Kwa wapenzi wa Korean Dramas, hii ni thread yako!

Hao madijay wa Arusha wameibadili jina tanthilia ya "DONG YI", sasa wanaiita "FRATENITY" kiukweli wanaweza kupoteza kabisaa
 
Hao madijay wa Arusha wameibadili jina tanthilia ya "DONG YI", sasa wanaiita "FRATENITY" kiukweli wanaweza kupoteza kabisaa
Wanazingua sana
Gye baek wameiita the black ninja
Are you human wameiita mr robot
Jang ok jung-sword of the prince
Princess man-wanted
Halafu tabia yao ya kuigawa episode mara nne ni upuuzi
 
Nilikuwa natamani sana kama King Gwanggaeto the
Wanazingua sana
Gye baek wameiita the black ninja
Are you human wameiita mr robot
Jang ok jung-sword of the prince
Princess man-wanted
Halafu tabia yao ya kuigawa episode mara nne ni upuuzi
Gybaek miye niliitazama ikiwa imetiwa maneno na Dj Black( dj Mark) ilikuwa tamu sana. Tabia ya madijay wa arusha kukata tamthilia kwenye vipande vidogo inaboa kweli
 


Ni Scene Kwenye Smile Has Left Your Eyes (Drama) Kwa Ambaye Anataka Kuaangalia Drama Isonamambo Mengi Karibu Kwenye Hii(Kinachotawala Umu Zaidi Ni Mahusiano) na Inazile Huzuni Huzuni Kama Mpenzi Wa Izi Karibu Tusmile Pamoja.
 
Niko na bad papa na 100 days my prince nahitaji nyongeza any suggestion?
  1. Where Stars Land at Dramanice
  2. Where Stars Land – QuickDrama – Watch Full Episodes Free HD on QuickDrama
where stars land (fox bride star) drama
kwa drama zinazoonyeshwa jumatatu na jumanne hii ndio drama yangu ya kwanza ninayoipa kipaumbele ikifuatiwa na the beauty inside, bad papa na 100 days my prince ambayo imemalizika wiki hii, nakuhakikishia hutajutia Mb zako kama utakapoanza kuifuatilia.

izo nyota zinazotuwa ardhini zilizokusudiwa hapo ni usafiri wa ndege ambao umekuwa ni miongoni mwa chanzo kikuu cha usafiiri kwa binadamu wa rika zote.
ni drama inayojaribu kuzungumzia maisha ya kila siku ya wafanyakazi wa Incheon International Airport ambao ndio uwanja mkubwa na kisasa nchini korea.Ningependa zaidi kuona wahusika wakuu wa usafiri wa ndege nchini kwetu wangelipata muda wa kuangalia jinsi gani wenzetu walivyo makini na wenye kufuata maadili ya kazi kwenye shughuli zao za kila siku.

Kinachovutia biashara ya ndege si kuwa na ndege kubwa, uwanja mkubwa, kuwa na wafanya kazi warembo bali ni kuwa na taasisi itakayoweza kutoa huduma za kisasa na za uhakika kwa wateja ikiwemo usalama wa abiria bila ya kuangalia heshima aliyonayo mteja kwenye jamii awe masikini au tajiriwatanzania tuna la kujifunza humu ndani

bila ya kusahau love story kati ya lee ji hoon na trouble maker chae soo bin ni ya kiwango cha Phd.
 
Niko na bad papa na 100 days my prince nahitaji nyongeza any suggestion?
ROOM NO 9
nathubutu kusema kupitia drama hii wanawake mumepewa heshima nyengine kubwa sana na muandishi wa hadithi hii kwa sababu waigizaji wakuu wote wa drama hii ni wanawake.
inazungumzia maisha ya mwanadada Eulji Hae-Yi ambaye ni mwanasheria na maisha ya mwanamama Jang Hwa-Sa ambaye amehukumiwa kifungo cha maisha gerezani kwa kusingiziwa kuhusika na mauaji ya Ki san
hadithi iko hivi​
miaka 34 iliopita huyu jang hwa sa kipindi hicho ni msichana mrembo alijikuta akiwa kwenye mahusiano na kijana mmoja aliyeitwa choi yun baek ambaye alitokea kwenye familia ya kitajiri lakini kijana huyo alizaliwa na hawara hivyo basi baba yake hakuona umuhimu mkubwa sana kuwa mrithi wa makampuni yake mbele ya mtoto wake halali wa ndoa ambaye aliitwa Ki San.
hali hiyo haikumfurahisha choi yun baek hivyo basi siku moja akamshawishi jang hwa sa wafanya mpango wa kuiba fedha za mzee ili baadae wakimbie na wakaanzishe maisha yao kama wanandoa.

kwenye ishu hiyo choi yun baek akagundulikana na kaka yake ambaye ni ki san hivyo basi jamaa akachukua hatua ya kumuua kaka yake baadae mwili wa kaka yake akauhifadhi kwenye gari aliokuwemo jang hwa sa.
kufariki kwa ki san ikawa nafasi kwa choi yun baek kurithi makampuni ya baba yake hivyo basi akaamua kuwahonga wachunguzi wa kifo cha kisan wakiwemo polisi, prosecutor, madaktari wamtengenezee kesi ya mauaji mpenzi wake ambaye ndiye alikuwa akifahamu mpango mzima wa mauaji na hatimaye choi yun baek akaamua kujibadilisha jina kujiita Ki San.

miaka 34 baadae akiwa gerezani akitumikia hukumu yake ya kifo jang hwa sa alitembelewa na jopo la wanasheria wakiongozwa na mwanadada Eulji Hae-Yi ambao walikuwa wanajadiliana ni jinsi gani wataweza kumsaidia ili apunguziwe adhabu yake.
siku moja nyakati za jioni kuna tukio moja la ajabu lilolotokana na shoti ya umeme iliosababishwa na defbrillator machine ambalo lilisababisha wawili hao mfumo wao wa maisha ubadilike ghafla ambapo Eulji Hae-Yi na jang hwa sa nafsi zao zilibadilika ila physical body ikawa ni vile vile.

nafsi ya mwanasheria Eulji Hae-Yi ikahamia kwenye mwili wa jang hwa sa aliyehukumiwa kifungo cha maisha na nafsi ya jang hwa sa ikahamia kwenye mwili wa Eulji Hae-Yi ambaye ni mwanasheria wa makampuni ya Ki san.
siku moja kabla tukio hilo halijatokezea mfungwa jang hwa sa alishangaa baada ya kuona taarifa yenye kumuonyesha CEO ki san akiendelea na majukumu yake ya kikazi wakati amehukumiwa kifungo cha maisha kwa kumuua ki san.
Ndipo akagundua ya kwamba kumbe choi yun baek ameamua kumtengenezea kesi ili apate kutumia uhusika wa ki san.
Kwa kutumia mwili wa Eulji Hae-Yi mwanamama jang hwa sa anataka kufichua uovu aliotendewa na choi yun baek ambaye kwa sasa anajiita ki san.
 
Anyeong Sunbaenim
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…