Kwa wapenzi wa Korean Dramas, hii ni thread yako!

Hahaaa Damushin Sunbae unavituko ww sasa hapo kuna ushawishi gani.? Yah, walipendana sana toka utotoni japo mwanzo walimnyanyapa sana kutokana na kuwa muoga na aliye kuwa anaonekana hajui kitu. Mpaka yule rafiki yake mwingine akawa nae bega kwa bega na kuhakikisha anajisikia amani na furaha kama wenzake. Kinacho nifurahisha ni yule rafiki yake aliyekuwa akimtenga baadae akaja kumuelewa na kushika urafiki imara sasa wakawa watu watatu Hahaa.

Bado najiuliza ile risasi iliyo mpata Admiral Yi Soon Shin kifuani je, ilimfanya akapoteza uhai ama ilikuwaje? Na je, ile series inaanza katika vita zile zilikuwa vita za mwishoni ama? Na inamaana baada ya kuanza kuona maisha yake inamaana mbeleni tutaenda alafu tufike pale tulipo komea kwenye tukio la Admiral Yi Soon Shin risasi inampata?
 
Damushin Sunbae bila kupoteza mda ikiwezekana kesho naishusha hii Drama The book of corrections Jingbirok. Mkuu kuna andiko hapo page za nyuma umeshuka mpaka nimekuogopa aisee.
 
Ah! mwenzio hapa sijui nimejichanganya nini nikaanza kuitafuta drama moja hivi niidownload inaitwa Misty ,basi kila niki search siioni hadi kwenda kutizama vizuri kumbe inatoka Feb 2 ipo kwenye list yangu ya drama nazozisubiri kwa hamu.
 
Ah! mwenzio hapa sijui nimejichanganya nini nikaanza kuitafuta drama moja hivi niidownload inaitwa Misty ,basi kila niki search siioni hadi kwenda kutizama vizuri kumbe inatoka Feb 2 ipo kwenye list yangu ya drama nazozisubiri kwa hamu.
Hahaaa kweli leo umepatikana haswaa. Vp ni nzuri ili niongeze katika lisiti yangu pia.
 
Damushin Kuna Kitu Nakifatilia Kuhusu Nyuma Ya Kpop Coz Hii Ndo Nimeona Watu Wengi Wanaongelea Tofauti Na Kdrama.
Kuna Madudu Sana Kwenye Hii Kitu
Kweli Kila Penye Nzuri Kuna Bays.
aminas noona kwa ajili yako imenibidi nami leo nianze kufuatilia habari zinazohusu tasnia ya muziki wa kpop ili nami nipate kujifunza yalio nyuma ya pazia.
kwa kuanza nimeona niweke habari hii ilioripotiwa mwezi march 2017 na mtandao mmoja maarufu unaoandika habari za korean entertainment. ninaomba radhi kwa tafsiri isiyo rasmi ya kiswahili, hii lugha ya kiingereza huku kwetu pwani imekuja kwa majahazi ndio maana imezidi kuwa ngumu kuielewa.
niliwahi kukutana na mzungu akaniuliza
what is your name?
nikamjibu: your name is Damushin
aigooooo kupatwa kwa kiingilishi
nikipita wasaa nitaweka kila nitakachokiona kwenye mtandao ambacho hakivunji sheria na utamaduni wa mama Tanzania.

8 Major Entertainment Companies Face Reforms In Unfair Contract Clauses
takribani makampuni 8 yanayojishughulisha na masuala ya sanaa nchini korea yamegundulikana kuwa yameingia mikataba ya kitumwa (slave contract) na waliowaajiri (trainees)
taasisi ya Korea Fair Trade Commission (KFTC) walifanya uchunguzi wao kupitia makampuni 8 yanayokadiriwa kumiliki asset zenye thamani ya zaidi ya won 12 billion (takribani $10 million).
na kuamua kuvirekebisha vifungu sita vya mkataba ambavyo havimpi haki muajiriwa.
baadhi ya makampuni yaliotajwa ni pamoja na SM Entertainment, YG Entertainment, JYP Entertainment, Loen Entertainment, FNC Entertainment, Cube Entertainment, Jellyfish Entertainment,na DSP Media.

baadhi ya vifungu vilivyobadilishwa
  1. adhabu kubwa kwa mwenye kuvunja mkataba :kwa mujibu wa KFTC makampuni makubwa kama vile SM entertainment, JYP entertainment na mengineo wameweka kifungu cha sheria kinachomtaka yoyote atakayevunja mkataba wake basi anapaswa kulipa gharama mara mbili au tatu zaidi ya gharama zilizotumika katika kumsimamia muajiriwa,kwa kuzingatia mkataba wa kawaida ni takribani miaka mitatu inakadiriwa adhabu itakuwa si chini ya won million 150($130500).KFTC wao wametoa mapendekezo ya kivungu hicho kibadilishwe na kwamba trainee atakayevunja mkataba basi anapaswa alipe kiasi cha gharama zilizotumika katika kumhudumikia.
  2. kuwalazimisha wasanii kuongeza mikataba yao baada ya mkataba wa mwanzo kuisha muda wake:JYP Entertainment, Cube Entertainment, na DSP Media wamekuwa wakiwalazimisha wasanii kuongeza mikataba yao au kuwalazimisha kulipa mara mbili ya kiwango cha pesa walichowekeza juu yao.KFTC kwa upande wao wamebadilisha kifungu hiki na kuzitaka kampuni zinazojoshuhulisha na masuala ya burudani kufanya mazungumzo ya awali na wasanii pindi mkataba unapomalizika.
  3. makampuni kuwa na mamlaka ya kuvunja mkataba bila ya kumpa taarifa au kumshirikisha muajiriwa:kifungu hiki kinawapa mamlaka makampuni kuvunja mikataba na waajiriwa wao bila ya kumshirikisha muajiriwa, kifungu hiki kimebadilishwa hivyo basi pande zote mbili zina mamlaka ya kukaa pamoja na kusuluhisha mgogoro.miongoni mwa makampuni ambayo waliweka kifungu hiki ni pamoja na Loen Entertainment, YG Entertainment, Cube Entertainment, JYP Entertainment, na DSP Media.
  4. kuvunja mkataba bila sababu maalumu (ambigous reason): kifungu hiki kinawaruhusu makampuni kuvunja mikataba na wateja wao bila ya sababu zilizowazi nacho pia kimeondolewa,miongoni mwa makampuni ambayo waliweka kifungu hiki ni pamoja na SM Entertainment, FNC Entertainment, na DSP Media
  5. kuwalazimisha trainees kulipa adhabu au faini kwa haraka:kifungu hiki nacho kimebadilishwa juu ya ukiukwaji wa mkataba ili kufuata na kulinda haki za kiraia za nchi ya korea.
 
Song Seung Heon And Liu Yi Fei Confirmed To Have Broken Up
wawakilishi wa muigizaji song seung hun leo hii wamethibitisha taarifa za mteja wao kuachana na muigizaji mwenye asili ya nchini china anayejulikana kwa jina la liu yi fei.
ni kweli wameachana na suala hilo ni lao binafsi na sisi hatujui sababu zilizowapelekea kuachana.
wawili hao walitangaza mahusiano yao mnamo mwaka 2015 baada ya kukutana pamoja kwenye movie inayokwenda kwa jina la Third love.


NB:
huyu dada nilimpenda kwenye movie ya forbidden kingdom,nimeanza kumuogopa Khantwe noona haiwezekani wapinzani wake wote wanaachwa solemba ila yeye bado anabaki kupendwa.
why always khantwe.

hahahahaaaaa nimecheka sana nilipokuwa nasoma statement ya agency wa song seung hun pale aliposema wawili hao sababu ya kuachana haihusiani na THAAD.
THAAD imeleta mgogoro mkubwa sana kati ya China na Korea jambo ambalo limesababisha China kupiga marufuku masuala yote yenye kuhusu utamaduni wa korea kusini.
 
wenyewe wanaita flash back kama sijakosea, admiral yi soon shin kifo chake kinatokana na kupigwa risasi kwenye vita ya noryang na bila shaka pale ndio itakapokuwa mwisho wa yi soon shin kwa sababu sidhani kama risasi ile itamfanya apone.hivyo basi maisha yake ya mwisho kabla hajakutana na muumba wake tumeshayaona.
We are at the height of battle. Don't let anybody know about my death!
moja kati ya maneno yake ya mwisho kuyazungumza wakati anapigania uhai wa maisha yake baada ya kupigwa risasi.
 
nilibahatika kuiangalia ile episode,ailee kivazi chake alichovaa hmmmmm ila wimbo wake wa
I Will Go To You Like the First Snow
alioimba umetumika kama ost kwenye drama ya goblin.
wasanii wa kiafrika itawachukua muda sana kupata pesa yangu kwa kisingizio cha kuangalia shoo zao, haiwezekani nilipie pesa yangu halafu uniambie mikono juu kila wakati, mara machizi piga keleleeeeeee.
 
jamani hii likizo kwangu mimi itawezekana?
EMPTY dongsaeng umenifanya leo hii kwa hamu yako ya kuisubiri drama ya mother umesababisha niidownload episode 1.
nimejiwekea nisifuatilie drama yoyote mpya isipokuwa viporo vyangu tu na going on kama money flower, hwayugi na black knight ila naona naelekea kushindwa.

mungu jaalia hii drama iwe mbaya mnoooo ili niachane nayo
aaaaaameeeeeeennnnnnnnnn.
 
pale unapojikuta unawasifia lady jay dee, shilole,vanessa mdee na wengineo eti wanajua kuimba na kuacha kumsifia mwanadamu kama huyu kwa kisingizio cha uzalendo.acha tu niendelee kutokuwa mzalendo na nipo tayari kupokea hata adhabu ya bakora 100 kwa kosa la kutokufuatilia muziki wetu.
aminas noona sijui nishawahi kukusifia huyu kiumbe anayeitwa so hyang?
 
Iko sikitisha Sana.
Kuna Page Moja Nimeona Wakisema kuwa Kama unamoyo Mdogo Achana Nayo,Ila ni Nzuri Though Sijaiona.
 
Doooh! Love Ni Ngumu Sana..
 

The End..

Ni Time Ya Awa Watu Sasa Kupumzika Duuhh!
2017 Wameitendea Haki Ikiwa Na Mafanikio Kibwena.
Wawe Na Gud Time Sa Ivi, Ama Wajipe Break..
 


Nchi Ina Baridi Hii..Niliona Juzi Kwenye Page Ya Seung Gi Akionyesha Nyuzi Joto Lao Kwa Siku Ile Ilikuwa 13

Na Awa WameFanya Hii Kazi Kwenye Baridi Sana.
 
Hehehe niacheni nijinafasi wapi aminas unakumbuka lile agano letu [emoji23]
 
baada ya takribani miaka 4 mwanadada anayejulikana kwa kina la han hye jin hatimaye amerudi tena kwenye ulimwengu wa uigizaji baada ya kukubali ofa ya kuwa muigizaji mkuu wa kike kwenye drama inayoitwa “Let’s Look at the Sunset Holding Hands" ambayo itaonyeshwa na shirika la MBC

Ni drama inayozungumzia simulizi nzuri yenye kuvutia inayowahusu wanandoa wawili ambao wanaamua kurudisha upendo wao waliokuwa nao baada ya kukabiliana na kifo (confronting the matter of death).
Nam Hyun Joo ni msichana aliyetokezea kumpenda mvulana tokea walipokuwa chuo kikuu, katikati ya maisha yao ya ndoa anaamua kuachana na mume wake na kuamua kwenda kutafuta upendo sehemu nyengine kwa ajili ya kutumia siku zake za mwisho wa uhai wake akiwa kwenye hali ya furaha na utukufu.
drama hii itakuwa ni ingizo jipya kwa mwezi Machi.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…