baada ya takribani miaka 4 mwanadada anayejulikana kwa kina la han hye jin hatimaye amerudi tena kwenye ulimwengu wa uigizaji baada ya kukubali ofa ya kuwa muigizaji mkuu wa kike kwenye drama inayoitwa
“Let’s Look at the Sunset Holding Hands" ambayo itaonyeshwa na shirika la MBC
Ni drama inayozungumzia simulizi nzuri yenye kuvutia inayowahusu wanandoa wawili ambao wanaamua kurudisha upendo wao waliokuwa nao baada ya kukabiliana na kifo (confronting the matter of death).
Nam Hyun Joo ni msichana aliyetokezea kumpenda mvulana tokea walipokuwa chuo kikuu, katikati ya maisha yao ya ndoa anaamua kuachana na mume wake na kuamua kwenda kutafuta upendo sehemu nyengine kwa ajili ya kutumia siku zake za mwisho wa uhai wake akiwa kwenye hali ya furaha na utukufu.
drama hii itakuwa ni ingizo jipya kwa mwezi Machi.