Kwa wapenzi wa Korean Dramas, hii ni thread yako!

Alikuwa anampenda Wang yu mpaka sio vizuri

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Kikundi kipi unachozungumzia?! Wale kina Gil Taemi na Gil Sumi, au wale ma- monk or ndugu zake na Chuk sagwa.?!
Kinaitwa Moomyung. Kile Kikundi Ambacho Mama Yao Ddang Sae Na Boon Yi Ndiye Alikuwa Leader. Gil Su Mi Alikuwa Member Pia. Kilikuwa Na Members Wengi Tu Hadi Court Ladies Ndani Ya Palace Yenyewe Na Pia Wafanyabiashara, Wanasiasa n.k. Wanafanya Shughuli Za Kawaida Za Kijamii Ila Wapo Kwenye Missions Maalumu Ingawa Wengi Wao Walikuwa Hawajuani Mpaka Pale Ambapo Siku Wanakutanishwa Kwenye Kikao Chao Maalumu Kinachofanyikaga Kwa Nadra Sana.
 
Halafu drama alizoigiza nilizoiona Auditor Noh huwa anaigiza roho nzuri (utu) i.e City Hunter, Jing Birok na hii ya sasa. Sijui atakuwa ana utu kweli? Ananivutia sana anavyoigiza vile...
hizi skendo zinazoibuliwa mara kwa mara nchini korea dhidi ya celebrities zinanifanya niogope kutoa hukumu kwa mzee wetu Assad lakini hata mimi nina imani mzee wetu ni mwenye matendo mema akiwa mbele ya camera na nyuma ya camera.
hivi uliwahi kudhani kama huyu mzee marehemu jo min ki atakuwa na tabia chafu?
kampeni ya me too ilipelekea mpaka ajitoe uhai wake
unaweza kukuta hata muandikaji wa hii comment ni shetani aliyevuka mipaka.
 
Kumbe Ashakufa!!! The Great Queen Seon Deok, ILjimae, Scarlet heart na aliigiza kama mwema.
 

Leo nimekuquote mapema kabla hujafuta kama jana, niliiona ile basi tu nimemute.

Haki umenishtua sana, nikiri nilikuwa sijui hili! Mpaka nimeenda kigoogle kwanza nihakikishe maana ndio naangalia great seer jamaa katisha sana, nimewahi kumuona ktk drama kibao tu so namjua vyema ila sikuwa najua hilo la kujiua na tuhuma zilizokuwa zikimuandama.

Nimejiuliza hili lilinipitaje ndio nikakumbuka wakati ule aliojinyonga niliachana na drama hizi nikapumzika, dah nimesikitika kwakweli.

Nimekoma kuaminia watu, khaaaaaaa! Hata Auditor Noh sitaki kumjengea picha ya wema tena.
Huyu baba alivyoigiza upole kwenye East of Eden na Queen Seondeok nimechokaaaaa!


Sent from my iPhone using JamiiForums
 
BTW Banker umeshaone ep ya jana? Naona KissAssian hawajaweka bado, ndio maana huwa sipendi haya mambo ya ongoing
"If you leave this town you won't have kids. That is what the fortune teller told me."
mama alipoona mtoto wake safari ya seoul imeshamtia wazimu akaamua kuziblock credit card zote 🤑🤑🤑, seo bo geo anafika seoul hana hela wala sehemu ya kukaa (wazee wengine vichwa ngumu kuliko jiwe la msingi)
nimependa uhusika wa kijana Seo Bo-Geor licha ya kuwa ni trouble maker lakini muda wote anaonekanwa kumjali sana bosi wake auditor noh dae ho hususan anapokutana na changamoto kubwa zinazoweza kuhatarisha maisha yake.

president Kang Sam-Do ni mwanadamu mmoja hatari sana kuliko mbwa mwitu aliye mawindoni, mpaka sasa sijajua dhumuni lake la kumleta noh dae ho makao makuu haliyakuwa anafahamu fika jamaa ni mwenye msimamo na asiyeogopa chochote haijalishi msosi wake ni mwili wa bosi.
jaribu kuangalia counter plan aliyokuja nayo kwa kumrudisha Lee Hae-Gon awe kama ni vice president wakati mwanzoni jamaa aliondoshwa ndani ya benki na kuishia kufanya kazi subsidiary company zilizochini ya daehan.

dah! vice president Yook Gwan alijipa matumaini makubwa sana ya kwamba anakwenda kumuondoa madarakani raisi wa benki kupitia kura wajumbe wa mkutano mkuu pamoja na nguvu aliyokuwa akipewa na viongozi wa serikali lakini cha ajabu ngoma imegeuka kwake, Yook Gwan anafahamu fika ya kwamba rais ndiye muhusika mkuu wa sakata la seomin agency lakini ameshindwa kumpa siri bwana Assad.

unawezaje kutoa siri haliyakuwa watoto wako wawili wameshapandishwa cheo ghafla baada ya wewe kufukuzwa kazi?
shikamoo president Kang Sam-Do.
naisubiria vita kati ya mbwa mwitu kang sam do dhidi ya simba wetu noh dae ho

uyo aliyevaa mavazi meupe mwenye jinsia ya kipekee ndie wa kwangu mimi na hao waliobakia chukua wewe wote kama sheria zinakuruhusu, kama sheria haziruhusu unaweza kuwagawa kwa wengineo wenye mahitaji humu ndani.

when you first become a banker, a good bankers mission is to be honesty and trustworthy that what we all learn, but once your sense of duty goes sour and your beliefs falter we must make a choice, whether that choice was right can be proven by honorable retirement thats why us bankers should never seize to question ourselves.
am I a good banker?
(auditor noh dae ho)​
fedha, fedha, fedha imekuwa muhimu kuliko ...............................................
 
huyu mzee katika muvi zote alizocheza akanikosha zaaidi ni kwenye Emperor of the Sea, kiukweli alikuwa ananikosha jinsi alivyokuwa anajua kuchangamkia fursa, but hata kichina chake kilinikosha alivyokuwa anaongea.
Kwenye Dong Yi sikumfaidi sana sababu alikufa mapeeeema kabisa mwa Tamthilia hiyo, na haielewekialikuwa mzuri or mbaya. But hizo zilizobakia huyu mzee ni Kauzu kweli kweli.

Hivi yule jamaa aliyecheza kwenye the Great King kama Genera FengBa hivi kuna tamthilia yoyote amewahi kucheza ni mwema?!
 

Hivi ujue kwangu Ep 5&6 hazikuwa na subtitles? Nilikuwa nabahatisha tu tena nikawa najisemea leo ngoja nipime uelewa wangu wa Kikorea, lol.
Nilikuwa nasikia tu Seoul mara naona dogo yupo kwenye gari, card zote zimegoma nikadhani hana pesa kumbe mama ndio aliziblock?
Ila baadae 7&8 subtitles zilikuwepo ambazo hizi episodes naona ndio zilikuwa kali zaidi, Banker imekuwa hatari fire, ngoja tuone itakuwaje.

Ila Vice Presidaa alimalizwa kimafia sana, yeye na wafuasi wake wote fyekelea mbali.
Yule Secretary wake alinusurika hahaaaaa
Na akafungwa mdomo kwa watoto kupewa ajira tena nzitonzito, President sio wa mchezo.
Niliogopa pale alipomuambia Auditor Noh kuwa “Don’t trust President Kang too much “! Akaondoka zake
Nahisi baadae utakuwa mpambano mkali...

Hahaaaaa mimi bado sijampata, naona hakuna mwenye vigezo vyangu, hivyo hapo kwenye picha vivulana na Auditor Noh namuona kama Uncle wangu.


Sent from my iPhone using JamiiForums
 

Mimi huyu drama nyingi nilizomuona huwa anaigiza kama Prime Minister hadi nimemzoea hivyo.
Kwenye Jumong alinikera alivyokuwa anatibua mambo na wapambe wake, na kwenye A man called God alikuwa mafia, kilema lakini mziki wake hatari.

Kwenye Dong Yi alikufa mapema maana alikuwa mwema, ndio wakamuondosha mapema maana alikuwa anazuia mipango ya akina Lady Jang na wenzie.


Sent from my iPhone using JamiiForums
 
Hahaha hata mie japo ndo natarajia niende episode ya pili niliona dalili kuwa hakuna Comedy likewise kwenye Sambong Project nionavyo.
 
Halafu hii thread ina nini?! Maana nishaanza kuwa mlevi sasa, wa humu kila nipatapo nafasi lazima nizame humu.
Jamani baadae wacha nikaiendeleze sambong project, maana nikisema nitazame The Great King Sejong nitalala saa saba na nusu sababu ni ndefu mno.
 
Utampenda ukimtazama kwenye Emperor of the Sea
 
Kuna drama yoyote iliyokamilika inanifaa kuangalia katika kipindi hiki??? Suggestion please
itafute the fiery priest drama hutajutia bando lako nakuahidi japokuwa imebakisha takribani episode 4 kumalizika.
kim nam gil a.k.a bidam, lee ha nee a.k.a honey lee and others. Ni mwendo wa action za ukweli, comedy pamoja na religion.
wahubiri kama hawa wanapaswa wawepo nchi za kiafrika ili watupiganie haki zetu, huku kwetu wahubiri wengi wa dini kauli mbiu yao kubwa ni mungu ataleta au toa fungu la 1000 kwa jina la bwana.

  1. https://www2.ondramanice.tv/drama/hot-blooded-priest-detail
  2. https://quickdrama.com/series/the-fiery-priest/
  3. https://kissasian.sh/Drama/The-Fiery-Priest
 
kabisa vita itakuwa ni kubwa sana, halafu kwenye preview mr president amemrudisha madarakani yule mama mwenye bifu na chae sira (madam jami kwenye emperor of the sea).
huenda mr president anataka kumsambaratisha yule mama na mapemaaa kwa kutumia mtego wa kumrudisha madarakani, si umeona auditor noh amekwenda kufanya ukaguzi wa ghafla kwenye ofisi yake mpya.
au labda macho yangu yana makengeza hivyo basi pengine sipo sahihi.
 

Geeeez! Hivi kweli Damushin hujaniambia kama Kim Nam Gil ana project mpya mpaka inataka kuisha jamani? Yani na kulia kote alivyokwenda jeshini? [emoji24][emoji24][emoji24]
Sijui nimekuwaje? Hili ni kosa kubwa kukosa drama ya Bidam bae...
Tena na hivi Oppa Song anazingua itabidi nimfanyie ‘sub’ na Bidam, no way.

Ngoja nimalize The Great Seer niianze hii fasterrrr, Sambong isubiri kwanza.
Bidam first [emoji4]


Sent from my iPhone using JamiiForums
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…