Actress Song Ha Neul Testifies On Sexual Harassment + Jo Min Ki Steps Down From Drama
Muigizaji
song ha neul ambaye anafanya shughuli zake kwenye kumbi maalum (theatre) amezungumzia shutuma za unyanyasaji wa kijinsia zinazomkabili muigizaji
jo min ki ambaye pia ni professor wa chuo kikuu.
Ikumbukwe kuwa upande wa chuo umethibitisha ya kwamba wamefanya uchunguzi juu ya suala hilo lakini upande wa jo min ki wamekanusha taarifa hizo na kuzichukulia kama ni uvumi kwa mteja wao, muigizaji huyo anasema vitendo vyake vya kuwagusa wanafuzi na kuwakumbatia (physical touch) hakuwa na malengo ya unyanyasaji wa kijinsia (molestation) ila ni kuwapa morali na matumaini ya kufikia malengo ya mafanikio (encouragement).
lakini upande mwengine siku ya jana muigizaji song ha neul aliandika kwenye ukurasa wake wa facebook kuhusiana na unyanyasaji wa kijinsia anaoufanya jo min ki kwa wanafunzi wake.
" mimi ni rookie actress ambaye ninafanya kazi zangu kwenye kumbi maalum za sanaa, na nilianza kazi baada ya kuhitimu elimu yangu kwenye chuo kikuu cha cheong ju. kiukweli huwa najaribu kusahau mambo yaliopita yaliowahi kunitokezea ila baada ya kusoma taarifa ya jo min ki ambayo anajitetea ya kwamba hana makosa juu ya shutuma za unyanyasaji wa kijinsia nimeshikwa na hasira sana.
mambo ambayo mimi,marafiki na wanafunzi wenzangu tumeyapitia na kuyavumilia sio "victimless rumors" wala sio uvumi na hadithi za kupanga.
mimi si mpumbavu kama nashindwa kutofautisha kati ya unyanyasaji wa kingono (molestation) na vitendo vya kumpa mtu morali (encouragement).kiukweli tumekutana na vitendo vingi vya unyanyasaji wa kijinsia ila niliogopa kuzungumzia suala hili hadharani na mpaka sasa pia naogopa kulizungumzia suala hilo lakini kama nitaendelea kuogopa kuna waathirika wengi wataendelea kuishi kwa uoga na khofu ndio maana leo nimeamua kulizungumzia suala hili.
mwaka 2013 wakati naingia chuoni walionizidi walinitahadharisha kuwa makini na jo min ki kuhusiana na vitendo vyake,lakini kwetu sisi wanafunzi tuliokuwa tunajifunza kuwa waigizaji wa theatre Professor jo min ki alikuwa na nguvu sana hivyo basi hakuna ambaye alithubutu kulalamikia vitendo vyake chuoni kwa sababu yeye alikuwa ni kama mfalme kwenye campus yetu na pia ni muigizaji mkubwa sana.
professor jo min ki alikuwa na officetel yake karibu na kampasi ya chuo hivyo basi alipokuwa anakuja kusomesha mara kwa mara alikuwa akiwaalika wanafunzi wa kike kwenye officetel yake wakati wa usiku, na alikuwa akiwaambia wanakwenda kujadili kuhusiana na uigizaji na masomo. njia pekee ya kuepukana na kadhia yake ilikuwa ni kwenda pamoja na marafiki zetu.
tulipokuwa tunakwenda mara nyingi alitaka tulale kwenye apartment yake na alitupa miswaki na nguo za kubadilisha. siku moja mimi na rafiki yangu tuliingia chooni na kufungua mfereji ili asisikie mazungumzo yetu wakati tulipokuwa tunajadili jinsi gani ya kuweza kutoroka ila tulishindwa kupata njia ya kutoroka hivyo basi baada ya kutoka chooni aliitulazimisha kulala kwenye kitanda chake.
baada ya hapo alipanda juu yangu na kunipaka lotion usoni huku akiniambia hii ni ya gharama sana na kiukweli sikuwa na chakufanya na akalala katikati yetu na kuanza kutupapasa na kuweka mikono yake kwenye viuno vyetu na aliendelea kufanya vitendo hivyo mara kwa mara na mpaka alipopata usingizi asubuhi yake tuliweza kuondoka
siku moja aliniita tena ofisini kwake lakini nikaamua kwenda na boyfirend wangu lakini bahati mbaya boyfriend wangu alikuwa ni dhaifu kwenye ulevi hivyo basi alipatwa na usingizi baada ya kulewa,niliogopa kwa kuhofia jambo baya litatokezea na sitopata msaada.
professor akaanza kuniuliza maswali kuhusiana na boyfriend wangu na mahusiano yetu
je tunafanya mapenzi mara ngapi kwa wiki
nilishikwa na aibu ila niliishia kucheka na nilijiapia siku hiyo nisilewe.Baadae jo min ki alikwenda kitandani baada ya kulewa na nilijaribu kumuamsha mpenzi wangu lakini hakuamka,professor akaniita chumbani kwake na ghafla akaanza kunigusa kifuani kwangu na nilipoanza kujipapatua akanicheka na kuniambia kumbe matiti yangu ni madogo sana kuliko nilivyodhania.
nilikereka sana nikaamua kumuamsha mpenzi wangu na kutoka kwenye officetel, siku ya pili tulipoonana alijifanya kama hakuna chochote kilichotokea usiku wa jana.
aliendelea kutuita ofisini kwake mara kwa mara na kutulazimisha tunywe pombe na siku moja senior student alilewa sana na kushindwa kujielewa baadae akatulazimisha tuondoke na kumlaza mwenzetu chumbani kwake lakini mimi nilikataa na nikalazimisha kuondoka na mwanafunzi mwenzetu jambo lililomkera jo min ki na kunitishia ya kwamba atanidhalilisha mbele ya hadhara.
mwaka 2014 tulikwenda karaoke room na jo min ki akaanza kutukumbutia kwa kutumia kisingizio cha kutupa pongezi na kuwataka wanafunzi wa kike kucheza muziki na kuanza kuwagusa sehemu ya kifua bila ya kujali kama yupo mbele yetu na alimvuta mwanafunzi mmoja ukutani na kumweka style ya kufanya mapenzi.
wakati tulipomuaga alikamata uso wangu na alinipiga busu la mdomo, kiukweli alitufanyia vitendo vingi vya kingono na mara nyingi ninapowaeleza watu yangu najihisi kama ni makosa yangu mwenyewe ila kwa sasa nimeifunza ya kwamba hayakuwa ni makosa yangu.
kiukweli waathirika wa vitendo hivi hawapaswi kuwa kimya na mtuhumiwa hapaswi kulindwa.
NB:
In South Korea, an
officetel (Korean: 오피스텔, a portmanteau of 'office' and 'hotel'), is a multi-purpose building with residential and commercial units. This is a type of studio apartment or studio flat.