Kwa wapenzi wa Korean Dramas, hii ni thread yako!




Huu Uzuri Kumbe Anao Tangu Mtoto, Kim Yoo Jung Alicheza Utoto Wa Cho Dong Yi au Chun Dong Yi
 
Ndg wadau nmetokea kuwa mpenzi sana wa hizi korean dramas hasa za action ila nimekuwa nikipata changamoto ya muda, maana inatokea nakuwa busy kidogo hivyo kushindwa kutazama ila zipo baadhi ambazo nimekwisha zitazama japo si nyingi na niza kitambo kidogo na ndo zilizonishawishi kupenda hizi drama. Kwa sasa nina muda ila nashindwa nitazame ipi nisije jutia muda wangu.


Najua humu kuna watu waliotazama nyingi.
Ni ipi naweza itazama nisijutie muda wangu iwe ya action
 
안녕, 내 친구들 어떻게 지내?
annyeong, nae chingudeul eotteohge jinae?
ni matumaini yangu ni wazima wa afya humu ndani.

hivi yule sungura aliyepotea ameshaonekana huko kwenu?
hivi ile ndege inayofanana na usafiri wa rais wa taifa lenye nguvu duniani imeshaanza safari ya kuelekea visiwa vya jeju?
hivi yule faru khadija bado hajapata mtoto?
jamani zile suti zenye mifuko ya bendera hata korean celebrity nao wameshaanza kushonesha style kama ile.

aminas popote ulipo nakuomba unitafutie mawasiliano ya huyu mwanadada hwang bo - ra.
naona muda si mrefu atanifanya niwe mwendawazimu wa kupenda.
nikila mihogo ya kuchemsha namuona kwenye sahani.
nikinywa chai kavu namuona kwenye kikombe cha plastiki.
nikilala kwenye kitanda changu cha kamba kama mzazi mpya najihisi tumelala pamoja.
nimejikuta naelekea kuwa chizi asiyetibika.
facial expression yake tu inakufanya utamani kuendelea kuangalia kazi zake huyu dada.
ananipa raha sana ninapomuangalia.
nakupa mpaka tarehe 31/07/2018 uwe umeshaniletea mawasiliano ya huyu dada.
 
whats wrong with secretary kim drama
wiki ijayo ndio mwisho wa hii drama inayofanya vizuri sana kila wiki.
aigoooo eotteoghae = 어떡해 (nitafanya nini).
ukija huku kwetu wiki nzima stori kubwa ni mbwa aliyepotea.
nikienda kwenye mpira timu ninayoishabikia haina habari ya kusajili wachezaji.
mwanadada park min young ana bahati sana kwenye project zake anazochagua.
ameshaigiza na waigizaji wengi wenye ushawishi mkubwa sana kwenye soko la burudani nchini korea.
ji chang wook = healer
lee min ho = city hunter
sungkyunkwan scandal = yooh ah in na song joong ki
queen for seven days drama = lee dong gun na yeon woo jin
DR JIN drama = song seung hun
whats wrong with secretary kim = park seo joon
princess jamnyung = jung kyoung ho
remember = yoo seung ho

wamependeza sana humu ndani na itapendeza zaidi kama ukaribu wao utaendelea hadi nje ya kazi na wakauhamishia ndani ya majumba yao.​

ngoja nami nianze mchakato wa kutafuta secretary mwenye mvuto usiomithilika kama kim mi soo
park min young anaonekana ana nyota ya kangi lugola.
 
Song Joong Ki, Kim Ji Won, And Jang Dong Gun Confirmed For New tvN Drama

Asadal
ni historical drama inatakayojikita zaidi kwenye ishu ya siasa, mapenzi na visasi.
ni drama ilioandikwa na waandishi wawili mahiri nchini korea ambao ni Kim Young Hyun na Park Sang Yeon ambao pia waliwahi kushirikiana kuandika drama tofauti kama vile six flying dragons, tree with deep roots, the greet queen seondeok.

pia drama hiyo ya asadal itaongozwa na PD kim won suk ambaye ndiye alisimamia criminal drama ya SIGNAL ambayo ilikuwa ndio drama bora kwa mwaka 2015 pamoja na best drama kwa miezi sita ya mwanzo kwa mwaka 2018 inayoitwa MY AHJUSSI.

Jang Dong Gun
ahjussi au samchon (삼촌)
ambaye project yake ya mwisho ilikuwa ni SUIT ataigiza uhusika wa ta gon ambaye alikuwa ni shujaa wa vita. nimemwita samchon (mjomba) kwa sababu tuna uhusiano wa nje ya damu.

song joong ki
a.k.a bwana harusi ataigiza uhusika wa Eun Sum mtoto aliyezaliwa na nyota ya kuleta majanga kwenye utawala.

kim ji won
naye ataigiza uhusika wa Tan ya ambaye naye pia amezaliwa na nyota mbayaaaaaa ila haishindi nyota ya taifa la T........G.........

kumbuka:

song joong ki na kim ji won walishiriki kwa pamoja kwenye drama inayoitwa descendent of the sun

cha kufurahisha zaidi hawa waigizaji wakuu wote wameshawahi kufanya kazi na mwanama kim eun sook ambaye kwa sasa anakimbiza upepo wa mafanikio kupitia drama ya MR SUNSHINE.
hivi huku kwenu yule sungura aliyepotea bandarini bado hajaonekana?​

jamani hiki kijiwe kimechoka kuliko watumishi wa umma wa serikali ya Somalia.
daebak, mulifikiri nitaitaja serikali ya Tanzania munipeleke kule ambapo watu wanafanyishwa kazi na mateke juu kama mtumwa wa joseon.
 
Last edited:
aminas nimeamua nikuite huku kijiweni kwetu kama una nafasi au nawewe umebanwa na ratiba kiasi ambacho unashindwa hata kutembelea facebukiiiiii na twitteriiiii.
hivi ile amri niliokupa umeshaifanyia kazi?
lazima unapaswa ufahamu ya kwamba damushin huyu ni tofauti na yule aliyekuwa akivaa bendera ya nchi shingoni kwake.
damushin huyu wa sasa hivi bendera ya taifa ameishonea kwenye shati lake hivyo basi ndio ufahamu jinsi gani nilivyo mzalendo wa taifa hili la.

kwenye maisha hutakiwi kupangiwa unachokifanya, fanya maamuzi kutokana na moyo wako kama anavyofanya mpenzi wangu mtarajiwa bong sera. Anavaa anachokipenda iwe miwani, bangili.
nakukumbusha tena nimekupa amri uniletee namba ya simu ya huyu mdada kabla episode ya 16 haijaonyeshwa siku ya leo.
episode ya 14 ilikuwa ndio episode zaidi ya drama hii.

hii drama natamani iongezwe episode 10 zaidi ili nipate kufaidi uhondo wa team work.
sielewi kwanini huyu bonge hana mchumba humu ndani.
 
Huwezi Amini, Nilikuwa Busy Na Dong Yi! Episode Zote Kwa Drama Ninazoziangalia Za Wiki Ilopita Na Wiki Hii Ndo Nimeanza Kuziangalia, Kwaiyo Ata Umu Nilikuwa Napita Nasoma Natoka! Sorry Dear Ndo Ntaanza Kulifanyia Kazi Hitaji Lako.
 


Hawa Majamaa Ni Cheche Nimependa Chemistry Yao.
  1. uyo wa kati kati anajifanya hajali hali ya nchi yake ilivyo ilimradi kwa kuwa maisha yake yanakwenda vizuri. anasahau ya kwamba wakoloni wanapovamia sehemu hawabagui aliyenacho na asiyenacho.
  2. uyo wa pembeni aliyevaa madeepa (deera) kama ahjumma wa kizanzibari moyo wake ameupeleka sehemu ambayo hapendwi na sababu kubwa yule binti anamchukulia kama ni mbwa wa kijapani,anabaki kuumia nafsini mwake na kubaki na hasira za samaki. vurugu nyingi akiwa kwenye bahari lakini dawa yake ni nyavu yenye matobo.
  3. uyo aliyevaa suti kama derick upande wangu wa kulia ameshaanza kuona wivu baada ya kugundua ya kwamba uyo jamaa wa katikati ndiye mchumba wa lady aesin, cheza na njaa ila usicheze na wivu wa kimapenzi, matokeo yake ameanza kusahau kilichomfanya aletwe korea.
Eugene Choi: "No matter where I go, I always end up drawing attention."
kuna uwezekano huyu mzee genius wa historical drama ndiye kiongozi mkuu wa harakati za kudai haki nchini joseon?
nimeikuta soompi thread
anaitwa kim gap soo
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…