY
JF-Expert Member
- Dec 14, 2011
- 979
- 1,195
Hii drama naisubirua kwa hamu.lee bo young alibubujikwa na machozi wakati alipokuwa akielezea sababu iliompelekea akubali offer ya kushiriki kwenye drama inayojulikana kwa jina la mother ambayo itaonyeshwa kupitia kituo cha TVN siku ya jumatano na alhamisi, bo young alisema kwake yeye jambo la muhimu zaidi ni muonekano wake kwenye jamii kuliko viewer ship rating ya drama.
baada ya kufanikiwa kupata mtoto wangu kiukweli makala zinazozungumzia unyanyasaji wa watoto nimekuwa nikizifuatilia sana
wakati napokea ofa hii kulikuwa na kesi takribani tatu zinazohusu unyanyasaji wa watoto na kutelekezwa, suala hili lilizidi kuimarisha uamuzi wangu wa kukubali ofa hii.
ni wajibu wetu kuhakikisha tunakuwa karibu na watoto ili kuwaepusha na unyanyasaji na kutelekezwa.
lee bo young ameigiza uhusika wa mwalimu ambaye anaamua kukimbia na mtoto wa kike mwenye miaka 8 ambaye ametelekezwa na mama yake.
lee pia ameongeza kwa kusema nilikuwa na wasiwasi mkubwa sana kwa heo yool ambaye anaigiza nafasi ya mtoto hususan vipande vya uigizaji wa drama, nilikuwa na wasi wasi juu yake huenda akaingiwa na mshituko pamoja na hofu.
nilikaa pamoja na film staff na kulijadili suala hili na kuona jinsi gani tunaweza kumsaidia ili aweze kutofautisha kati ya maisha ya ukweli na maisha ya uigizaji,
namshukuru mungu ni mtoto ambaye yupo vizuri sana kimaarifa na kiukweli yupo vizuri.
Natarajia itakuwa poa kama 'Oh My Gum Bi'.