Gyeoul
JF-Expert Member
- Jan 28, 2015
- 3,758
- 5,365
HahahahahaMR SUNSHINE DRAMA ep 17
- ukiachana na kiongozi mkuu wowote wa nchi au wa taasisi binafsi, mwanadada go Ae sin ndiye anayeshikilia rekodi ya kuwa na ulinzi mkubwa sana kuliko mtu yoyote duniani. kwenye maisha yake amezungukwa na mashujaa zaidi ya 500 ila wanaojitokeza hadharani kumlinda kwa nyakati tofauti ni eugene choi, goo dong mae, kim huiseong, mwalim Jang Seung-Goo na wafuasi wengineo wa righteous army walioanza kumlinda tokea alipozaliwa na kumuepusha na shambulio la kifo. mhhhhhhhhhh bahati alionayo akiilalia mlango wazi nitamuibia. Nina wasiwasi huyu bidada huenda akawa anatumia ndumba kama za wale bongo celebrities uchwara.
“I chose to not kill because unlike our parents, we have the ability to choose.” kupitia hii nukuu utagundua tofauti nyengine kubwa kati ya goo dong mae na choi eugene.
utakapojifanya siasa ya nchi yako haikuhusu basi fahamu ya kwamba utakuwa ni miongoni mwa wajinga watakaosababisha nchi kuongozwa na watu ambao utakuwa umewazidi kimaarifa, Na maisha yote mpumbavu na mwedawazimu (chizi) ndiyo huzidiwa maarifa na mtu mjinga.
- dong mae aliporudi korea jambo la kwanza alilolifanya kwenye ardhi ya korea ni kuwaua wale wote walisababisha mateso kwa familia yake huku upande wa pili eugne alipotoka marekani licha ya mateso na huzuni kubwa inayoendelea kumuandama kila siku kwa kuuawa wazazi wake wawili bado ameendelea kuzuia hasira dhidi ya maadui wa familia yake. Na ana uwezo wa kulipa kisasi tofauti na wazazi wao ambao hawakuwa na uhuru wa kuchagua jambo lolote kwa sababu ya utumwa wao. kumbe binadamu tunaweza kuepuka kutenda jambo lolote ovu, huwa nawashangaa sana wale wanaomsingizia shetani pindi wanapotenda uovu, Unamnajisi mtoto mdogo baadae unamsingizia shetani. goo dong mae alimjibu they have the ability to choose between a sword or a gun. Hahahahaaaaa dong mae ana maneno ya ovyo kuliko mvuvi.
- nimeyapenda majibu ya eugene choi kwa mama yake kim hee sung, eugene alimwambia hawezi kumbebesha msalaba wa dhambi hui seong kwa sababu yeye hahusiki na dhambi ya familia yake ila bado ataendelea kutokumsamehe baba, mama na hata late grand father kwa matendo yao ya kinyama walioyatenda kwa familia yake. Tukirudi nyuma kwenye episode 1 babu yake kim hui seong yeye alikuwa na mtazamo tofauti, baada ya wazee wake eugene kutenda makosa babu aliamini familia nzima inapaswa ipokee adhabu ya kifo kwa kosa waliloloitenda. Yule harabuji hataiweza kuinusa harufu ya pepo kwa unyama aliyoutenda kwa kitendo chake cha kumbebesha dhambi mtoto mdogo asiyekuwa na hatia yoyote.
- tanzania bado wapo wazalendo wa ukweli kama alivyo mzee go sa hong na joseon yake? nimependa msimamo wake mzee go sahong, yupo tofauti na noble family wengineo ambao wanajifanya hawana muda wa kufuatilia siasa za nchi yao, Ae sin amerithi kila kitu kutoka kwa babu yake ila cha ajabu babu hataki mjukuu wake afuate kivuli chake.Mzee go sa hong amepewa utajiri wa mali, uzalendo,upambanaji, hekima, huruma, busara, elimu. hivi kuna kitu ambacho mzee go sa hong amenyimwa? Kipo alichonyimwa na si chengine isipokuwa bado anaamini nchi inapaswa iwe na utabaka kati ya aliyenacho na asiyekuwa nacho, Ila nimeona picture preview zinazoonyesha mzee go sahong akiwaalika eugene choi na goo dong mae kwenye makaazi yake, unahisi atawaomba kitu wanadamu hao wawili?
sitaki kuzungumzia tukio la kuvunjika mahusiano kati ya ae sin na kim hee seong kwa sababu kuna mtu ameshalijibu tukio lile kwa kutolea mfano wake binafsi.
- episode 18 nimevutiwa zaidi na ujasiri aliyouonyesha mwanadada Nam-Jong ambaye ni rafiki wa karibu sana wa Ae shin, na ndiye aliyeanza kumfanya awe na mzuka wa kusoma kiingilishi.licha ya kutokuwa na uwezo wa kupambana na wanajeshi wa kijapani lakini bado alionyesha ujasiri wa hali ya juu kwa kuendelea kumtetea mwalimu wake wa skuli. Nawaza hapa kama tukio lile linamtokezea aminas angelikimbia mpaka kwao. hahahahahaaaaaa unafanya masihara na bunduki.
ndio maana nimedhamiria kutokupenda mpaka nitakapotimiza miaka 80 ya kuzaliwa ndio nitafikiria kujaribu kupenda.
Naiwe ivyo baada ya Miaka Iyo!!!
Uku Mola Akikuongozee Uko.
Mi wala nisingekimbia Ningekomaa Nao Tuu kwani Nashukuru Sinaga Tabia Ya Kukimbia.