Kwa wapenzi wa Korean Dramas, hii ni thread yako!

Hahaha kwakweli wenye wivu watuachee

8. Wazazi wasotaka kukubali uhalisia wa matatizo ya watoto wao (coach Kim)

9. Watoto wenye uthubutu wa kumsema mzazi mpaka akajiona sio timamu lol ( se ri yeh bin, seo Joon)

10. Wapenda kutumikishwa bill hata kujali kuwa utu wao unapotezwa (Dr. Woo, Driver joo).
Naipenda Sana hi drama wacha rate ziendelee kupanda inastahili mwanzo sikuelewa kabisa, nlikua naona watu wengi lol

Sent using Jamii Forums mobile app
 
[emoji16][emoji16][emoji16][emoji16][emoji16][emoji16][emoji23][emoji23][emoji23] hapana mkuu sijachukia ila mi ni expert wa muvi nimeangalia season more than 130 ila city hunter ndio nilitoa bikra ya k drama 2012 na faith ikafatia miaka hio hio ndio maana mpaka leo nazipenda na nna ziheshimu afu six yenyewe napenda action yake na uwepo wa lee bang ji na cheuk sa gwang mkuuu ila izo n top three ila nnaseries ambazo nna zipenda kama

1.queen seondok
2.the legend
3.legend of blue sea
4.k2
5.moon lover
6.healer
7.remember war of the son
8.doctor stranger
9.blood
10.mr sunshine
11.iris
12.athena
13.warrior dong soo

Izo nazo nnazikubali kinyama pia

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Namtaka huyohuyo sukari ya warembo, akichepuka na mimi si nachepuka

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Afu anafanya cameo kwenye crowned crown au kingdom moja kati ya hizo
 
Afu anafanya cameo kwenye crowned crown au kingdom moja kati ya hizo
yes amefanya kwenye the crowned clown drama episode 1 kwa sababu ya uhusiano wake na director kim hee won. Wawili hao walifanya kazi kwa pamoja kwenye drama ya MONEY FLOWER.
ameigiza uhusika wa mfalme seonjo ambaye ndiye baba wa mfalme gwanghae
 
Wazee,
Ni drama zipi za kiinteligence kama IRIS, City hunter, Athena zilizotoka?

Sent using Jamii Forums mobile app
  1. secret forest /stranger
  2. criminal mind
  3. pied piper
  4. 3 days
  5. tunnel
  6. life on mars
  7. k2
  8. hidden identity
  9. less than evil
  10. terius behind me
  11. lawless lawyer
  12. signal
  13. the player
  14. mad dog
  15. bad guys
  16. the ghost detective
  17. partners for justice
  18. heartless city
  19. gap dong
  20. queen of mystery
  21. mrs cop 2
  22. sign
  23. incarnation of money
  24. voice season 1, 2
  25. defendant
  26. black
  27. come and hug me
  28. children of a lesser god
  29. phantom
unywaji pombe kupita kiasi ni faida kwa mzalishaji.​
 
daebak, umemaliza kila kitu.
kama ungelikuwepo uwezekano tungelianzisha special thread kwa ajili ya SKY CASTLE, ila nimehofia tutakuwa tunafanya ubaguzi kwa wale wenzetu wanaoangalia makjang (막μž₯ ) drama kwa sababu ili uingie kwenye thread yetu lazima usajiliwe.
hahahaaaaaaaaa watapata tabu sana team encounter, gwanggaeto, yi san, the crowned clown n.k​

nimeshaihifadhi episode 17 muda huu lakini naiweka kiporo mpaka itoke episode 18 usiku wa leo inshaallah, si unajua raha ya kizuri ukile kwa wakati mmoja na si kwa mapande kama ujenzi wa barabara za nchi za kiafrika.

sasa basi mwenzangu kwa mujibu wa takwimu zilizotolewa leo na taasisi ya Nielsen Korea ni kwamba episode ya 17 imefikia 19.9% kwa kuangaliwa nchi nzima, na mji wa Seoul imegonga 21.9 % ukilinganisha na episode 16 hivyo basi kwa hesabu za kutumia vijiti na mzigo wa mawe kama watoto wa nursery, rate imeongezeka kwa 0.7%.
kwa cable tv goblin drama ndio inashikilia rekodi ya kufikia 20.5% nchi nzima kwa episode, zimebaki episode tatu na kama itatokezea na leo rate ikaongezeka kwa 0.7% basi sky castle ndio itakuwa ni drama iliyoangaliwa zaidi na wakorea kwa cable tv drama per episode.

kuna watu humu ndani na wale wanaopita bila ya kuchangia chochote unaweza kushangaa wanatamani account yangu niisahau nywila ili stori za sky castle niwapunguzie.
teh teh teh teh povu naruhusu............
 
Yi San(Wind of the Palace) nimefika Ep. ya 50. kwa sasa nafikiri historical drama mpya. Miye natumia Drama cool wala sipati tabu, Ingawa ilikuwa ina-play na kugoma wakati nilipokuwa natumia Google Chrome lakini sasa mambo ni hot sababu natumia UC Browser.
 
wale walevi wenzangu tunaokunywa korean ost pamoja na sauti za waimbaji tukutane kwenye TEST 1 yenye marks 15 πŸ˜›πŸ˜›πŸ˜›,.
kuna bwege anaitwa damushin humu JF akisikiliza wimbo kidogo basi ameshamfahamu muimbaji kwa wale anaowafahamu lakini test ya leo kapigwa 0/15.
hii video kwa wale wenye mb 20 za bure waiangalie halafu kwa ukweli na uwazi pasina kuwepo chembe chembe za cheating atwambie kama amepata au kinyume chake.
  1. je kati ya hao watatu ni yupi LYN mwenyewe?
  2. je kati ya hao watatu ni yupi mwanamme?
ukisikia copy and paste ndio hii si kama ya bwana yule mchekeshaji.............
sitaki kusema jawabu linaanzia dakika ya ngapi japokuwa kama naliona.
hivi huyu ni mwanamme au mwanamke aliyevaa nguo za kiume?
hapana hapana anapaswa afanyiwe uhakiki wa kijinsia, isijekuwa mambo ya sungkyunkwan scandal drama.

kama namuona mzee mo palmo akiwa na tabasamu usoni, mzee wa mizuka.
bonyeza cc button kwa tafsiri ya kiingereza.
variety show za korea ndio zinanifanya nirambwe hela kwa ajili ya internet kila siku, hivi TBC, ITV, star tv, channel 10 na nyenginezo bado zipo?

ngoja niwakumbuke walevi wenzangu ila sifahamu kama bado wanaendelea na unywaji wa kilevi cha ost.
Prishaz noona.
Khantwe mpenda wengi.
Nifah mpenda il kook.
aminas simba mbovu.
 
Hehehe japo simjui Lyn Wala nyimbo zake, ila no. 3 nlidhani ndo mwenyew maana hiyo sauti ni motooo.


Sent using Jamii Forums mobile app
 
Nami usiku najishushia zangu Nani anataka stress ya kujua kilichojili ya kuwaza niumwe kichwa nikufe hahaha. Sky castle all the way

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Kweli huu unywaji pombe kupita kiasi khaaa

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Sunbae mimi ost sio mlevi kabisa kifupi huwa sizielewi na sizifuatilii maana nyingi zinaimbwa kwa lugha yao. OST pekee ambazo hazinitoki kichwani ni Dream High, How can I love you kutoka Descendants of the sun na nyingine ya kwenye The Heirs siikumbuki jina zingine zote huwa nazipenda ndio ila nikimaliza drama nazo naachana nazo

Sent using Jamii Forums mobile app
 
hivi huku Tanzania upo timu gani
ya msafi au yule more moto aliyepata msiba juzi?

unapenda nyimbo za kihindi?
hili swali la mwisho jibu lake bora liwe hapana.

nikikwambia nina miaka takribani au zaidi ya 3 sijafuatilia sanaa ya kimagharibi utaniamini?

kipindi kile chris brown anatamba na wimbo wake unaoitwa dont wake me up ndio niliacha kufuatilia muziki wa magharibi.
 
Hahahaha mimi sina timu ila napenda muziki mzuri ambao kwa mooo faya naona umeshuka kiwango kidogo si kama siku za nyuma (Nifah asione hapa...na hata akiona asijibu)
Nyimbo za kihindi walaaa sema huwa napenda kuwaangalia wanavyocheza
Kuna swali nimebakiza?
Ndio naamini, maana ulishawahi kusema hata siku za nyuma
Sent using Jamii Forums mobile app
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…