hahahahahahaaaaaaaaaa 0.00000000001%Na kwa Tanzania ni asilimia moja tu imetizama episode ya kwanza ambayo ni mimi tu [emoji23][emoji23][emoji23]. Leo nashusha episode ya pili. Bonge la drama ile sehemu hukumu inapitishwa unaweza mwaga machozi. Mwanzo wa episode wazazi wote wawili wanaonyesha upendo wa dhati kwa mtoto wao.
Nzuri sanaghost detective nimeangalia episode 2 za mwanzo ipo vizuri.
hahahahahahaaaaaaaaaa 0.00000000001%
Mieeeeeee Nimeionaaaaa! Nimetoka kuangaliaa Mudaaa huuu“100 Days My Prince”kuna aliyebahatika kuiangalia hii drama iliyoanza wiki hii kupitia kituo cha TvN?
View attachment 865546
inazungumzia maisha ya crown prince Lee Yool ambaye amepatwa na ugonjwa wa kupoteza kumbukumbu baada ya kushambuliwa na watu wasiojulikana na hatimaye kushindwa kurudi mji mkuu kwa siku 100 jambo lililopelekea kufunga ndoa na mwanamke mwengine akiwa mafichoni.
- kabla ya hapo alikuwa tayari ameshafunga ndoa na mtoto wa left councillor ambaye ni kama waziri mkuu ila kama kawaida ya ndoa za kisiasa hakuvutiwa na mke wake, kibaya zaidi mke wake alibeba ujauzito na cha kushangaza hajawahi kulala na mume wake hata sekunde moja. humu ndani kwa episode mbili za mwanzo zimejikita zaidi kwenye vita ya kisiasa kati ya pande tatu kuu zinazokinzana.
- malikia ana mtoto wake hivyo basi anataka arithi nafasi ya crown prince lee yool anaamua kufanya kila namna amsambaratishe bwana mdogo ambaye ni mtoto wake wa kambo (step mother)
- mfalme aliingia madarakani kwa njia ya mapinduzi baada ya kumpindua kaka yake, na muongozaji mkuu wa mapinduzi baada ya kufanikisha azma yake alimuomba mfalme aruhusu ndoa kati ya mtoto wake wa kike na crown prince. Hivyo basi nguvu kubwa ya kiuongozi ipo chini ya huyu left councillor Kim Cha-Eon.
- kwa watazamaji wa bongo movies naomba wanisaidie kunitajia waigizaji bora wenye umri chini ya miaka 15 tafadhali, dakika 40 za episode ya mwanzo zilikuwa za kuvutia sana, hawa watoto wawili ambao ni jung ji hoon na heo jung eun uigizaji wao umenifurahisha zaidi ya kuangalia uigizaji wa ray na wema sepetu.Nimevutiwa zaidi na uhusiano wao wa kimapenzi ulivyoanza kuchipua tokea wakiwa wadogo ila ndio hivyo tena siasa ikatenganisha uhusiano wao, sijui kitatokezea kitu gani siku ambayo mwanadada Hong-Sim atakapogundua ya kwamba aliyeongoza kampeni ya mauaji ya wazazi wake ni mfalme ambaye ndiye baba wa crown prince lee yool. Nisiandike sana nikawachosha ila kwa anayehitaji kuangalia historical drama basi hii ipo vizuri na love story yake itakuwa onfire.
View attachment 865579
cherry blossom tree nitakapokutana na bibi yenu miaka 5 ijayo
EXO D.O na mwanadada Nam Ji Hyun ndio waigizaji wakuu wa hii drama.
hivi hawa wakorea kwa nini wanapenda kutuwaminisha ya kwamba ni rahisi sana kumtongoza mwenza wako.
ukiziangalia mara kwa mara hizi drama zinazozungumzia tawala ya joseon utagundua ya kwamba love story kati ya wawili kwa kiasi kikubwa huchangiwa na mti wa cherry blossom.
yaani binti ukimpeleka sehemu yenye miti hii hujisikia furaha sana kama mcheza kamari anaposhinda kitita kikubwa na itokezee vipande vya barafu na maua (snow flower) viwe vinaanguka kwa wakati mmoja
daebak siku hiyo hiyo atakuwa mchumba wako.
pumbavu zao wakorea kwa kuzidi kunitia ujinga na umri huu nilionao wa miaka 75.
View attachment 865553
- Watch 100 Days My Prince Episode 1 online at Dramanice
- Watch 100 Days My Prince Episode 2 online at Dramanice
ost 1 ameimba mwanadada gummy na unaitwa erase.
team korean family drama fans
ingizo jipya (15/08/2018)
My Only OneKim Do-Ran ni msichana mwenye tabia njema, mcheshi, anajituma licha ya kuwa anakabiliwa na tatizo la ukosefu wa fedha. Ndoto yake kubwa ni kumaliza elimu yake ya chuo kikuu ili awe mtumishi wa umma. Baada ya miaka 28 siku moja anafanikiwa kuiona sura ya baba yake ambaye walipoteana na ndipo baba yake anamuelezea sababu iliyomfanya afiche uhusika wake kwa miaka 28.
pia baba yake kwa mujibu wa episode mbili za mwanzo amehukumiwa kifungo cha maisha kwa kosa la mauaji na kumtelekeza mtoto wake
ina maana wakorea ni wapenzi wakubwa sana wa family drama.
- kwa mujibu wa Nielsen korea episode ya kwanza iliangaliwa na 21.2% ya watu wanaoishi korea kwa siku ya jana.
- episode ya pili iliangaliwa na 24.3% ya watu wanaoishi korea kwa siku ya jana.
starring
choi soo jong ahjussi = (emperor wang guhn, emperor of the sea, dae jo young, comrade drama)
uee noona = (my husband oh jak doo, manhole, marriage contract, white night drama)
Lee Jang-Woo hyungnim = rosy lovers drama na pia itakuwa ni drama yake ya kwanza baada ya kutoka jeshini.
View attachment 867935
Hahahahanakwambia hili gonjwa la korean drama limeshatuathiri kiasi ambacho hata tukibadilishwa damu bado vimelea havitaweza kuondoka.
hii comment yako imenifanya nikumbuke siku yangu ya mwanzo kufahamu sanaa za korea nakujiuliza maswali.
dalili zifuatazo ukiwa nazo basi juwa umeshaathiriwa na korean drama
naomba tusaidiane njia ya kuachana na huu ugonjwa usio na madhara mwilini mwetu jamani.
- kutumia muda mwingi kwa ajili ya kutembelea tovuti maalum zenye mijadala ya korean entertainment.(hahahahahahaaaa hii inanihusu)
- kuchukia pale ambapo tovuti unayoitembelea haijaweka subtitle ya drama unayoifuatlia (hahahahahahaaaa hii pia inanihusu)
- kuanza kujifunza lugha ya kikorea (inanihusu)
- kuwafahamu 20% ya korean celebrities (hii inanihusu)
- kusubiria notification za wachangiaji wa thread hii
unajua korean drama hazichosi simulizi zake ndio maana inakuwa ni ngumu sana kuachana nazo.
View attachment 868342
Wanawatengeneza kwa Mbali Sana! Wanawafanya Wanakuwa Huru na Camera Na Zile Light na Hata Shouts Za Madirector! Wanawatengeneza Kujiamini Ndomana Wanawachukua Wakiwa Wadogo Ili Kuwafanya Wawe Best Stars.licha ya vitimbi vyao vinavyofanyika nyuma ya pazia ila wakorea wanathamini vipaji vyao.
Nam ji hyun ametoka mbali sana mpaka leo hii anasimama kama lead actress.
ni funzo kubwa sana tunalipata.
ngoja nimtakie kheri ya kuzaliwa na mapemaaa kabla wajanja hawaja wahi siti ya mbele
- princess deokman (teen)
- lobbyst drama (maria teen)
- king sejong drama = Queen So-Yeon (young)
Birthdate: September 17, 1995
fugitive plan b niliipenda ni bonge la dramaLee Na Young And Lee Jong Suk In Talks For Upcoming tvN Drama
kwa mujibu wa Eden9 ambao wanamsimamia mwanadada lee na young wamethibitisha ya kwamba mteja wao amepata offer ya kushiriki kwenye drama inayoitwa ‘Romance Supplement.'” ila hakuna maamuzi yoyote yaliofikiwa.
kama mwanadada huyo atakubali kushiriki kwenye drama hiyo itakuwa ni mara yake ya kwanza baada ya kupita miaka 8 tokea aliposhiriki kwenye fugitive plan B drama.
upande wa lee jong suk naye pia hajathibitisha rasmi ushiriki wake kwenye drama hiyo, kama atashiriki kwenye drama hiyo huenda ikawa ni project yake ya mwisho kabla hajatumikia jeshi.
“Romance Supplement” inategemewa kuonyeshwa 2019.
View attachment 865522
BogoshipoYoo In Na And Lee Dong Wook In Talks To Reunite For New tvN Drama
“Goblin” co-stars wamepata nafasi ya kushiriki pamoja kwenye drama inayoitwa “Touch Your Heart” itakayoonyeshwa na kituo cha TnN lakini mpaka sasa hakuna upande wowote uliothibitisha kukubali ofa ya kushirika kwenye drama hiyo.
Yoo In Na ataigiza uhusika wa top actress ambaye anajikuta akiwa kwenye scandal baada ya kujulikana ana mahusiano na mjukuu wa tajiri mkubwa sana na lee dong wook ataigiza nafasi ya mwanasheria.
drama hiyo itaonyeshwa mapema mwezi january 2019director Park Joon Hwa ndiye atakayeisimamia project hiyo na hapo nyuma amesimamia project mbili ziilizofanya vizuri sana.
hii couples TvN watafanya kila njia wailete pamoja.
- because this is my first life drama
- whats wrong with secretary kim drama
View attachment 871306
Bogoshipo
Na Una Nini Siku Hizi? Kila Ukiandika Unafuta? Shida Nini??
Hmmmm!!!episode mbili za mwisho za drama ya mr sunshine hazitaonyeshwa week end hii kwa sababu ya sherehe za chuseok nchini korea.
Pole Sanahappy chuseok (Korean Thanksgiving on 9/23-9/25) mpendwa.
huku kwetu kuna msiba wa taifa.
swadakta ahjumma 💑👍🏻mtarajiwa baada ya miaka 40Hmmmm!!!
Hichi Unachosema Ni Kweli Ama??