Kwa wapenzi wa Korean Dramas, hii ni thread yako!

Nakuelewa sana mkuu.. Hongera[emoji120]

Sent from my GT-I9300 using Tapatalk
 
Hi ni bonge la drama nilivyoanza nilisema tu ngoja nitazame maana Sina drama pendwa ila nimekua mgonjwa taaban...Natamani wamama wengi watizame waone jamani.


Sent using Jamii Forums mobile app
 
[emoji7][emoji7][emoji7][emoji7]
hivi sikupaswa kuongeza "the"?
hii lugha inatufanya wengine tuwe bad debt written off.
Hahaa mkuu hapa hatupo kwenye mtihani wa grammar cha msingi uandike nielewe.. Kiswahili tu tunaputanga.. hasa mm

Sent from my GT-I9300 using Tapatalk
 

Ndio kwanza nipo ep ya 21, yupo kwenye harakati za kumuozesha mwanae kwa Prince Dammang...

Yi San nzuri ila huku nishazoea mikikimikiki basi nikiiangalia hiyo naona imepoozaaaaa ila ni nzuri sana na visa vyake ni vizuri na vya kuhuzunisha.

Sometimes nahisi ni vile tu nimezoea KissAsian ila kuna kipindi inanisumbua nakuwa kwenye moto wa kuangalia drama halafu inakataa kuplay mf ep 11 & 18 sikuangalia. Jana usiku nimemaliza ya 19 ya 20 ikakataa inaniambia error gani sijui!
Nikaachana nayo nikaangalia Yi San leo nairudia nikajaribu ep 20 ikakubali!

Sina namna maana kuna drama nyingi hazipo KissAsian hivyo lazima nipambane nayo tu.


Sent from my iPhone using JamiiForums
 
Hii Queen Sandeok ndio ameigiza yule dada wa kwenye 49 days? Huwa naitamani ila ndefu sana khaaa

Sent using Jamii Forums mobile app

Uwiiiiiiii Unnie kama hujaangalia hiyo season sahau kama umewahi kuangalia season za kikorea.
Yani nilipokuwa nakaribia kuimaliza nilinunaje? Ni nzuri mnooooo mpaka nilitamani wangeongeza episode.
Ina ep 62 tu, wenzio tunakamua hadi 120 hizo unasema nyingi? Lol


Sent from my iPhone using JamiiForums
 
Hivi ni 62 sio 80? Swali langu halijajibiwa ndio hiyo ninayoijua?

Sent using Jamii Forums mobile app
 
[emoji12][emoji12][emoji12] mimi nina bae wengi wewe karibu kila drama natoka nae mmoja japo huwa sidumu nao, halafu mimi mara nyingi huwa navutiwa na second lead sijui kwa nini

Sent using Jamii Forums mobile app

Nilitaka kukuiga nikashindwa maana tulishaanza kumgombea Jin Goo hahaaaaa
Ila kiukweli kabisa hakuna wa kumfikia Il Gook, ile ni habari nyingine.


Sent from my iPhone using JamiiForums
 
Nilitaka kukuiga nikashindwa maana tulishaanza kumgombea Jin Goo hahaaaaa
Ila kiukweli kabisa hakuna wa kumfikia Il Gook, ile ni habari nyingine.


Sent from my iPhone using JamiiForums
[emoji23][emoji23][emoji23] bora maana undugu ulikuwa unaelekea kuisha. Baba mkwe mimi nampenda pia ila kawaida nadhani ni kwa sababu sikuwahi kuimaliza Jumong

Sent using Jamii Forums mobile app
 

Sasa ngoja nikupe siri [emoji4]
Nilianza kumkubali tokea kwenye Jumong, baadae na nyingine za historical lakini sikuwa nimemfaudu vizuri.
Drama iliyonikata kiu ni A Man Called God! Achaaaaaaa

Si unajua kule kijijini kuko rafu sana kuna vitu huwezi notice kwa haraka, ila pale alipoigiza Choi Kang Ta/Peter Pan nilichokaaaa.
Yani nilikuwa natamani nimtoe Sin Bobae niingie mimi hahaaaaa
Ndio maana wadada watatu waligongana mule, japo aliyeendana nae ni yule mtoto wa tajiri too bad moyo wake ulikuwa kwa muandishi masikini Sin Bobae.

Zile modern fights, jamaa alikuwa anapigana kibishoo hatari, ile mikato ya kigentleman...
Scene niliyoipenda ni pale yupo kwenye ndege na Vivian na pale darajani anapomuambia Vivian “Disappear....”
Niishie hapo bwana.

Natamani aje na series 2 kwa mpigo, historical na mjini na zote nitaziangalia zikiwa on going kwa mara ya kwanza.

Wala usisumbuke kunionesha hao wengine, I’ve made up my mind, forever Il Gook team [emoji1434]


Sent from my iPhone using JamiiForums
 
Haha A man called God nimeisahau aisee siku nyingi sana nimeiangalia, kama miaka 7 iliyopita

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Haha A man called God nimeisahau aisee siku nyingi sana nimeiangalia, kama miaka 7 iliyopita

Sent using Jamii Forums mobile app

Sawasawa na mimi ila mwenzio hata uniamshe usingizini uniulize chochote nitakujibu kwa ufasaha kabisa.

Yani mpaka leo huwa nakumbuka jinsi yule Detective alivyokuwa anambembeleza Sin Bobae... “Bobae....” hahaaaaa


Sent from my iPhone using JamiiForums
 
Hi ni bonge la drama nilivyoanza nilisema tu ngoja nitazame maana Sina drama pendwa ila nimekua mgonjwa taaban...Natamani wamama wengi watizame waone jamani.
Sent using Jamii Forums mobile app
  1. wapenda majivuno inawahusu hii drama (Han Seo-Jin)
  2. wapenda kusoma kwa kuhofia bila ya kuwa na elimu kubwa basi mafanikio yako yatakuwa madogo inawahusu hii drama (Kang Ye-Suh + cha min hyuk + han seo jin)
  3. wale wazazi wanaolazimisha watoto wao wasome fani wanazopendelea wao inawahusu hii drama (han seo jin + Cha Min-Hyuk)
  4. wale wazazi wasiopendelea kuona wenza wao wakiwa na kauli kubwa za kimaamuzi ndani ya familia inawahusu hii drama.(Seung-Hye)
  5. wale ambao hupendelea kupanda juu kimafanikio kwa kutegemea mgongo wa wenzao inawahusu hii drama (kang joon sang )
  6. wale wasiofungamana na upande wowote inawahusu hii drama (wazee wa sometime yes and sometime no) kama namuona ahjumma wangu (jin jin hee)
  7. ongeza na zako talnam ili wenye wivu na SKY CASTLE wazidi kupasuka kama mabofu.
huyu ahjumma atakuwa wa kwanza kwenye list yangu napenda sana tabia zake, leo rafiki kesho adui.
🙂🙂🙂
jin jin babyyyyyy
 
[emoji23][emoji23][emoji23] bora maana undugu ulikuwa unaelekea kuisha. Baba mkwe mimi nampenda pia ila kawaida nadhani ni kwa sababu sikuwahi kuimaliza Jumong

Sent using Jamii Forums mobile app
baba mkwe kwa sababu ya SONG MANSE?
hivi utamsubiri hadi lini yule mpendwa na wengi?
kazi unayo kwa brother man yule, njia pekee ya kuwa wakwako peke yako ni kumfunga kamba kama mwendawazimu aliyetolewa kwao ili familia iwe tajiri.
😛😛😛

wa kwangu mimi uyo mwenye tabia za baba yake aliye upande wa kulia kwangu, Song Miguk hafai kuanzisha udugu kwa sababu ana akili nyingi kuliko za mdogo wangu wa kike.
 
Me my best series n CITY HUNTER,FAITH AND SIX FLYING DRAGON

Sent using Jamii Forums mobile app
mkuu inaonekana umeangalia drama 5 ndio maana ukaweka top 3 zako city hunter, faith na six flying dragon
natania tu natumai hutachukia.

faith drama nakumbuka lee min ho aliigiza uhusika wa general choi young, miongoni mwa watu wagumu kuwahi kutokezea kwenye tawala ya GORYEO. Urafiki wake na general yi seong gye ulifutika ghafla kwa sababu ya madaraka, kweli siasa haina rafiki wala adui wa kudumu.

ukiangalia jung do jeon drama ndio wameelezea kiundani sababu zilizopelekea wawili hao kutwangana majambia wenyewe kwa wnenyewe.
unajua kilitokezea kitu gani?​
mwaka 1388 yi seong gye aliamrishwa akapambane na jeshi la MING china ambalo lilikuwa linaupigania mji wa liaodong ambao GORYEO walikuwa wanadai ya kwamba ni mji wao kwa sababu liaodong ulikuwa ni mji wa GOGURYEO nyakati hizo za mwendawazimu GWANGGAETO.
Lakini cha ajabu general Yi Seong-gye akakataa amri ya mfalme ya kuelekea kaskazini na jeshi lake na alitoa sababu 4 za msingi zilizomfanya akatae kueleke kaskazini kwa dhumuni la kupambana na MING China.
Sambong aliandika barua kwa mfalme kwa mujibu wa drama yenye sababu zifuatazo
  1. GORYEO ni taifa dogo hivyo basi halina uwezo wa kupambana na taifa kubwa la MING
  2. Ni ujinga kuanzisha kampeni ya kijeshi wakati ambao wananchi walipaswa wawekeze kwenye kilimo.
  3. kama tutawapeleka vijana wetu kupambana maeneo ya kaskazini basi tutawapa upenyo wajapani watushambulie maeneo ya kusini
  4. mvua kubwa zitakazonyesha zitasababisha maandalizi ya kivita yawe hafifu.
kilichotokezea choi young akaamua kuweka ngumu si anajua ana sauti mbele ya mfalme, kudadadeki general yi seonggye akamsikiliza sambong na kuamua kurudi mji mkuu bila kuelekea vitani.
acha wachapane wenyewe kwa wenyewe mpaka choi young akanyanyua mikono juu.
mwisho wa siku general choi young alinyongwa hadharani, kifo chake ndio kilizidi kudidimiza matumaini ya taifa la goryeo kuendelea kuwepo.
bwana huyu kabla ya kunyongwa alitabiri ya kwamba kaburi lake halitaota hata jani moja, cha jabu utabiri wake ulitimia kwa muda mrefu sana na kaburi lake liliota majani mnamo mwaka 1976 wakati alifariki 1388.
baada ya miaka 588 ndio kaburi lake liliota majani, hmmmmmmmmm fixed costing
huyu jamaa alikuwa mtabiri wa ukweli.
🙂🙂🙂
hivi kwenye six flying dragons stori yake mbona niliiona ya kawaida lakini watu wengi wanaisifu
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…