Kwa wapenzi wa Korean Dramas, hii ni thread yako!

Kwa wapenzi wa Korean Dramas, hii ni thread yako!

Na kwa Tanzania ni asilimia moja tu imetizama episode ya kwanza ambayo ni mimi tu [emoji23][emoji23][emoji23]. Leo nashusha episode ya pili. Bonge la drama ile sehemu hukumu inapitishwa unaweza mwaga machozi. Mwanzo wa episode wazazi wote wawili wanaonyesha upendo wa dhati kwa mtoto wao.
hahahahahahaaaaaaaaaa 0.00000000001%
 
MR SUNSHINE EP 21
mwanamke ni kama majani ya chai huwezi kujua nguvu yake mpaka uyachanganye kwenye maji ya moto.
1537096134510.png
daebak daebak
heshima kwenu agassi, noona, ahjumma, halmeoni, gyemo kwa hizi mbio munazo tuendesha sisi wa jinsia ya pili.

Ae Shin ni mwanamke mkatili sana, kwa kuwa anafahamu fika eugene choi anampenda kuliko anavyoupenda mwili wake basi anamwendesha kama amemroga kwa babu wa Tanga, eugene amekuwa hana tofauti na wanaume wa Dar.
ila nimeyapenda sana majibu ya captain choi kwa mwanadada Aeshin baada ya kumwambia nipo tayari twende pamoja marekani.
angalau si ungeliniambia unanipenda na upo tayari kuwa na mimi kimahusiano, laiti kama ningeliyasikia maneno hayo matamu japokuwa ni ya uwongo kutoka kwenye kinywa chako yangelinifanya nizidi kuwa tayari kufanya lolote kwa ajili yako.
poor captain eugene choi mapenzi yamekutia ujinga mwanamme wewe mpaka maziwa unasema ni tui la nazi.

Takashi mori na yeye ana mikwala mingi kuliko bata mzinga lakini mwisho wa siku anageuziwa kibao yeye.
takeshi mori: tutakapokutana kwa mara nyengine tena sijui utakuwa upande gani kati ya korea au marekani
eugene choi : ni kazi kwako kufikiri, ila mimi nimeshafanya maamuzi ya lipi la kufanya tutakapokutana tena (akimaanisha atamuua).

muandishi kim eun sook ametumia ubunifu mzuri sana kwenye hili tukio la kuuawa Takeshi mori bila ya kuharibu uhalisia wa tukio hili kwa asilimia 90.Takeshi mori aliuliwa na mjapani mwenzake ambaye ni Major kenji Hatanaka mnamo mwaka 1945 baada ya japani kujisalimisha na kuacha kupambana kwenye vita ya pili ya dunia, ina maana takeshi mori alifariki mwaka ambao korea walifanikiwa kupata uhuru wao kutoka kwa wajapani.

Aeshin : bado upo hapa kwanini hujaondoka
eugene : meli imenikimbia na nimeona wajapani wenye mapanga wana kufuatilia ndio nimekuja kwako.

daebak mimi ni captain eugene choi najisalimisha kwenu nipo na mke wanguuuuuuuu.
pumbaavuuuuuuuu kwa sauti ya vincent kigosi (ray)


1537097847967.png
 

Attachments

  • 1537096656618.png
    1537096656618.png
    144.3 KB · Views: 44
“100 Days My Prince”
View attachment 865546
kuna aliyebahatika kuiangalia hii drama iliyoanza wiki hii kupitia kituo cha TvN?
inazungumzia maisha ya crown prince Lee Yool ambaye amepatwa na ugonjwa wa kupoteza kumbukumbu baada ya kushambuliwa na watu wasiojulikana na hatimaye kushindwa kurudi mji mkuu kwa siku 100 jambo lililopelekea kufunga ndoa na mwanamke mwengine akiwa mafichoni.
  1. kabla ya hapo alikuwa tayari ameshafunga ndoa na mtoto wa left councillor ambaye ni kama waziri mkuu ila kama kawaida ya ndoa za kisiasa hakuvutiwa na mke wake, kibaya zaidi mke wake alibeba ujauzito na cha kushangaza hajawahi kulala na mume wake hata sekunde moja. humu ndani kwa episode mbili za mwanzo zimejikita zaidi kwenye vita ya kisiasa kati ya pande tatu kuu zinazokinzana.

  • malikia ana mtoto wake hivyo basi anataka arithi nafasi ya crown prince lee yool anaamua kufanya kila namna amsambaratishe bwana mdogo ambaye ni mtoto wake wa kambo (step mother)
  • mfalme aliingia madarakani kwa njia ya mapinduzi baada ya kumpindua kaka yake, na muongozaji mkuu wa mapinduzi baada ya kufanikisha azma yake alimuomba mfalme aruhusu ndoa kati ya mtoto wake wa kike na crown prince. Hivyo basi nguvu kubwa ya kiuongozi ipo chini ya huyu left councillor Kim Cha-Eon.

  1. kwa watazamaji wa bongo movies naomba wanisaidie kunitajia waigizaji bora wenye umri chini ya miaka 15 tafadhali, dakika 40 za episode ya mwanzo zilikuwa za kuvutia sana, hawa watoto wawili ambao ni jung ji hoon na heo jung eun uigizaji wao umenifurahisha zaidi ya kuangalia uigizaji wa ray na wema sepetu.Nimevutiwa zaidi na uhusiano wao wa kimapenzi ulivyoanza kuchipua tokea wakiwa wadogo ila ndio hivyo tena siasa ikatenganisha uhusiano wao, sijui kitatokezea kitu gani siku ambayo mwanadada Hong-Sim atakapogundua ya kwamba aliyeongoza kampeni ya mauaji ya wazazi wake ni mfalme ambaye ndiye baba wa crown prince lee yool. Nisiandike sana nikawachosha ila kwa anayehitaji kuangalia historical drama basi hii ipo vizuri na love story yake itakuwa onfire.

View attachment 865579
cherry blossom tree nitakapokutana na bibi yenu miaka 5 ijayo
EXO D.O
na mwanadada Nam Ji Hyun ndio waigizaji wakuu wa hii drama.
hivi hawa wakorea kwa nini wanapenda kutuwaminisha ya kwamba ni rahisi sana kumtongoza mwenza wako.
ukiziangalia mara kwa mara hizi drama zinazozungumzia tawala ya joseon utagundua ya kwamba love story kati ya wawili kwa kiasi kikubwa huchangiwa na mti wa cherry blossom.
yaani binti ukimpeleka sehemu yenye miti hii hujisikia furaha sana kama mcheza kamari anaposhinda kitita kikubwa na itokezee vipande vya barafu na maua (snow flower) viwe vinaanguka kwa wakati mmoja
daebak siku hiyo hiyo atakuwa mchumba wako.
pumbavu zao wakorea kwa kuzidi kunitia ujinga na umri huu nilionao wa miaka 75.
View attachment 865553

ost 1 ameimba mwanadada gummy na unaitwa erase.

Mieeeeeee Nimeionaaaaa! Nimetoka kuangaliaa Mudaaa huuu

TvN Ni Cheche hii Drama Ni Moto

Izi episode za Mwanzo ni Nzurii Sana

Damushin kuacha Kuangalia Korean drama Sidhaniii, Sidhani kwa Mambo haya
 
Woooiii naiweka pending october mwishoni itanifaa hii
team korean family drama fans
ingizo jipya (15/08/2018)
My Only One
Kim Do-Ran ni msichana mwenye tabia njema, mcheshi, anajituma licha ya kuwa anakabiliwa na tatizo la ukosefu wa fedha. Ndoto yake kubwa ni kumaliza elimu yake ya chuo kikuu ili awe mtumishi wa umma. Baada ya miaka 28 siku moja anafanikiwa kuiona sura ya baba yake ambaye walipoteana na ndipo baba yake anamuelezea sababu iliyomfanya afiche uhusika wake kwa miaka 28.
pia baba yake kwa mujibu wa episode mbili za mwanzo amehukumiwa kifungo cha maisha kwa kosa la mauaji na kumtelekeza mtoto wake
  • kwa mujibu wa Nielsen korea episode ya kwanza iliangaliwa na 21.2% ya watu wanaoishi korea kwa siku ya jana.
  • episode ya pili iliangaliwa na 24.3% ya watu wanaoishi korea kwa siku ya jana.
ina maana wakorea ni wapenzi wakubwa sana wa family drama.
starring

choi soo jong ahjussi = (emperor wang guhn, emperor of the sea, dae jo young, comrade drama)
uee noona = (my husband oh jak doo, manhole, marriage contract, white night drama)
Lee Jang-Woo hyungnim = rosy lovers drama na pia itakuwa ni drama yake ya kwanza baada ya kutoka jeshini.
View attachment 867935
 
nakwambia hili gonjwa la korean drama limeshatuathiri kiasi ambacho hata tukibadilishwa damu bado vimelea havitaweza kuondoka.
hii comment yako imenifanya nikumbuke siku yangu ya mwanzo kufahamu sanaa za korea nakujiuliza maswali.
dalili zifuatazo ukiwa nazo basi juwa umeshaathiriwa na korean drama

  1. kutumia muda mwingi kwa ajili ya kutembelea tovuti maalum zenye mijadala ya korean entertainment.(hahahahahahaaaa hii inanihusu)
  2. kuchukia pale ambapo tovuti unayoitembelea haijaweka subtitle ya drama unayoifuatlia (hahahahahahaaaa hii pia inanihusu)
  3. kuanza kujifunza lugha ya kikorea (inanihusu)
  4. kuwafahamu 20% ya korean celebrities (hii inanihusu)
  5. kusubiria notification za wachangiaji wa thread hii
naomba tusaidiane njia ya kuachana na huu ugonjwa usio na madhara mwilini mwetu jamani.
unajua korean drama hazichosi simulizi zake ndio maana inakuwa ni ngumu sana kuachana nazo.
View attachment 868342
Hahahaha

Nimempenda Nam Hyun Umu. Yupo Comfortable Kabisaa Anaigiza Kwa Kurelax Wachache Watanielewa.
 
licha ya vitimbi vyao vinavyofanyika nyuma ya pazia ila wakorea wanathamini vipaji vyao.
Nam ji hyun ametoka mbali sana mpaka leo hii anasimama kama lead actress.
ni funzo kubwa sana tunalipata.
  • princess deokman (teen)
  • lobbyst drama (maria teen)
  • king sejong drama = Queen So-Yeon (young)
ngoja nimtakie kheri ya kuzaliwa na mapemaaa kabla wajanja hawaja wahi siti ya mbele
Birthdate: September 17, 1995​
Wanawatengeneza kwa Mbali Sana! Wanawafanya Wanakuwa Huru na Camera Na Zile Light na Hata Shouts Za Madirector! Wanawatengeneza Kujiamini Ndomana Wanawachukua Wakiwa Wadogo Ili Kuwafanya Wawe Best Stars.

Mwisho wa Siku Tunawaona Wakiigiza Uku Wakichukua Hisia Zako!

Na Hii Ndo Kazi Ya Kuinvest, Weka Ela Upate Thamani Ya Ela Uloiweka Hata Ukipata Hasara Isiwe Ya Mara Zote.
 
First Impressions: “100 Days My Prince” Provides Plenty Of Charm, Intrigue, And Talented Actors

1537163846453.png


Nasubili Tonight Episode Nicheke Maana Naona Itakuwa Na Vitukoo
 
Lee Na Young And Lee Jong Suk In Talks For Upcoming tvN Drama

kwa mujibu wa Eden9 ambao wanamsimamia mwanadada lee na young wamethibitisha ya kwamba mteja wao amepata offer ya kushiriki kwenye drama inayoitwa ‘Romance Supplement.'” ila hakuna maamuzi yoyote yaliofikiwa.
kama mwanadada huyo atakubali kushiriki kwenye drama hiyo itakuwa ni mara yake ya kwanza baada ya kupita miaka 8 tokea aliposhiriki kwenye fugitive plan B drama.
upande wa lee jong suk naye pia hajathibitisha rasmi ushiriki wake kwenye drama hiyo, kama atashiriki kwenye drama hiyo huenda ikawa ni project yake ya mwisho kabla hajatumikia jeshi.
“Romance Supplement” inategemewa kuonyeshwa 2019.
View attachment 865522
fugitive plan b niliipenda ni bonge la drama
 
Yoo In Na And Lee Dong Wook In Talks To Reunite For New tvN Drama
“Goblin” co-stars wamepata nafasi ya kushiriki pamoja kwenye drama inayoitwa “Touch Your Heart” itakayoonyeshwa na kituo cha TnN lakini mpaka sasa hakuna upande wowote uliothibitisha kukubali ofa ya kushirika kwenye drama hiyo.

Yoo In Na ataigiza uhusika wa top actress ambaye anajikuta akiwa kwenye scandal baada ya kujulikana ana mahusiano na mjukuu wa tajiri mkubwa sana na lee dong wook ataigiza nafasi ya mwanasheria.
drama hiyo itaonyeshwa mapema mwezi january 2019​
director Park Joon Hwa ndiye atakayeisimamia project hiyo na hapo nyuma amesimamia project mbili ziilizofanya vizuri sana.
  • because this is my first life drama
  • whats wrong with secretary kim drama
hii couples TvN watafanya kila njia wailete pamoja.
1537366759687.png
 
Yoo In Na And Lee Dong Wook In Talks To Reunite For New tvN Drama
“Goblin” co-stars wamepata nafasi ya kushiriki pamoja kwenye drama inayoitwa “Touch Your Heart” itakayoonyeshwa na kituo cha TnN lakini mpaka sasa hakuna upande wowote uliothibitisha kukubali ofa ya kushirika kwenye drama hiyo.

Yoo In Na ataigiza uhusika wa top actress ambaye anajikuta akiwa kwenye scandal baada ya kujulikana ana mahusiano na mjukuu wa tajiri mkubwa sana na lee dong wook ataigiza nafasi ya mwanasheria.
drama hiyo itaonyeshwa mapema mwezi january 2019​
director Park Joon Hwa ndiye atakayeisimamia project hiyo na hapo nyuma amesimamia project mbili ziilizofanya vizuri sana.
  • because this is my first life drama
  • whats wrong with secretary kim drama
hii couples TvN watafanya kila njia wailete pamoja.
View attachment 871306
Bogoshipo

Na Una Nini Siku Hizi? Kila Ukiandika Unafuta? Shida Nini??
 
episode mbili za mwisho za drama ya mr sunshine hazitaonyeshwa week end hii kwa sababu ya sherehe za chuseok nchini korea.
1537536763543.png
 
Hmmmm!!!

Hichi Unachosema Ni Kweli Ama??
swadakta ahjumma 💑👍🏻mtarajiwa baada ya miaka 40

The final two episodes, ep.23 & 24, will air one week later than originally planned. A special Korean Thanksgiving Day director's version "Mr. Sunshine Gun, Glory, Sad Ending" will air on Saturday, September 22, 2018 and entertainment program "Great Escape" will air on Sunday, September 23, 2018. Ep.23 will now air on Saturday, September 29, 2018 and ep.24 will air on Sunday, September 30, 2018.
 
Back
Top Bottom