Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
Ungeandika kwa kikorea ndiyo tungejua wewe kweli mkorea mwenzetu.usk mwema wakorea wenzangu
Teh teh tehUngeandika kwa kikorea ndiyo tungejua wewe kweli mkorea mwenzetu.
dah hii drama nitaangalia nikiwa myself kwenye my roomhttps://ondramanice.io/drama/terms-of-endearment-detail
nimemaliza kuangalia drama ya terms of endearment (conditions of love) ni drama ya mwaka 2004 inayozungumzia migogoro na changamoto zinazotokezea ndani ya ndoa na pia matatizo yanayotokezea pindi mwanamke anapoamua kuishi kinyumba na mwanamme asiyemuaminifu bila ya kufunga ndoa na bila wazazi kutambua (huku kwetu tunaita kusomana tabia). Nimeiweka kwenye rekodi kuwa ni miongoni mwa tamthilia iliyonifanya nilie kama nimepigwa na mwalimu wa madrassa nilipokuwa naiangalia.
![]()
Kang Han Geol ni mzee aliyekuwa na watoto wa tatu wa kike,kang geunpah,kang eunpah na kang jin pah. Kang geun pah ndie mtoto wa kwanza kuzaliwa aliolewa na mwanamme ambae alikuwa ni wakili Jin jung han,mwanzoni mwa maisha yao waliishi kwa raha na upendo wa hali ya juu na walibahatika kupata mtoto wa kiume walimwita jina la sukbin,ila baadae maisha yao ya ndoa yalibadilika baada ya jin jung han kuwa na michepuko na mfanyakazi mwenziwe jambo hilo lilimuumiza sana kang geun pah mpaka siku moja akamfumania mumewe akiwa na mchepuko wake hotelini ila kwa ujasiri akaamua kuvumilia bila ya kuiambia familia yake wakati huo mume wake alikuwa hajamalizia kujenga nyumba yao kwa hivyo walikuwa wakiishi apartment ya mzee kang han geol.
![]()
geun pah aliamini mume wake anaweza kurudisha upendo wake wa zamani kwake yeye na familia yake kwa ujumla ila hali ilizidi kuwa mbaya na kufika mahali mume wake alikuwa anarudi usiku wa manane akiwa amelewa.mambo yalizidi kuwa mabaya ndani ya ndoa yao baada ya geun pah naye kushindwa kuvumilia vitendo vya mumewe na yeye kujikuta akiingia kwenye dimbwi la michepuko na kuwa na uhusiano wa karibuni na mwanamme mwengine hadi siku moja mume wake akamfumania na mwanamme balaa likaanzia hapo wakaamua kuachana ila mwishoni walirudiana na mapenzi yao yakaimarika tena.
![]()
Kang eun pah ndie alikuwa mtoto wa mwisho kuzaliwa ambaye naye maisha yake ya kimapenzi yalikuwa mabaya,ni mwanamke aliyependana sana na yun taek na wote walisoma pamoja na walikuwa na ndoto ya kuwa walimu ila mahusiano yao hawakuweza kuzaa matunda kwani eun pah alijikuta akiwa na mahusiano na mwanamme mwengine baada ya yun tek kwenda kutumikia jeshi kwa miaka miwili, eun pah alijingiza kwenye mahusiano na jung san ki na aliishi nae miaka miwili pasina kufunga nae ndoa na hakuwa mwanamme muwajibikaji jambo lililomfanya kang eun pah kujituma yeye zaidi. baada ya kusomana tabia kwa muda mrefu eun pah alipata ujauzito jambo lililosababisha familia yake kuchukizwa na mwishoni familia ikataka jung san ki amuoe eun pah ili wafiche aibu ya binti wao kuzaa nje ya ndoa lakini siku ya ndoa jamaa aliingia mitini (alikimbia kwenye sherehe ya harusi) baadae eun pah alilazimishwa na familia atoe ile mimba yake kwa sababu mtoto angelikosa matunzo ya baba.
![]()
Maisha yaliendelea hadi siku moja eun pah akakutana na mwanamme mwengine ambaye alikuwa ni jang soo ambaye mwanzo alikuwa marekani kwa masomo alikuwa anatokea kwenye familia ya kitajiri,jang soo alivutiwa mno na eun pah ila mwanzo eun pah hakumpenda jang soo kwa kuhofia yatamkuta kama ya yaliyomkuta kwa jung san ki, ila kadri maisha yalivyosogea mapenzi yao yalikuwa ya furaha na amani ila kikwazo ikawa ni wazee wa jangsoo hawakuvutiwa na eun pah kwa kuwa ni masikini na pia alikuwa ameajiriwa kwenye kitengo cha kulelea watoto kinachomilikiwa na mama yake jang soo ila jang soo alikataa maamuzi ya mama yake na kuamua kutangaza ndoa,kosa kubwa alilofanya eun pah ni kutokumueleza ukweli jang soo kuhusu maisha yake ya zamani kwani maisha yalikuja kuwa mabaya kwake baada ya jang soo kujuwa maisha ya zamani ya mke wake ambaye ni eun pah na kupelekea mgogoro wa ndoa kumkumba eun pah na familia yake. Jang soo alikuwa ni mwanamme aliyeonyesha mapenzi ya dhati kwake na hata kufikia kumsamehe mke wake kwa kushindwa kumwambia ukweli ila tatizo likawa kwa familia ya jangsoo wao hawakutaka kumwona eun pah akiwa na mtoto wao.
Pia nimevutiwa na original sound track (ost) zilizotumika ni nzuri sana.
Cast member
chae si raa - kang geun pah
han ga in - kang eun pah
ji sung - yun tek
lee jung won -jung han
song il kook - jang soo (kuanzia episode ya 25)
kbs drama awards 2004
song il kook na han ga in (best couple)
NB:
kwa wale masikini kama mimi tafadhali utakapoanza kuiangalia drama hii tafuta tambara la kujifutia machozi
naomba unisifie kwanza ndipo angalau nifikirie kuitafuta, niliwahi kusoma andiko linaloihusu drama hiyo ambayo ameigiza park hyung sik.
Damushin Siisifiii Ila Ina Iyo Sifa Kipindi Kile Inaonyeshwa Niiliipaga Kisogo Japo ilikuwa Inafanya Vizuri Sana Sana Nazani Ni Drama Ilokuwa Inaongoza Kwa Rating Kwa Wakati Ule.naomba unisifie kwanza ndipo angalau nifikirie kuitafuta, niliwahi kusoma andiko linaloihusu drama hiyo ambayo ameigiza park hyung sik.
Final Episode ya Black Knight Bado Sijaitazama.aigooo vyuma vishaanza kukaza kwangu mimi, hii likizo ya wafanyakazi wa tanzania awamu hii ya tano kumbe hata kisafisha viatu hupewi.
- 3/02/2018 : money flower drama final episode
![]()
- 8/02/2018 : black knight drama final episode.
![]()
- duh nitabakisha hwayugi drama tu ndio nitakayoendelea kuiangalia
tafadhalini nitafutieni drama ya kuangalia hata kama ni ya mwaka 1980
eottokkeeeeeeeeee
Oooooh kumbe! Ngoja zikamilike kabisa kisha nitazishusha nazo pia.aigooo vyuma vishaanza kukaza kwangu mimi, hii likizo ya wafanyakazi wa tanzania awamu hii ya tano kumbe hata kisafisha viatu hupewi.
- 3/02/2018 : money flower drama final episode
![]()
- 8/02/2018 : black knight drama final episode.
![]()
- duh nitabakisha hwayugi drama tu ndio nitakayoendelea kuiangalia
tafadhalini nitafutieni drama ya kuangalia hata kama ni ya mwaka 1980
eottokkeeeeeeeeee