Kwa wapenzi wa Korean Dramas, hii ni thread yako!

Kwa wapenzi wa Korean Dramas, hii ni thread yako!

Nifah noona anakusabahi, umenikwaza sana hukuwa umeiona Dong Yi mpaka sasa, naipenda mnooo nilishairudia mara kadhaa huwa siichoki kabisa. Enjoy hun, love from this side.

My pretty noona...
Nimekumind kinoma,wewe kweli wa kuninyima huu uhondo wa Dong Yi mpaka nimeigundua mwenyewe? Jamani jamani hii historical drama ni nzuri mnoooooo! Sijui ilikuwaje sijaiona miaka yote hii!

AIPOLO alianza kuiangalia sijui kaishia wapi hanipi feedback hadi leo!

Haishangazi wahusika pamoja na drama yenyewe kusomba tuzo miaka ile,wameigiza haswaaaaa.
Wewe unampenda nani kule?
Love you more Noona [emoji8]
 
naenda kudowload hiyo dong yi my dear kama ni nzur thanks niko naangalia whats wrong with secretary kim imepooza haina amsha amsha inachosha
My pretty noona...
Nimekumind kinoma,wewe kweli wa kuninyima huu uhondo wa Dong Yi mpaka nimeigundua mwenyewe? Jamani jamani hii historical drama ni nzuri mnoooooo! Sijui ilikuwaje sijaiona miaka yote hii!

AIPOLO alianza kuiangalia sijui kaishia wapi hanipi feedback hadi leo!

Haishangazi wahusika pamoja na drama yenyewe kusomba tuzo miaka ile,wameigiza haswaaaaa.
Wewe unampenda nani kule?
Love you more Noona [emoji8]
 
My pretty noona...
Nimekumind kinoma,wewe kweli wa kuninyima huu uhondo wa Dong Yi mpaka nimeigundua mwenyewe? Jamani jamani hii historical drama ni nzuri mnoooooo! Sijui ilikuwaje sijaiona miaka yote hii!

AIPOLO alianza kuiangalia sijui kaishia wapi hanipi feedback hadi leo!

Haishangazi wahusika pamoja na drama yenyewe kusomba tuzo miaka ile,wameigiza haswaaaaa.
Wewe unampenda nani kule?
Love you more Noona [emoji8]
Kwa kweli nimekukosea sana itabidi nilipe fine, nampenda sana Dong Yi, King mwenyewe, mtoto wa pili wa Dong Yi, Chun soo (sp) kaka wa Dong Yi, team nzima iliyokuwa inamsupport Dong Yi ikiongozwa na yule ofisa wa polisi, Yang Dal na mwenzie walioko kny kitengo cha music. OST zilizotumika pia nazikubali sana hasa ile ya Dong yi haegenium hapa mdogo wangu Damushin ndio uwanja wake. Uko episode ya ngapi? List yako inaendana na yangu?
 
Nipo ep7, ukweli hii http://kissasian.sh/Drama/Dong-Yi nilishaiona miaka ya nyuma nadhani 2011 kama sikosei, ujue mimi ni muhenga nilisahau jina lake, hatahivyo inanibidi niirudie tena maana iko poa sana.
 
Kwa kweli nimekukosea sana itabidi nilipe fine, nampenda sana Dong Yi, King mwenyewe, mtoto wa pili wa Dong Yi, Chun soo (sp) kaka wa Dong Yi, team nzima iliyokuwa inamsupport Dong Yi ikiongozwa na yule ofisa wa polisi, Yang Dal na mwenzie walioko kny kitengo cha music. OST zilizotumika pia nazikubali sana hasa ile ya Dong yi haegenium hapa mdogo wangu Damushin ndio uwanja wake. Uko episode ya ngapi? List yako inaendana na yangu?

Ooooopppssss finally nimeimaliza Dong Yi!
Jamani nimeliaje pale alipokuja kujengewa na wale masikini? (Final episode)
Hii drama ina mafunzo mengi sana kuliko nyingine zote nilizowahi kuziangalia.
Mali sio kitu bali utu

Tuko sawasawa ktk list,nimeinjoi sana couple ya King na Dong Yi. Na naweza kusema huyu ndiye mfalme bora kabisa ktk drama zote nilizoangalia. Jumong nilimkubali ila muandishi alinikera kwa kutokuwapa nafasi Jumong na Ye Soya.
Bora hii imekuwa na happy ending.
Nipe basi suggestion ya drama nyingine kali ya historical kama hii?
 
Sijasema ni mbaya bhana,ni vile tu nimeona kama ni overrated. Imekuwa popular sana,imetikisa sana ila haijafanikiwa kunitikisa kihivyo.

Anyways,nakaribia kumalizana na Dong Yi kisha nianze Mr. Sunshine.
Naomba uniwekee vyuma vitatu vikali vya historical niangalie maana kiukweli navutiwa zaidi na drama za vijijini kuliko hizi za umjini-mjini.
Naomba viwe vikali kwelikweli maana nakuaminia,episode zisivuke 60 please maana Dae Joyoung niliishiaga njiani sababu ya episode nyingi na najuta maana nimeitafuta sana siipati tena.
itapendeza kama utaiangalia Mr Sunshine Drama pindi utakapomaliza kuiangalia Dong Yi drama kwa sababu pia imeandikwa na kim eun sook akishirikiana na director lee eung bok kwa mara ya tatu.
kwenye list ya historical drama nathubutu kusema umenipa mtihani mgumu sana kuliko hata wa somo lile nisilolipenda darasani kipindi kilee halafu wewe mwenyewe unafahamu fika ya kuwa umekimbia humu ndani kwa zaidi ya mwaka mmoja so that ingelipendeza zaidi kama ungeliweka japo 50% ya historical drama ulizoziangalia.
lakini hakijaharibika kitu hivyo basi utaleta mrejesho wewe mwenyewe kwa drama uliowahi kuiangalia kama itakuwepo kwenye list hii.
Labda tuanzie hapa dada yangu mpendwa​
ulishawahi kusoma hadithi au kuangalia drama, movie inayozungumzia vita ya Imjin kati ya korea na japan?

  1. kama bado basi drama yangu ya kwanza nakushauri uitafute hii inayoitwa The Jingbirok: A Memoir of Imjin War. kwa ufupi The jing bi rok hiki ni kitabu kilichoandikwa na Ryu Seong-ryong (1542–1607) ambaye aliwahi kushika nyadhifa nyingi sana nyakati za uawala wa joseon chini ya mfalme seonjo. maana halisi ya jing bi rok ni kujisahihisha akimaanisha ya kwamba joseon inapaswa ijifunze kutokana yaliyotokea nyakati za vita iliyodumu kwa miaka 7 dhidi ya wajapani. yapo mambo mengi yaliochangia joseon iwe dhaifu kipindi hicho na kupelekea kuwapa nafasi wajapani wafanye wanachokitaka kwenye ardhi ya korea. humu ndani anazungumzwa zaidi huyu great thinker aliyeitwa Ryu Seong-ryong na harakati zake za kuipambania joseon mpaka mwisho wa nguvu zake.humu ndani ni mwendo wa vita za makundi ya kisiasa kwenda mbele. aliyeigiza uhusika wa ryun seong ryeong ni mzee kim sang joong a.k.a mzee ahmogae wa rebel thief who stole the people pamoja na city hunter drama
1542110297955.png

2. admiral yi soon shin: aigooo nimesahau kumbe hutaki drama inayozidi episode 50 lakini kwa ukaidi wangu wa kiafrika nimeamua niiweke na hii ili usije ukanisumbua huko mbele. Ryu Seong-ryong na yi soon shin wote hawa ndio walikuwa ni nguzo ya korea wakati wa vita dhidi ya japan tofauti yao ni kuwa mmoja alikuwa ni mwanasiasa na mwengine alikuwa ni mwanajeshi. hii drama inazungumzia zaidi maisha ya huyu shetani wa baharini aliyeitwa yi sooon shin kuanzia maisha yake ya utotoni, alipokutana na ryu seong ryong mpaka kufikia nyadhifa ya kuwa naval commander. laiti kama huyu jamaa angelikuwa ni mzungu basi tungelazimishwa tumsome kwenye somo letu la historia lakini bahati mbaya alikuwa ni mkorea. kama si uwepo wa huyu jamaa maeneo ya baharini basi pengine leo hii korea isingelikuwepo kwa sababu uvamizi wa japan ulipelekea waweze kuiteka miji mikuu mitatu ya joseon na kupelekea mfalme seonjo na watu wake wakimbie mji lakini kikwazo kikubwa ilikuwa ni kwa huyu shetani wa baharini. kwenye vita 23 alizoziongoza dhidi ya japan huku akiwa na rasilimali chache zaidi ya wajapani aliwafanya wajapani waoenakane ni mafala na mapimbi kumbe wajapani hawakuwa na makosa ila kosa ilikuwa ni la yi soon shin kuwepo hai.kuna vita moja ya myeongyang huyu shetani alikuwa na meli 13 tu na wajapani walikuwa na meli 133 lakini cha ajabu wajapani waliomba pooo bila ya meli hata moja ya wakorea kuharibika, hahahahaaaa jamaa alikuwa mzimu.hii drama ina episode 134 halafu ni ya mwaka 2004 naogopa hutovutiwa na camera zake ila ni nzuri sana.muigizaji mkuu ni kim myung min ambaye kupitia six flying dragons aliigiza uhusika wa sambong (jeong do jeon)
1542110520698.png
3. gu am heo jun drama: daebak, ina maana kumbe huyu ryu seong ryung, yi soon shin na doctor heo jun wote walikuwepo nyakati za utawala wa mfalme seonjo, drama hii inazungumzia maisha ya daktari genius aliyekuwa hajasomea elimu yake ya udaktari chuo chochote kikubwa duniani na jina lake ni heo jun ambaye ndiye daktari wa kwanza nchini korea kuandaa kitabu chenye kuzungumzia tiba mbali mbali za kitamaduni kilichoitwa dongui bogam, huyu heo jun baadae anachaguliwa kuwa daktari binafsi wa mfalme seonjo na familia yake,siku utakayoamua kuitafuta drama hii basi unapswa uandae na ndoo ya maji kabisa kwa ajili ya kuhifadhia machozi yako kwa sababu pindi maji yatakapokuwa hayapatikani mtaani kwenu basi utatumia machozi yako kwa ajili ya kusafisha mwili wako. jamaa anapata tabu sana sana kama alivyokuwa jang young sil ambaye ndiye mwanasayansi wa kwanza nchini korea.hii drama imeniliza mpaka nikawa natamani niingie kwenye Tv nimtwange mtu ngumi kwa hasira na hisia za uchungu nilizokuwa nazo, dah pumzika kwa amani kim joo hyuk.
1542110668174.png
4. jeong do joon drama: kama umebahatika kuiangalia six flying dragons basi utakapoiangalia drama hii utakuwa unapita mule mule, kwenye six flying dragons kwa kiasi kikubwa tuliaminishwa ya kwamba shujaa alikuwa ni yi bang won ambaye baadae anakuwa mfalme wa tatu wa joseon na aliitwa Taejong.Lakini kupitia drama hii utapata kujifunza kiundani maisha ya huyu msomi na mwanamapinduzi jeong do jeon kuanzia zero to hero and finally kifo chake. jeong do jeon jina lake la umaarufu ndio hili sambong. ilikuwa kuwaje mpaka akakutana na yi seong ye, ilikuwa kuwaje mpaka akawa na akili nyingi kwenye ulingo wa siasa,akaweza kuwaingiza kwenye mgogoro mkubwa mageneral wawili wakubwa ambao ni yi seong ye na choi young na ilikuwaje mpaka akaingia kwenye mgogoro ni yi bang won na kupelekea yi bang won kumuua sambong na kumtangaza ni msaliti wa joseon utafahamu pindi utakapoangalia drama hii.
1542111227643.png

5. Yi San drama: huyu yi san baba yake alikuwa ndiye crown prince sado ambaye aliuwawa na baba yake mzazi baada ya kumfunga bila ya kumpa hata tone la maji, aigooo baba alikuwa mkatili sana, baada ya kumrithi babu yake huyu yi san ameendelea kutajwa kama ni miongoni mwa wafalme bora waliowahi kutokezea nyakati za utawala wa joseon.

unaonaje ukachagua moja kati ya hizo au kama hakuna iliokuvutia cha kufanya weka list ya drama ulizoziangalia baadae nitakuchagulia nyenginezo inshaallah.

1542111585844.png
 
Yan dr.heo jin ni drama ambayo siwez isahau na sijui Kama nitaona drama nyingine yenye hisia zakwel,, some time imenifanya nidondoshe choz,,,R.I.P bro
nilifikiri niko peke yangu kumbe nina wenzangu wamejaa kapuni.
ushawahi kuangalia drama ukafikia steji hadithi ya drama unataka uibadilishe na uipeleke unavyotaka wewe mtazamaji?
hahahahahahahaaaaaa yalinikuta wakati naangalia gu am heo jun.
nilikuwa nawachukia wale madaktari wazee waliokuwa wanamuwekea bifu heo jun wakati jamaa kaweka rekodi ambayo hakuna mpumbavu yeyote aliyeiweka baada ya kufaulu alama za juu mtihani wa taifa.
jamaa aliweka rekodi ya kuwa daktari wa kwanza kupewa nyadhifa ya uwaziri wa ngazi ya juu serikalini lakini kuna pimbi bado wakawa wanamwekea bifu.
hii dunia haiwezi kuwa ya amani kama haters wataendelea kuwepo lakini pia dunia haiwezezi kuwa ya amani kama haters hawatakuwepo.
ni mwendo wa kula korosho huku ni unaji konki konki
 
Nimemaliza Episode Ya Kwanza Ya The Beauty Inside...

Nimecheka Mpaka Nimejishtukia...

Mambo Yake ni ya Kama This is My Firts Life, Nimecheka Damushin...

Huyu Kaka Ni Chizi Sana..
 
Ruler+Master+Of+The+Mask+Episode+09_283383.jpeg

Nimemaliza kuangalia hii kitu,nilikuwa nikiona cover naichukulia poa ila mambo ya humu ndani ni makubwa.

Ila niliumia sana pale mrembo Hwa Gun alipodead,nimeupenda uhusika wake humu hadi nilitamani kaka yetu Prince Yi Sun awe nae.
Ruler Master of the mask sio poa kabisa najuta kuchelewa kuiangalia,najipanga kuvamia kitu ya GOOD WITCH
ruler-master-of-the-mask-korean-drama-2017-wiki-cast-summary-yoon-sohee-1.jpeg
 
Kwa kweli nimekukosea sana itabidi nilipe fine, nampenda sana Dong Yi, King mwenyewe, mtoto wa pili wa Dong Yi, Chun soo (sp) kaka wa Dong Yi, team nzima iliyokuwa inamsupport Dong Yi ikiongozwa na yule ofisa wa polisi, Yang Dal na mwenzie walioko kny kitengo cha music. OST zilizotumika pia nazikubali sana hasa ile ya Dong yi haegenium hapa mdogo wangu Damushin ndio uwanja wake. Uko episode ya ngapi? List yako inaendana na yangu?
hahahahahaaaaaa huwezi amini nimepunguza sana ufuatiliaji wa korean ost ila bado sijaacha kufuatilia korean music.
ni mpenzi wa nyimbo za kawaida siku hizi ila ziwe za miondoko ya ballad.
lakini sikumbuki ni lini nimefuatilia muziki wa nyumbani kwetu na marekani.
huyu brother park hyo shin na ahjussi wengineo wanazidi kunitumbukiza kwenye shimo la wakorea na kutoka siwezi.
sasa kuna ahjussi mwengine anaitwa lim chang jung nimeanza kumfuatilia tokea jana yaani ananimalizia bando langu kwa ajili ya kutafuta nyimbo zake na balaa lake anapoimba kama sakata la korosho.
jamani wakorea kila unayemtazama anamshinda mwenzake wakati huku kwetu diamond ana mwaka wa 10 anaringa yeye tu.
mpaka najisikia aibu kuwafuatilia wakorea.

ujumbe wa leo jamani lakini natumai huu wimbo haumuhusu yeyote humu ndani.
Lim Chang Jung -There has never been a day I haven't loved you.

hadithi ya mapenzi ndio hadithi pekee ambayo msimuliaji anaweza kukusimulia jinsi mapenzi yao yalivyoanzia hadi yalipoishia

Jamaa noma huyu kuna ost yake moja ipo kwenye Three Days ni nomaaa
Nimezijaza zaidi ya 200
 
Mona Umejishukiza?

Basi Itakuwa Yupo Unaemuhusu...
 
Back
Top Bottom