Kwa wapenzi wa Korean Dramas, hii ni thread yako!

Kwa wapenzi wa Korean Dramas, hii ni thread yako!

MR SUNSHINE DRAMA ep 17

  • ukiachana na kiongozi mkuu wowote wa nchi au wa taasisi binafsi, mwanadada go Ae sin ndiye anayeshikilia rekodi ya kuwa na ulinzi mkubwa sana kuliko mtu yoyote duniani. kwenye maisha yake amezungukwa na mashujaa zaidi ya 500 ila wanaojitokeza hadharani kumlinda kwa nyakati tofauti ni eugene choi, goo dong mae, kim huiseong, mwalim Jang Seung-Goo na wafuasi wengineo wa righteous army walioanza kumlinda tokea alipozaliwa na kumuepusha na shambulio la kifo. mhhhhhhhhhh bahati alionayo akiilalia mlango wazi nitamuibia. Nina wasiwasi huyu bidada huenda akawa anatumia ndumba kama za wale bongo celebrities uchwara.
“I chose to not kill because unlike our parents, we have the ability to choose.”
kupitia hii nukuu utagundua tofauti nyengine kubwa kati ya goo dong mae na choi eugene.
  • dong mae aliporudi korea jambo la kwanza alilolifanya kwenye ardhi ya korea ni kuwaua wale wote walisababisha mateso kwa familia yake huku upande wa pili eugne alipotoka marekani licha ya mateso na huzuni kubwa inayoendelea kumuandama kila siku kwa kuuawa wazazi wake wawili bado ameendelea kuzuia hasira dhidi ya maadui wa familia yake. Na ana uwezo wa kulipa kisasi tofauti na wazazi wao ambao hawakuwa na uhuru wa kuchagua jambo lolote kwa sababu ya utumwa wao. kumbe binadamu tunaweza kuepuka kutenda jambo lolote ovu, huwa nawashangaa sana wale wanaomsingizia shetani pindi wanapotenda uovu, Unamnajisi mtoto mdogo baadae unamsingizia shetani. goo dong mae alimjibu they have the ability to choose between a sword or a gun. Hahahahaaaaa dong mae ana maneno ya ovyo kuliko mvuvi.
  • nimeyapenda majibu ya eugene choi kwa mama yake kim hee sung, eugene alimwambia hawezi kumbebesha msalaba wa dhambi hui seong kwa sababu yeye hahusiki na dhambi ya familia yake ila bado ataendelea kutokumsamehe baba, mama na hata late grand father kwa matendo yao ya kinyama walioyatenda kwa familia yake. Tukirudi nyuma kwenye episode 1 babu yake kim hui seong yeye alikuwa na mtazamo tofauti, baada ya wazee wake eugene kutenda makosa babu aliamini familia nzima inapaswa ipokee adhabu ya kifo kwa kosa waliloloitenda. Yule harabuji hataiweza kuinusa harufu ya pepo kwa unyama aliyoutenda kwa kitendo chake cha kumbebesha dhambi mtoto mdogo asiyekuwa na hatia yoyote.
  • tanzania bado wapo wazalendo wa ukweli kama alivyo mzee go sa hong na joseon yake? nimependa msimamo wake mzee go sahong, yupo tofauti na noble family wengineo ambao wanajifanya hawana muda wa kufuatilia siasa za nchi yao, Ae sin amerithi kila kitu kutoka kwa babu yake ila cha ajabu babu hataki mjukuu wake afuate kivuli chake.Mzee go sa hong amepewa utajiri wa mali, uzalendo,upambanaji, hekima, huruma, busara, elimu. hivi kuna kitu ambacho mzee go sa hong amenyimwa? Kipo alichonyimwa na si chengine isipokuwa bado anaamini nchi inapaswa iwe na utabaka kati ya aliyenacho na asiyekuwa nacho, Ila nimeona picture preview zinazoonyesha mzee go sahong akiwaalika eugene choi na goo dong mae kwenye makaazi yake, unahisi atawaomba kitu wanadamu hao wawili?
utakapojifanya siasa ya nchi yako haikuhusu basi fahamu ya kwamba utakuwa ni miongoni mwa wajinga watakaosababisha nchi kuongozwa na watu ambao utakuwa umewazidi kimaarifa, Na maisha yote mpumbavu na mwedawazimu (chizi) ndiyo huzidiwa maarifa na mtu mjinga.
  • episode 18 nimevutiwa zaidi na ujasiri aliyouonyesha mwanadada Nam-Jong ambaye ni rafiki wa karibu sana wa Ae shin, na ndiye aliyeanza kumfanya awe na mzuka wa kusoma kiingilishi.licha ya kutokuwa na uwezo wa kupambana na wanajeshi wa kijapani lakini bado alionyesha ujasiri wa hali ya juu kwa kuendelea kumtetea mwalimu wake wa skuli. Nawaza hapa kama tukio lile linamtokezea aminas angelikimbia mpaka kwao. hahahahahaaaaaa unafanya masihara na bunduki.
sitaki kuzungumzia tukio la kuvunjika mahusiano kati ya ae sin na kim hee seong kwa sababu kuna mtu ameshalijibu tukio lile kwa kutolea mfano wake binafsi.
ndio maana nimedhamiria kutokupenda mpaka nitakapotimiza miaka 80 ya kuzaliwa ndio nitafikiria kujaribu kupenda.
sunshine-17-00055.jpg
Hahahahaha

Naiwe ivyo baada ya Miaka Iyo!!!
Uku Mola Akikuongozee Uko.

Mi wala nisingekimbia Ningekomaa Nao Tuu kwani Nashukuru Sinaga Tabia Ya Kukimbia.
 
MR SUSHINE DRAMA
wakati huu tunangojea subtitle ya episode ya 19 na next episode ya 20 hapo kesho ngoja tuondoe stress zinazotukabili kwenye maisha yetu ya kila siku, kuna wengine huondoa stress kwa kunywa pombe na akina sisi wengineo tunaondoa stress zetu za maisha kwa mapira na korean drama.
Na bahati mbaya wiki hii ulevi wangu mkuu wa manchester united haujaingia sokoni.

binadamu kumbe akili zetu zenye mihemuko ya kimwendo kasi tunazijuwa wenyewe, ngoja nijicheke mwenyewe kwanza kabla sijaandika sentensi niliyokusudia kuiandika.
hahahahaahhahahahaaaaaaaa​
kuna mashabiki wameanza kumlalamikia muandishi wa drama hii ambaye ni mwanamama kim eun sook pamoja na director Lee eung bok.
uvumilivu umeanza kuwashinda wafuatiliaji wa hii drama kwa sababu imeshafika episode ya 18 lakini hawajaona hata dalili ya kiss scene.
  • kuna wale wanaongojea kwa hamu kiss scene kati ya captain eugene choi (lee byung hun) na lady go ae sin (kim te ri), kundi hili la mashabiki ndio wapo wengi zaidi duniani na povu lao hata nguo za wafungwa wa gereza la keko au kiinua miguu lililopo zanzibar unaweza kufulia, bahati nzuri Kwenye kundi hili mimi sihusiki
  • kuna wale wanaongojea kwa hamu kiss scene kati ya mtemi aliyezaliwa na wazee wawili waliokuwa wakiuza butcher goo dong mae (yoo yeon seok) na mwanadada kudo hina (kim min jung) ambaye ameachika na mume wa kijapani na pia ndiye mtoto wa lee wan ik msaliti wa joseon, pia kwenye kundi hili mimi simo.wafuasi wa kundi hili wana hasira kali kuliko upanga wa Dong mae, unapaswa ukae nao mita 600.
  • kundi la tatu nipo peke yangu na sitaki mfuasi kwenye kundi hili,bado nasuburia kwa hamu kiss scene kati ya ahjumma Haman-daek na yule ahjussi ambaye pia ni mtumishi wa lady aesin na mzee go sa hong. Nitafurahi sana kama hawa wazee wawili watafunga ndoa na kuishi kwa amani na upendo na kuondokana na minyororo mizito ya utumwa,nasisitiza tena kwenye kundi hili sihitaji mfuasi.
aminas , talnam hivi nyinyi mupo team gani kwenye kiss scene?
hahahahahahhaaaaaaaa bangi za usiku ni mbaya sana zinaweza kukufanya ukayanunue makontena ya makonda.

huku kwetu serikali imebana, kule kwenye mpira manchester united wamebana na huku kwenye drama mwanamama kim eun sook ameendelea kubana.
huu mwaka kwa hali inavyokwenda sisi wengine tutakufa na tai shingoni.
2113770c-4938-4929-a3a3-080309976d9e.jpg
Mi Mwenyewe Natamni Iyo Namba 3 Itokea.

Uwezi Sema Mtu Asitamni Hiko Wakati Mi Nilishatamni Ilo.
 
MR SUNSHINE DRAMA ep 18
  • Takashi Mori uhusika wake nimeupenda sana na anaonekana ni mwanadamu aliye na chuki zisizopimika dhidi ya joseon, Lee wan ik na kelele zake zote alipokutana na takashi mori aliuficha mkia wake.Jahazi la joseon linaelekea kuzamishwa na wahuni wa japani.
  • Ms Haman na yeye hana siri kama mlevi aliyekunywa chupa 40 za soju, ametoa siri zote za ae sin kuhusiana na notebook yake kwa choi eugene. nimecheka sana
  • nisipomuona Kudo Hina moyo wangu huwa haufanyi kazi inayotakiwa, nampenda zaidi kudo hina uhusika wake kuliko ae sin, aigoooo macho yake unaweza kuombea mkopo benki kuu.
  • mfalme hakufanya maamuzi ya kijinga kwa kumfunga mzee go sa hong ambaye alikuwa ni mwalimu wake, mfalme anaamini kitendo cha kumweka ndani mzee kitazidi kuinua hamasa kwa wananchi wake wajitolee kupambana dhidi ya uvamizi wa wajapani kwenye nchi yao. na tayari tumeona wananchi wa joseon wameanza kukataa kutumia fedha ya japani kwenye nchi yao.lakini je itawezekana wakati japani nao wana mwandamu mwenye akili nyingi Takashi Mori?
  • je kim hui seong atakubali offer ya takashi mori? Takashi anataka gazeti la kim hui seong liandike habari zenye kuisifu japani ili kuiwachanganya raia wa joseon na waamini ya kwamba japani ni watu wazuri.
  • hizi tawala zote zilizopita za korea hazikumpa heshima inayostahili mwanamke, msichana hakuwa na ruhusa hata ya kupata elimu, ni shida
  • hivi kile kitendo cha dong mae kumkata nywele zake mwanadada ae sin kina maana gani?
ba9c4da56d330549ebf660f0c99dfd4de75d3168caf16886676b1e66ba24332f.gif
je inawezekana kitendo kile kinamaanisha ya kwamba ae sin anapaswa aachane rasmi na utambulisho wake kama ni mzaliwa wa familia ya kitajiri hivyo basi anapaswa kuishi kama wanaharakati wengine.
kwenye episode 1 tuliona choi eugene anakata nywele zake wakati yupo marekani na kitendo kile kina maaana ya kwamba amevunja mahusiano yake yote na joseon na ndio maana bado anaendelea kujitambulisha kama ni raia wa marekani.
sunshine-18-00196.jpg
 
Hahahahaha

Naiwe ivyo baada ya Miaka Iyo!!!
Uku Mola Akikuongozee Uko.

Mi wala nisingekimbia Ningekomaa Nao Tuu kwani Nashukuru Sinaga Tabia Ya Kukimbia.
  • ameeen ila kuna atakaenipenda pindi nitakapofikisha miaka 80.
  • kama wasichana munaogopa mende halafu usikimbie bunduki ilioshikiliwa na mwendawazimu wa kijapani. mimi binafsi ningelikimbia bila ya kuangalia nyuma kama kifaru.
748801113-peshawargun6_6.jpg
 
  • ameeen ila kuna atakaenipenda pindi nitakapofikisha miaka 80.
  • kama wasichana munaogopa mende halafu usikimbie bunduki ilioshikiliwa na mwendawazimu wa kijapani. mimi binafsi ningelikimbia bila ya kuangalia nyuma kama kifaru.
748801113-peshawargun6_6.jpg
Hmmmm!!!

Umeamua Kukubali!

Utapendwa tuuh Mbona Miaka Bado
 
Unaona Unavyojichanganyaaa!

Nilijua Niwewe Tuuh Muonee
  1. muandiko wangu haujabadilika
  2. na siku ya kwanza nilikuambia ndio nini kukimbilia kituo cha polisi
  3. nikakwambia ID ya damushin ndio imechukua likizo ila mwenye id bado yupo
mimi mwenyewe nilifikiri unanienjoy kumbe upo serious?
hahahahahahahaaaaaaaaaaa
 
  1. muandiko wangu haujabadilika
  2. na siku ya kwanza nilikuambia ndio nini kukimbilia kituo cha polisi
  3. nikakwambia ID ya damushin ndio imechukua likizo ila mwenye id bado yupo
mimi mwenyewe nilifikiri unanienjoy kumbe upo serious?
hahahahahahahaaaaaaaaaaa

Aku Sikuwa Serious Mie.

Nilikuwa Nakuzingua tuu
 
Mipaka Kivipi!???
  • nilitengeneza ID hii september 1 na utakuwa unafahamu nilichodhamiria kukifanya ndani ya mwezi huu hakuna ulazima wa kurejea.
  • ukiachana na thread hii pia nilikuwa na access kwenye sports forum pekee kwa kutumia ID ya damushin.
  • nimeamua kutengeneza ID hii ili niitumie kwa kutembelea majukwaa yote ya JF. pia hata kama itatokezea nimekutana na mtu mwenye tabia za ovyo itanibidi nitumie nafsi yangu ya pili kukabiliana naye.humu jf baadhi ya wakati unaweza kukutana na watu wenye tabia tofauti zisizoridhisha ambazo kama utaendelea kuzivumilia kila siku zitakuletea athari kubwa sana. kwa kutumia id ile nimeshakutana na matukio mengi yasio furahisha lakini nimekuwa nikiyavumilia ila kwa id hii itakuwa ni tofauti.
hahahahahaaaaaa wanasema uvumilivu una kikomo.
 
  • nilitengeneza ID hii september 1 na utakuwa unafahamu nilichodhamiria kukifanya ndani ya mwezi huu hakuna ulazima wa kurejea.
  • ukiachana na thread hii pia nilikuwa na access kwenye sports forum pekee kwa kutumia ID ya damushin.
  • nimeamua kutengeneza ID hii ili niitumie kwa kutembelea majukwaa yote ya JF. pia hata kama itatokezea nimekutana na mtu mwenye tabia za ovyo itanibidi nitumie nafsi yangu ya pili kukabiliana naye.humu jf baadhi ya wakati unaweza kukutana na watu wenye tabia tofauti zisizoridhisha ambazo kama utaendelea kuzivumilia kila siku zitakuletea athari kubwa sana. kwa kutumia id ile nimeshakutana na matukio mengi yasio furahisha lakini nimekuwa nikiyavumilia ila kwa id hii itakuwa ni tofauti.
hahahahahaaaaaa wanasema uvumilivu una kikomo.
Anhaa!!! Hongera

Si mbaya Japo Ilinishtua.
 
Nini epispde 10,huwa natenga siku maalumu navuta episode hata 50 kwa mkupuo mmoja
unaweza kushusha episode 10 kwa siku moja?
going on drama zimeshaanza kuniletea athari kiasi ambacho najihisi kutokuvutiwa na drama za kizamani labda iwe nzuri mnoo.
 
Aloangalia Episode ya 19 naomba njoo tulie wote (Mr Sunshine)

Hii episode imenitoa Chozi Walah.

Hii Episode imeniumiza Tena.

Userious Wa Waigizaji Episode Hii Ni Wakuumiza! Nimelia Nao Yaani
 
Kuna Binadam Wanaroho Kama Ya Huyu Mzee (Lee Wan Ik) Yaani Unaenda Iumiza Famila ya Mtu Sababu Tuu We Ufanikiwe Kweli,

Uhisi Hata Maumivu Yao Najua Haya Ni Maigizo Lakini Kuna Maisha Ya Watu Waliishi Ivyi na Waliyapitia Haya Na Wapo Mpka Leo Wanaishi Ivyi.

Na Serikali Inashindwa Hata kutetea Watu Wake Lol!!!
 
Back
Top Bottom