Kwa wapenzi wa Korean Dramas, hii ni thread yako!

Enyohaseyo*
 
Twende Wote kwenye hiyo likizo.

Robot Anamgeuka Mom Wake.
mhhhhhhhhhhhhh nilichopanga kukifanya kimeenda kinyume na matarajio yangu, ngoja niendelee kupambana na hali yangu.
likizo imebuma dakika za majeruhi kama uingereza na world cup
dongsaeng naomba unikumbushe ile nukuu ya juzi.

yap upo sahihi nam sin amebadilika sana kuanzia episode ya 10 na mabadiliko yake yamechangiwa zaidi na nguvu ya mwanadada so bong alipomtaka ajisimamie yeye mwenyewe bila ya kuendeshwa na kupangiwa cha kufanya.
mama yake anataka awe na nguvu za kuendelea kumpangia kila kitu kwa sababu yeye ndiye aliyemtengeneza.
halafu final epsode ya wiki hii anaonekana binadamu namsin anarudisha nguvu zake baada ya kuzimia kwa muda mrefu (coma).
daebak sijui kitatokezea kitu gani watakapokutana robot na binadamu.
bila ya kusahau nipo team robot na muda si mrefu so bong atakuja kwangu huku akisahau dharau na kejeli alizokuwa akizielekeza kwangu.
ameniita majina mengi sana nimevumilia kama vile
plastic man
slave
mdoli

hakuna maisha bila ya kuhisi njaa hivyo basi ngoja nijipange kama miaka 10 ili nipate kwenda jeju island.
naamini siku moja aliye juu ya kila kitu ataninyanyua na kufikia daraja la juu zaidi ambalo naliota kila siku
 
Jin Goo To Join Ha Ji Won’s New Drama β€œPrometheus” As Male Lead
ataigiza uhusika wa park hoon ambaye ni millitary officer kwenye ubalozi wa korea kaskazini ambaye anajikuta akikabiliwa na changamoto ngumu sana kuhusiana na hatma yake nchini Russia ambako ndio sehemu ya makaazi yake.
β€œPrometheus drama inaanza kwa kuzungumzia tukio la mwanasayansi wa korea kaskazini aliyebobea kwenye masuala ya nuclear ambaye alikuwa anarudishwa nyumbani kwao na hatimaye kupotea jambo linalosababisha zadi ya nchi tano kumtafuta mwanasayansi huyo wa upande wa pyongyang.
park hoon anajikuta akiwa karibu sana na mwanadada Chae Eun Seo ambaye anatokea korea kusini ambao ni upande hasimu wa korea kaskazini, ni mtumishi wa shirika la ujasusi la korea kusini na amepewa kazi ya kuhakikisha anaharibu mipango ya nuclear ya korea kaskazini.
(denuclearize)
bajeti ya drama hii inakadiriwa kufikia billioni 60 kwa pesa za tanzania.
kwa jinsi inavyoonekana park hoon atakuwa ni mkorea kaskazini ila sina uhakika
  • je mkorea kasikazini na kusini watashirikiana na kuangamiza mpango wa silaha hatari za kaskazini?.
  • je mkorea kaskazini hataonekana msaliti nchini kwao au ndio korea kaskazini hata raia wake hawafurahishwi na hali iliopo nchini kwao?
  • je hataonekana ameamua kushirikiana na korea kusini kwa sababu ya mapenzi?
bingo
hii drama stori yake imeandikwa mwaka mmoja kabla ya tukio la kihistoria kutokezea ambao mwaka huu tumeshuhudia korea kaskazini, korea kusini na marekani wakifikia hatua kubwa sana ya kimakubaliano juu ya amani ya korean peninsula.
sijui walishapiga ramli na kugundua hili tukio litatokezea mwaka huu hivyo basi waandike hadithi na mapema?
 
β€œFamiliar Wife” Offers Some Clues In Official Posters Of Ji Sung, Han Ji Min

ni drama inayozungumzia maisha ya wanandoa wawili Cha Joo-Hyuk na Seo Woo-Jin ambao wamefunga ndoa takribani miaka 5 iliopita.
cha joo hyuk ni mwanamme anayefanya kazi benki na anajikuta anafanya tukio linalosababisha maisha ya wawili hao kubadilika.
sijui kama aliiba pesa benki na kufungwa?
sijui kama alikutwa na mchepuko na hatimae mama watoto akashindwa kuvumilia?
sijui kama alimfanyia mkewe suprize mbaya baada ya kumpelekea zawadi ambayo aliwahi kumfuma mume wake akimpelekea mchepuko wake
mimi sijui hivyo basi
inshaallah tukutane 1/08/2018 ndani ya kituo cha tvN pindi itakapomalizika drama ya whats wrong with seretary kim ambayo imebakiza episode 4 tu ili imalize.
niwe mkweli licha ya kuwa ji sung ni muigizaji hodari mnoo na ana project nyingi sana ila nimeangalia drama tatu tu ambazo ni defendant, swallow the sun na secret love.
nimeangalia drama mbili tu za mwanadada han ji min ambazo ni cain and abel na yi san ambayo nilifika episode ya 17.
wawili hao walikutana kwa mara ya kwanza kwenye drama ya All in ya mwaka 2003 ambapo ji sung alikuwa second lead actor na han ji min aliigiza nafasi ya youngest version ya muigizaji mkuu wa kike.
muigizaji mkuu alikuwa ni Lee Byung hun
nimemuona jang boo cheon wa money flower kwenye poster


korean drama forever
 
Heri, Karibu Tena.
 
So Bong Anamchanganya Robot Wetu Jamni...Pale Ambapo Anamsikiliza Mwanamke Zaid Ya Mzazi, Na Hii Ndo Uharisia Wa Binadam Anaeitwa Mwanaume Kwao Wanawake Wao Ndo kila Kitu Mbele Ya Mama Zao.
 


wakuuu naomba mnisaidie jina la hii series na pamoja na pakuipata.
Inazungumzia maisha ya Kim Chunchu na Kim Yusin tangu wakiwa wadogo.
Silla na Descendandant of Gaya pamoja na mnyukano na Baekje.
Wausika wakuu ni Kim Yusin,Kim Chunchu,Bihyeong,gold fox etc.
CC aminas , Damushin ,Kazz0 na wadau wengineo
 
Naona KDrama original zinaanza kurudi kwa kasi.
Kila nikirudia rudia kuitazama hiyo scene bado....

Naweza kaa siku nzima naangalia hicho kipande tu.. Daebak!!!

Daebak! Daebak! Dae'bak!
 
πŸ˜€πŸ˜€πŸ˜€gamsahamnidaπŸ˜€πŸ˜€πŸ˜€
 

Umu Ndani Sijuhi Kipi Kinakosekana, Chuki, Dhuruma, Uchu Wa Madaraka, Upendo, Urafiki Wa Kweli, Undugu wa Kweli, Tamaa, Visasi, Vita Na Vinginevyo, Ina Episode 60, Ila Mi Ndo Kwanza Ya 40 Lakini Ni Best Best.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…