Kwa wapenzi wa Korean Dramas, hii ni thread yako!

https://ondramanice.io/drama/terms-of-endearment-detail

nimemaliza kuangalia drama ya terms of endearment (conditions of love) ni drama ya mwaka 2004 inayozungumzia migogoro na changamoto zinazotokezea ndani ya ndoa na pia matatizo yanayotokezea pindi mwanamke anapoamua kuishi kinyumba na mwanamme asiyemuaminifu bila ya kufunga ndoa na bila wazazi kutambua (huku kwetu tunaita kusomana tabia). Nimeiweka kwenye rekodi kuwa ni miongoni mwa tamthilia iliyonifanya nilie kama nimepigwa na mwalimu wa madrassa nilipokuwa naiangalia.

Kang Han Geol ni mzee aliyekuwa na watoto wa tatu wa kike,kang geunpah,kang eunpah na kang jin pah. Kang geun pah ndie mtoto wa kwanza kuzaliwa aliolewa na mwanamme ambae alikuwa ni wakili Jin jung han,mwanzoni mwa maisha yao waliishi kwa raha na upendo wa hali ya juu na walibahatika kupata mtoto wa kiume walimwita jina la sukbin,ila baadae maisha yao ya ndoa yalibadilika baada ya jin jung han kuwa na michepuko na mfanyakazi mwenziwe jambo hilo lilimuumiza sana kang geun pah mpaka siku moja akamfumania mumewe akiwa na mchepuko wake hotelini ila kwa ujasiri akaamua kuvumilia bila ya kuiambia familia yake wakati huo mume wake alikuwa hajamalizia kujenga nyumba yao kwa hivyo walikuwa wakiishi apartment ya mzee kang han geol.

geun pah aliamini mume wake anaweza kurudisha upendo wake wa zamani kwake yeye na familia yake kwa ujumla ila hali ilizidi kuwa mbaya na kufika mahali mume wake alikuwa anarudi usiku wa manane akiwa amelewa.mambo yalizidi kuwa mabaya ndani ya ndoa yao baada ya geun pah naye kushindwa kuvumilia vitendo vya mumewe na yeye kujikuta akiingia kwenye dimbwi la michepuko na kuwa na uhusiano wa karibuni na mwanamme mwengine hadi siku moja mume wake akamfumania na mwanamme balaa likaanzia hapo wakaamua kuachana ila mwishoni walirudiana na mapenzi yao yakaimarika tena.

Kang eun pah ndie alikuwa mtoto wa mwisho kuzaliwa ambaye naye maisha yake ya kimapenzi yalikuwa mabaya,ni mwanamke aliyependana sana na yun taek na wote walisoma pamoja na walikuwa na ndoto ya kuwa walimu ila mahusiano yao hawakuweza kuzaa matunda kwani eun pah alijikuta akiwa na mahusiano na mwanamme mwengine baada ya yun tek kwenda kutumikia jeshi kwa miaka miwili, eun pah alijingiza kwenye mahusiano na jung san ki na aliishi nae miaka miwili pasina kufunga nae ndoa na hakuwa mwanamme muwajibikaji jambo lililomfanya kang eun pah kujituma yeye zaidi. baada ya kusomana tabia kwa muda mrefu eun pah alipata ujauzito jambo lililosababisha familia yake kuchukizwa na mwishoni familia ikataka jung san ki amuoe eun pah ili wafiche aibu ya binti wao kuzaa nje ya ndoa lakini siku ya ndoa jamaa aliingia mitini (alikimbia kwenye sherehe ya harusi) baadae eun pah alilazimishwa na familia atoe ile mimba yake kwa sababu mtoto angelikosa matunzo ya baba.

Maisha yaliendelea hadi siku moja eun pah akakutana na mwanamme mwengine ambaye alikuwa ni jang soo ambaye mwanzo alikuwa marekani kwa masomo alikuwa anatokea kwenye familia ya kitajiri,jang soo alivutiwa mno na eun pah ila mwanzo eun pah hakumpenda jang soo kwa kuhofia yatamkuta kama ya yaliyomkuta kwa jung san ki, ila kadri maisha yalivyosogea mapenzi yao yalikuwa ya furaha na amani ila kikwazo ikawa ni wazee wa jangsoo hawakuvutiwa na eun pah kwa kuwa ni masikini na pia alikuwa ameajiriwa kwenye kitengo cha kulelea watoto kinachomilikiwa na mama yake jang soo ila jang soo alikataa maamuzi ya mama yake na kuamua kutangaza ndoa,kosa kubwa alilofanya eun pah ni kutokumueleza ukweli jang soo kuhusu maisha yake ya zamani kwani maisha yalikuja kuwa mabaya kwake baada ya jang soo kujuwa maisha ya zamani ya mke wake ambaye ni eun pah na kupelekea mgogoro wa ndoa kumkumba eun pah na familia yake. Jang soo alikuwa ni mwanamme aliyeonyesha mapenzi ya dhati kwake na hata kufikia kumsamehe mke wake kwa kushindwa kumwambia ukweli ila tatizo likawa kwa familia ya jangsoo wao hawakutaka kumwona eun pah akiwa na mtoto wao.

Pia nimevutiwa na original sound track (ost) zilizotumika ni nzuri sana.

Cast member

chae si raa - kang geun pah
han ga in - kang eun pah
ji sung - yun tek
lee jung won -jung han
song il kook - jang soo (kuanzia episode ya 25)

kbs drama awards 2004

song il kook na han ga in (best couple)

NB:
kwa wale masikini kama mimi tafadhali utakapoanza kuiangalia drama hii tafuta tambara la kujifutia machozi
 
Suzy na nam joo hyuk huenda wakashiriki kwenye drama inayokwenda kwa jina la come hug me ambayo itaonyeshwa na kituo cha MBC.
kwa mujibu wa taarifa kutoka MBC wawili hao tayari wamepokea ofa lakini bado hawajathibitisha kushiriki kwao kwenye drama.
come hug me inategemewa kuonyeshwa mwezi wa May.


NB:
huyu bwege nilimchukia sana kwenye drama ya bride of the water god, uhusika wake pamoja na shin se kyung ulikuwa unaboa sana kuliko kusikiliza hotuba za juma pombe maharage suala lililopelekea niishie episode ya pili tu.
ukwelli bado hajastahili kuigiza nafasi ya muigizaji mkuu ila ngoja tusubiri project hii huenda akabadilika.
kama ni mimi siwezi kuwaweka pamoja bae suzy na nam joo hyuk kwenye drama moja kwa sababu wote bado uwezo wao ni wa kawaida.
 
Kim Min Kyu Talks About Working With Chae Soo Bin In Their Second Drama Together
kwenye drama ya Im not a robot iliyoonyeshwa na kituo cha MBC kim min kyu ameigiza uhusika wa robot engineering na kufanikiwa kutimiza ndoto yake ya kushiriki kwenye drama zinazoonyeshwa na mashirika ya umma.
kufanya kazi na muigizaji mzoefu kama uhm ki joon ni jambo la heshima sana, wakat tulipokuwa tukiigiza kwenye timu yetu ya santi maria kiukweli tulionyesha ushirikiano mkubwa sana kama ni familia moja.

kwa mara ya kwanza nilipokutana na chae soo bin kwenye KBS special drama inayoitwa If We Were A Season nilimuona ni msichana anayejituma sana ili kufikia mafanikio makubwa katika tasnia ya uigizaji, soo bin ni mrembo katika maisha ya kawaida ila ni mrembo zaidi anapoigiza uhusika wa robot (aji 3).
nilipokuwa shuleni kiukweli sikuwa na ndoto ya kuwa muigizaji lakini baada ya kuangalia movie inayoitwa Memories of a Murderer nilianza kuvutiwa na sanaa ya uigizaji.
kim min kyu atashiriki kwenye drama inayokwenda kwa jina la clean with passion for now ambayo itaonyeshwa na kituo cha JTBC.
NB:
Kuna kim min kyu mwengine nchini korea, usije ukachanganya chai na pombe, kama umeangalia because this is my first life hii sura utakuwa unaikumbuka
 
dah hii drama nitaangalia nikiwa myself kwenye my room
 
aigoooooo mjr95 andiko lako limenikumbusha mbali na limenifanya nicheke sana, nimekumbuka wakati naanza kuangalia korean drama bado ushamba umenizidi nilikuwa najiuliza swali kama la kwako wewe.
hahahahhaaa kwa kuanzia kwenye drama ya the book of three han mwanzo nilifikiri drama ile imeigizwa na waigizaji wawili tofauti kwenye uhusika wa jumong kumbe masikini nilikuwa najidanganya.
inawezekanaje muigizaji mmoja kuigiza tabia tatu au zaidi?
nilikuwa naamini jumong yule aliyekuwa prince na
jumong aliyekuwa general wa dae mul army ni watu wawili tofauti kwa sababu nilikuwa nahisi hawafanani kitabia na hata uzungumzaji wao unatofautiana.
nadhani sababu kubwa ni muigizaji mwenye jinsi gani anavyoweza kujitofautisha kutokana na muda na nafasi anayoigiza na suala hili linachangiwa zaidi na vipodozi wanavyotumia (make up).

kuhusiana na song il kook mashabiki wanasema ni mwanadamu mwenye sura 100, ni ngumu sana kuamini kama ndio yeye aliyeigiza kwenye emperor of the sea, jumong na kingdom of the wind na hata a man called a god.
ukiangalia kingdom of the wind kabla hajaweka ndevu anaonekana ni mzembe mzembe kama alivyokuwa prince kwenye jumong.
ni mwanadamu mwenye mwili mmoja lakini nafsi nyingi.
je wajua muigizaji oh yeon soo aliyeigiza nafasi ya lady yuhwa (mama yake jumong) amezaliwa mwaka mmoja na song il kook na wote kwa wakati ule walikuwa na miaka 34.

achana na song il kook muigizaji mwengine ni choi soo jong ndio amezidi kuonekana na umri mdogo anapoigiza. kwenye emperor wang gun alikuwa na miaka 41, emperor of the sea alikuwa na miaka 44, dae jo young miaka 46, lakini ana uwezo wa kuigiza uhusika wa kijana bila ya wasi wasi wowote. wenyewe wanamwita the time machine actor.
 
  • 3/02/2018 : money flower drama final episode
  • 8/02/2018 : black knight drama final episode.
  • duh nitabakisha hwayugi drama tu ndio nitakayoendelea kuiangalia
aigooo vyuma vishaanza kukaza kwangu mimi, hii likizo ya wafanyakazi wa tanzania awamu hii ya tano kumbe hata kisafisha viatu hupewi.
tafadhalini nitafutieni drama ya kuangalia hata kama ni ya mwaka 1980
eottokkeeeeeeeeee
 
naomba unisifie kwanza ndipo angalau nifikirie kuitafuta, niliwahi kusoma andiko linaloihusu drama hiyo ambayo ameigiza park hyung sik.
Damushin Siisifiii Ila Ina Iyo Sifa Kipindi Kile Inaonyeshwa Niiliipaga Kisogo Japo ilikuwa Inafanya Vizuri Sana Sana Nazani Ni Drama Ilokuwa Inaongoza Kwa Rating Kwa Wakati Ule.

Niliiweka Kiporo Nikasema Kuwa Lazima Niitazame Nimeanza Jana Mpaka Sa Ivi Nipo Episode Ya 12 Ina Episode 16.

Nimecheka Damushin Mpaka Mbavu Zauuma Now Ndo Naelewa Kwa Nini Ilipendwa Vile Kwa Nini Mashabiki Bado Wanatamni Hii Couple ya ParkPark Iendeleee Mpaka Leo.

Ni Bonge Moja La Drama Ina Kila Kitu Mule Ndani Kila Kitu Yaani..Itakufanya Siku Zisonge Kwa Amani Kidogo Kwa Kipindi Utakachokuwa Unaangalia..Ni Kucheka Mwazo Mwisho Yaani..

Imeifanya Siku Iende Poa Kiukweli Ndani na Nje Ya Nafsi.
Itafute Damushin Puleeeez Iangalie Then Uje Apa Puliiiiiz Chingu.
 
Final Episode ya Black Knight Bado Sijaitazama.
Ila Kiukweli Inastahili Pongezi Kuanzia PD,Writer ,Director,Actors Na Actress Na Wote Walousika

Ni Drama Flani Ivi Ya Kutulia Aina MishiKe Mishike Kiviiilee Wala Kuumiza Kichwa, Ni Ya Kurelax Sana

Rae Won kama Kawa Naona Anakimbizana Na Min Ho na Chang Wook Kwenye Maswala Ya Kupenda Na Sa Ivi Pia Namwona Uyu lead wa Kwenye I'm not Robot Naye Akija Juu Kuwapiku Wakubwa Zake.
Yote Ya Yote Ni Drama Poa Sana Sana.
Money Flower Ngoja Tuone Kesho Ila Kiukweli Damushin Nimempenda Jong Hyuk Umu ndani Mpaka.....
 
Oooooh kumbe! Ngoja zikamilike kabisa kisha nitazishusha nazo pia.
 


Ma Current Fave...
Ni Moja ya Show Yake ya Fan Meeting Hyung Sik (New Bias) Alomualika Idol Wake..Hyo shin (Ma New Bae)
 

Awa Watu Wmefunga Ndoa Leo Lakini Hakuna ata Picha Moja Iliyopatikana Si Kama Ndoa Ya Hye kyo ndo Joong ki Hii Yao Wameitaita Sana.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…